Close

Results 1 to 5 of 5
 1. #1
  Member
  Join Date
  May 2015
  Posts
  33
  Rep Power
  0
  Likes Received
  6
  Likes Given
  0

  MHESHIMIWA RAIS WANANCHI WA KINONDONI WAMEKUKOSEA NINI?

  Mheshimiwa Rais,kwanza nikutakie heri ya kuzaliwa kama wanavyofanya wengine,nimeona nitumie siku hii unapofurahia na kula na kunywa basi ujue kuna watu wako MANISPAA YA KINONDONI wanasimanzi,majuto na chuki kubwa sana dhidi yako.

  Mheshimiwa Rais huenda wasitokee wakukwambia ukweli kama mimi,waliokuzunguka wanapenda kukuona unafurahi wakati wote na wanatafuta tabasamu lako hata kwa gharama za maisha au uhai wa watu wengine.

  Mheshimiwa Rais leo nakuandikia ujumbee huu nikiwa nimetuliza mizuka,jazba,hasira nilizo nazo juu ya mwenendo wa serikali yako na chama chako,ndiyo maana naandika ikiwa ni siku 6 tangu MAHARAMIA WA DEMOKRASIA WAVAMIE manispaa ya kinondoni.

  Mheshimiwa Rais manispaa ya kinondoni walishafanya maamuzi ya kutaka nani na wa chama gani awaongoze kwa miaka 5 ijayo na kwa fulsa hiyo ndiyo inakufanya na wewe uwe IKULU bila bugza huku ukitimiza uliyowaahidi Watanzania.

  Mheshimiwa Rais wapinzani waliopewa ridha ya kuongoza sehemu mbali mbali tumekuwa kila siku tukikulalamikia juu hujuma wanazofanyiwa mameya wa UKAWA wasio ccm na wabunge pia,lakini kwa bahati mbaya hukuwahi kujitokeza hadharani kukemea au kukana kuhusika na mipango ovu yakukwamisha maendeleo pale walipochaguliwa wapinzani.

  Mheshimiwa Rais (style) yako tunaijua vizuri sana, sisi si watoto wadogo kwakuwa unajua palipo na utulivu,umoja na mshikamano basi panamaendeleo,hapo ndipo unapotumia rungu lako la uteuzi kutuletea wavuruga (VIVURUGE)amani na mshikamano ili wapinzani tukwame,lakini tunajiuliza mbona hatujawahi kuona halmashauri za CCM au mameya,au wabunge wa ccm wakifanyiwa dhihaka,vurugu,na kila aina ya hujuma kama wanapoongoza wapinzani? Jibu nikuwa wametumwa kazi maalum.

  ONA manispaa ya kinondoni,Mheshimiwa Rais,wananchi walikuwa wanaishi kama wapo peponi miezi 8 chinibya chaguo la lao kipenzi (UKAWA) Na maamuzibya nani aongoze halmashauri yao walisha yafanya tangu october 2015MHESHIMIWA RAIS WANANCHI WAKINONDONI WAMEKUKOSEA NINI?

  Mheshimiwa Rais,kwanza nikutakie heri ya kuzaliwa kama wanavyofanya wengine,nimeona nitumie sikuu hii unapofurahia na kula na kunywa basi ujue kuna watu wako MANISPAA YA KINONDONI wanasimanzi, Majuto na chuki kubwa sana dhidi yako.

  Mheshimiwa Rais huenda wasitokee wakukwambia ukweli kama mimi tuh,waliokuzunguka wanapenda kukuona unafurahi wakati wote na wanatafuta tabasamu lako hata kwa gharama za maisha au uhai wa watu wengine.

  Mheshimiwa Rais leo nakuandikia ujumbee huu nikiwa nimetukiza mizuka,jazba,hasira nilizo nazo juu ya mwenendo wa serikali yako na chama chako ndiyo maana naandika ikiwa ni siku 6 tangu MAHARAMIA WA DEMOKRASIA WAVAMIE manispaa ya kinondoni.

  Mheshimiwa Rais manispaa ya kinondoni walishafanya maamuzi ya kutaka nani na wachama gani awaongoze kwa miaka 5 ijayo na kwa fulsa hiyo ndiyo inakufanya na wewe uwe IKULU bila bugza huku ukitimiza uliyowaahidi Watanzania.

  Mheshimiwa Rais wapinzani waliopewa ridha ya kuongoza sehemu mbali mbali tumekuwa kila siku tukikulalamikia juu hujuma wanazo fanyiwa mameya wa UKAWA wasio ccm,na wabunge pia lakini kwa bahati mbaya hukuwahi kujitokeza hadharani kukemea au kukana kuhusika na mioango ovu ya kukwamisha maendeleo pale walipo chaguliwa wapinzani.

