Close

Results 1 to 5 of 5
 1. #1
  Senior Member Kansiime's Avatar
  Join Date
  Feb 2015
  Posts
  358
  Rep Power
  6
  Likes Received
  12
  Likes Given
  36

  Rais Magufuli kueleza Utendaji wake wa Mwaka MMOJA live TBC1 na Azam Ijumaa Nov 4

  Wadau, amani iwe kwenu.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Joseph Magufuli atazungumza na taifa moja kwa moja yaani live aka Mubashara kupitia vyombo vya habari Ijumaa Novemba 4, 2016. Miongoni mwa vyombo vya habari vitakavyorusha matangazo hayo ni Azam TV na TBC1. Pia vyombo vingine vya habari vitarusha matangazo hayo kupitia channel hizo.

  Yapo mengi ambayo naamini Rais wetu atayazungumza. Naamini kuwa Rais atazungumzia jinsi alivyofanikiwa kurejesha nidhamu serikalini, kuokoa fedha nyingi zilizokuwa zinapotea kutokana na HEWA kuwa nyingi kama kwenye mikopo, watumishi, wanafunzi nk

  Naamini pia kuwa Rais atazungumzia kwa nini yeye hasafiri sana lakini anakaribisha wageni wengi kuja nchini. Miongoni mwao ni pamoja na Marais wa Rwanda, Uganda, DRC, Mfalme wa Morocco pamoja na mkutano wa Mabohora. Rais atazungumzia manufaa ya ziara hizo kwa taifa ijapokuwa miongoni mwa hizo ziara zilipewa kisogo na vyombo vya habari.

  Vilevile ni imani yangu kuwa Rais wetu atazungumzia mambo aliyojifunza katika mwaka mmoja wa utawala wake

  Pia natarajia Rais ataeleza changamoto zilizojitokeza wakati akileta mabadiliko ya kweli katika nchi yetu. Moja ya changamoto ni zile zilizojitokeza wakati wa utoaji wa elimu bure ambapo baadhi ya watu walianza kuingiza wanafunzi hewa. Pia changamoto hizo zimejitokeza wakati wa utoaji mikopo kwa wanafunzi ambapo amebaini hakuna coordination baina ya TCU, Bodi ya Mikopo na Vyuo ambapo inatarajiwa kuwa atatangaza rasmi utaratibu wa vyuo vikuu vyote kufunguliwa kwa siku moja.

  Pia Rais anatarajiwa kueleza miradi mikubwa ambayo Serikali yetu inatekeleza. Miongoni mwa miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa Bomba la Mfuta kutoka Hoima Uganda hadi Tanga. Pia ujenzi wa Reli ya Kati kwa Standard Gauge. Pia ujenzi wa Bomba la Mafuta kutoka DRC kuunganisha na Bomba la Uganda. Vile vile ataeleza mkakati wa Serikali katika kupanua miundombinu ya nchi ikiwemo barabara, reli, bandari na viwanja vya ndege. Ununuzi wa ndege ni miongoni mwa mambo ambayo naamini hatasahau kuelezea

  Ijapokuwa Rais wetu ana muda wa mwaka mmoja tu, amefanya mambo mengi makubwa na ambayo naamini atapata fursa ya kueleza kupitia kikao hicho na waandishi wa habari.

  Naamini pia waandishi wa Habari watapata fursa ya kumuuliza maswali ili kuomba ufafanuzi wa masuala kadhaa.

  Haya nimeyawaza tu kutokana na jinsi ninavyofuatilia mwenendo wa serikali ya awamu ya tano.

  Ka wale ambao vifurushi kwenye ving'amuzi vyao vimeisha, huu ni wakati wa kulipia ili usikose uhondo siku hiyo.

 2. #2
  Senior Member
  Join Date
  Aug 2014
  Posts
  2,379
  Rep Power
  8
  Likes Received
  144
  Likes Given
  164

  Re: Rais Magufuli kueleza Utendaji wake wa Mwaka MMOJA live TBC1 na Azam Ijumaa Nov 4

  Habari ya MUJINI kwa sasa ,ni MSWADA WA HOVYO WA HABARI unaotaka kupitishwa na hiyo “SAKOSI” YENU huko Dodoma.

  Mawaziri Wakuu Wastaafu,watetezi wa wanyonge watakuwa viunga hivyo kutoa somo kwa vijana wao.
  Last edited by Nyaluhala; 31-10-2016 at 12:10.

 3. #3
  Senior Member
  Join Date
  Aug 2015
  Posts
  2,802
  Rep Power
  7
  Likes Received
  89
  Likes Given
  66

  Re: Rais Magufuli kueleza Utendaji wake wa Mwaka MMOJA live TBC1 na Azam Ijumaa Nov 4

  Ccm mbele kwa mbele ataongea upuuzi tu ......

 4. #4
  Senior Member GURU's Avatar
  Join Date
  Aug 2014
  Location
  Gangstarr
  Posts
  906
  Rep Power
  6
  Likes Received
  26
  Likes Given
  41

  Re: Rais Magufuli kueleza Utendaji wake wa Mwaka MMOJA live TBC1 na Azam Ijumaa Nov 4

  Akimaliza tutawaomba wazee wa KULALAMIKA na KULIALIA wafanye tathimini yao ya Mwaka mmoja wa KULIZWA.

 5. #5
  Senior Member
  Join Date
  Aug 2014
  Posts
  2,379
  Rep Power
  8
  Likes Received
  144
  Likes Given
  164

  Re: Rais Magufuli kueleza Utendaji wake wa Mwaka MMOJA live TBC1 na Azam Ijumaa Nov 4

  Isije ikawa NAYEYE ASHAYAJUWA MASWALI ya kuulizwa kama ilivyokuwa kwa Hillary Clinton.

Posting Permissions

 • You may not post new threads
 • You may not post replies
 • You may not post attachments
 • You may not edit your posts
 •