Jeshi la polisi mkoani Arusha linajipanga kumkamata mbunge wa Arusha Mjini na Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha leo usiku au alfajiri sana kesho

Taarifa za uhakika zinasema kuwa polisi wanashinikizwa na Mkuu wa mkoa wa Arusha Bwana Mrisho Gambo kumkamata mbunge huyo kutokana na mgogoro mkubwa uliopo kati ya wawili hao.Shinikizo la RC Gambo limewachukiza baadhi ya maofisa wa polisi hasa kitengo cha upepelezi kwa kuwa wao polisi hawana sababu ya kumkamata,hata hivyo Bwana Mrisho Gambo amesisitiza kuwa lazima wakamatwe kutokana na kile yeye RC anachodai kuwa Mbunge amemkosea yeye binafsi na mh Rais.

Katika mikutano ya hadhara aliyofanya mbunge pamoja na madiwani akiwepo Mstahiki meya walitangaza kutompa ushirikiano wowote RC na DC kwa kile walichoita matumizi mabaya ya madaraka yanayofanywa na RC na DC.Tamko hilo limeungwa mkono na wananchi mbalimbali katika jiji la Arusha na viunga vyake.Kufuatia uungwaji mkono huo RC amekosa amani na imani ya kutembea bila ulinzi mkali wa polisi.

Itakumbukwa kuwa mke wa Mh. Mbunge wa Arusha mjini Bi. Neema Lema alishikiliwa na jeshi la polisi kwa masaa manne juzi Jumatano wiki hii Octoba 26 . Neema Lema alishikiliwa kwa amri ya mkuu wa mkoa wa Arusha Bwana Mrisho Gambo! Inadaiwa kuwa Neema amekuwa nguzo kuu ya ujasiri wa mumewe na katika kila hatua amekuwa na mchango mkubwa sana kwa mumewe ambaye ni mbunge aliyechaguliwa kwa zaidi ya kura 65,000. Taarifa zinazidi kusema kuwa mkuu wa mkoa amechukizwa na kitendo cha line ya simu ya Mbunge kuwa na jina la Neema ambaye ni mkewe.

Baada ya kuhojiwa kuhusu line inayohisiwa kutuma sms yenye neno *Shoga* Bi Neema Lema alikana kuhusika na kumiliki line iliyotuma sms hiyo,hata hivyo alisema neno Shoga sio tusi bali ni rafiki,na akatoa mfano kuwa kwa utamaduni wa wanawake huitana Shoga!
Baada ya kushikiliwa kwa muda wa masaa manne Bi. Neema ametolewa bila masharti, wala bila kuwa na kesi yoyote ya kujibu.

My take
RC acha kutumia madaraka vibaya,je ni hasira ya kuzomewa kula burka ulikotaka kupotosha umma?Je ni hasira ya hotuba kali za Mbunge?Hizi hotuba zinaeleza ukweli?je utaweza kushindana na Ukweli?
Kamwe mtu aliyeteuliwa na mtu mmoja hawezi kushinda mbunge mwenye kura 65,000 ni swala la muda tu