  Mheshimiwa Rais taili yako tunajua vizuri sana, sisi si watoto wadogo kwakuwa unajua palipo na utulivu,umoja na mshikamano basi panamaendeleo,hapo ndipo ubaootumia rungu lako la uteuzi kutuletea wavuruga amani na mshikamano ilibwaoinzani tukwame lakini tunajiuliza mbona hatujawahi kuona halmashauri za CCM au mameya,au wabunge wa ccm wakifanyiwa dhihaka,vurugu,na kila aina ya hujuma kama wanapoongoza wapinzani? Jibu nikuwa wametumwa kazi maalum

  ONA manispaa ya kinondoni,Mheshimiwa Rais,wananchi walikuwa wanaishi kama wapo peponi mismezi 8 chini ya chaguo lao kipenzi (UKAWA) Na maamuzi ya nani aongoze halmashauri yao walishayafanya tangu october 2015.

  Inatumika nafasi ya kugawanya halmashauri kama njia ya kuleta vurugu rasmi kwa wananchi wa manispaa ya kinondoni,swali mbona Temeke imegawanywa na namba ziko wazi UKAWA hawaleti vurugu? Au kwakuwa hawana Dola? Au kwakuwa hawana polisi na mahakama? Au kwakuwa wasimamizi wa hizi chaguzi hawateuliwi na UKAWA?

  Mheshimiwa Rais wananchi wa manispaa ya kinondoni wanajua kuwa linalotafutwa pale si UKAWA watafanya nini? Bali ni kwamba:-

  1.Manispaa ya kinondoni isitawalike tena.

  2.Wawakilishi,wabunge na madiwani wajikite kwenye mgogoro uliopandikizwa makusudi waache kujadili maendeleo.

  3.Kuvuta muda uende ili miaka 5 ipite bila mandeleo ya maana kwa wananchi.

  4.kutuonyesha jeuri ya Dola kwamba CCM ndiyo wanaotoa Amri,hatuna chakufanya mbele ya bunduki na magereza.

  Mheshimiwa Rais nakukumbushaa tena kwakufanya hivyo uwakomoi Wapinzani hata kidogo(UKAWA) bali unaowapa adhabu ni wananchi wanyonge waliomaua kwa ridhaa yao kuwa waongozwe na UKAWA kwa miaka 5.

  Mheshiniwa Rais nakukumbusha tena kuwa kwakufanya hivyo utuondoi kwenye mioyo ya wananchi waliochagua wapinzani bali unapandikiza chuki juu yako na ccm yako kwa ujumla,si uliona Arusha kilichotokea? Mandeleo yalisimamishwa na mgogoro wa kupandikiza kwa miaka 5,lakini wananchi waliwaadhibu CCM kwakuwafuta kabisa kwenye halmshauri ya jiji la Arusha leo wanadiwani mmoja.Wananchi si wajinga hata kidogo wanaona yanayotendeka.

  Mheshimiwa Rais mtego mlioweka KINONDONI utawatega nyinyi wenyewe CCM, wala si wapinzani,(swala la muda tu)

  Mheshimiwa Rais tunajua unajua kuwa Meya wako ana wajumbe 11 tu wengine mawaziri 4,naibu spika 1. Na mbunge 1

  1.prof makame mabalawa
  2.Maiga
  3.Angela kairuki
  4.Ndalichako
  5.Akson Tulia

  Mbunge
  1.Amina mwakilagi

  Mheshimiwa Rais tunajua kuwa unafahamu hata wewe Meya wako hatokuwa na uwezo wakuitisha kikao halali,isipokuwa ni kutuonyesha mkiamua chochote kinawezekana.

  Tunajua unafahamu hakuna tena maamuzi halali ya baraza ya kisheria meya wako anaweza kuyafikia kwa idadi yake ndogo ya madiwani huku madiwani 20 wakiwa nje ya halmashauri.

  Mheshimiwa Rais hakuna kikao sasa manispaa ya kinondoni kitafanyika watu 11 waongoze watu 20,kwakuwa mawaziri na wabunge na naibu spika watakuwa bungeni na kwenye majukumu mengine.

  Mheshimiwa Rais maharamia wademokrasia wamefanya makusudi kutuletea mgogoro usio wa msingi,huku wakijua CCM wana "KINO" na ukawa wana "NDONI" hakuna mshindi kati yetu na maharamia wa demokrasia....wakemee wairudishe "KINO" Tuendelee na KINONDONI 1.

