Close

Results 1 to 2 of 2
 1. #1
  Senior Member
  Join Date
  Jan 2014
  Posts
  2,227
  Rep Power
  9
  Likes Received
  73
  Likes Given
  3

  NINI TOFAUTI YA ALICHOKIPIGANIA MZEE AKILIMALI WA YANGA NA DK. SLAA WA CHADEMA?

  Sote tunajua Sakata la Clabu ya mpira ya Yanga kutaka kukodishwa kwa Mfanyabiashara Yusufu Manji.

  Ni Mzee maarufu na mwanachama wa siku nyingi wa timu hiyo kongwe Kabisa, Yahaya Akilimali ndiye aliyeongoza kupinga mpango huo uliokuwa na lengo la kuiondoa timu kutoka kumlikiwa na wananchama kwenda kwa* mtu binafsi bila ya kuwa na mkataba unaoelelweka. Katika utetezi wake, mzee Akilimali alisema:

  1. YANGA haiwezi kukodishwa kama viti

  2. Haiwezekani kuwepo na YANGA mbili yaani, Yanga asili na Yanga Kampuni.


  Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya RICHMOND na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Edward LOWASSA wakati anahamia CHADEMA* yapo mambo mengi yalisemwa lakini kubwa ni lile la kwamba LOWASSA aliuziwa CHAMA jambo lililowapa wasiwasi Wanachama na wapenzi wa Chadema kuwa huwenda CHADEMA ikagawanyika kuwa CHADEMA asili yaani CHADEMA ya M4C iliyokuwa yenye MRENGO wa Kupiga vita UFISADI* na CHADEMA ya ULIPO TUPO, yaani CHADEMA ya 4U MOVEMENT, Chadema yenye mrengo wa KIMTANDAO* na yenye KUKUMBATIA MAFISADI.


  Tayari kuna dalili kuwa CHADEMA ya ULIPO TUPO ndiyo iliyochukua hatamu

  Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema ambaye siyo kiongozi anaweza kukaa meza kuu yaani HIGH TABLE ni Edward Lowassa. Aidha tayari HEMEDI ALI, mwana 4U MOVEMENT ameshachukua nafasi ya MKUU WA IDARA YA UENEZI ya CHADEMA Taifa. Hayo ni baadhi tu ya Mambo yanayodhihirisha dalili za CHADEMA YA ULIPO TUPO kuichukua CHADEMA juu kwa juu.


  Mytake: Alichokipigania Mzee YAHAYA AKILIMALI kuirudisha YANGA kwa wanachama kina tofauti gani na alichokuwa* anakipigania DK. SLAA CHADEMA?* Kuna uwezekano wa kuibuka kwa VITA kati ya CHADEMA ya M4C na Chadema ya 4U MOVEMENT? WANANCHI Bado wana imani na CHADEMA? NGUVU KUBWA inayotumika kumshambulia RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, D.k John Pombe Magufuli aliyejipambanua toka mwanzo kupambana* na UFISADI lakini akaambiwa ni NGUVU YA SODA inatoka katika Mtandao wa MAFISADI unaoanza kuota mizizi taratobu ndani ya CHADEMA baada ya kuona nguvu ya rais Magufuli siyo ya SODA bali nguvu ya BIA?

 2. #2
  Senior Member
  Join Date
  Aug 2014
  Posts
  2,379
  Rep Power
  8
  Likes Received
  144
  Likes Given
  164

  Re: NINI TOFAUTI YA ALICHOKIPIGANIA MZEE AKILIMALI WA YANGA NA DK. SLAA WA CHADEMA?

  Ni baada ya mbinu ya kuwagawa kikabila na kidini kushindwa,sasa unakuja na UHARO wako wa M4C na 4U Movement.

  Kwa jinsi CCM ilivyooza,ningetamani ashuke shetani“LUSIFA”aje atusaidie KUIFUTA CCM

Posting Permissions

 • You may not post new threads
 • You may not post replies
 • You may not post attachments
 • You may not edit your posts
 •