  Mheshiwa Rais,nimeandika kwako ushauri huu wa wazi si kama kukufundisha kazi la hasha, bali kukumbusha kuwa unapaswa utende sawa na maneno yako, ambayo maranyingi umekuwa ukiyasema hadharani,kuwa maendeleo hayana chama,uchaguzi umeisha tujenge nchi, basi tunakuomba kupitia maneno yako wananchi wakinondoni wapewe haki yao na heshima yao ya kuchagua upinzani kama ambavyo Temeke wameichagua ccm na hakuna wakuisumbua,wewe ukiamja unaweza kuwakemea maharamia wa demokrasia wache na wakaacha kwakuwa wengi wao umewateua wewe.

  Mheshimiwa Rais mkurugenzi na watendaji wake siyo wajinga wanajua kipindi hiki cha mgogoro na mvutano usio wa lazima baina yetu na maharamia wa demokrasia wao nikipindi cha neema kwao, kipindi cha kutumia fedha bila usimamizi, kipindi cha kujiibulia miradi hewa kwakuwa viongozi wana mgogoro, kwa mantiki hiyo wamefanya makusudi kuachia ubakaji mkubwa wa demokrasia.

  Mheshimiwa Rais, vifua vyenye hasira na chuki juu yako na chama chako ni laana kwa utawala wako,hatuna Dola lakini tunaye Mungu wa kumlilia tunapoona uonevu umezidi kikomo.Mwambie Meya wako kuwa Baba yake alishatuuumiza kwa kuvuruga mchakato wa katiba mpya kabla hatujamsamehe na yeye anafanya kosa kubwa maishani mwake kwa kuivuruga Manispaa ya kinondoni,mwambie mkurugenzi wako kuwa hatukuwa na uwezo wakuchagua nani awe mkurugenzi,bali tumefanya kazi na makada wako kwa kuwa hatuna jeuri dhidi ya uteuzi wako.

  MWISHO
  Mheshimiwa Rais,wananchi wa kinondoni wamekukosea nini,mbona ghafla umewakatisha ndoto zao za kupata utumishi uliotukuka kwa wabunge waliowachagua?, mbona ghafla umekatisha matumaini walipoanza kuyaona maendeleo ya shughuli zao za kila siku? Mbona umeacha maharamia wa demokransia waivunjevunje vipande manispaa iliyokuwa ni mfano wa kuigwa popote.? Hatuna Dola lakini tunaye Mungu wa kumlilia yote haya.

  Na BONIFACE JACOB
  EX MAYOR
  Manispaa ya Kinondoni

 2. #2
  Senior Member
  Join Date
  Aug 2014
  Posts
  2,379
  Rep Power
  7
  Likes Received
  144
  Likes Given
  164

  Re: MHESHIMIWA RAIS WANANCHI WA KINONDONI WAMEKUKOSEA NINI?

  Inaumiza sana sana.Watu wanaponyang'anywa haki yao ya kuongozwa na watu waliowachaguwa,INAUMIZA SANA.

 3. #3
  Senior Member
  Join Date
  Jun 2015
  Posts
  722
  Rep Power
  4
  Likes Received
  23
  Likes Given
  1

  Re: MHESHIMIWA RAIS WANANCHI WA KINONDONI WAMEKUKOSEA NINI?

  huo uhalisho usiletwe Ubungo ubaki hukohuko kinondoni maana panaweza kujengeka badala ya kuchimbika siasa za kifedhuli naman hiyo hatutaki kila mtu atajikomboa mwenyewe atapigana mwenyewe mateso yakizidi hakuna atakaye vumilia CCM haina siafa ya kuongoza tena ni wahuni na majambazi
  punda hajasoma lakini kazi hakosi

 4. #4
  Senior Member mahakama ya kadhi's Avatar
  Join Date
  Jan 2014
  Posts
  993
  Rep Power
  5
  Likes Received
  31
  Likes Given
  31

  Re: MHESHIMIWA RAIS WANANCHI WA KINONDONI WAMEKUKOSEA NINI?

  Nyie wahuni msiojitambua hebu nyamazeni wanaume wafanye kazi nyie kaeni vibarazani mle chapati na supu za utumbo wa kuku.

 5. #5
  Senior Member KISIKI's Avatar
  Join Date
  May 2014
  Posts
  2,831
  Rep Power
  7
  Likes Received
  171
  Likes Given
  339

  Re: MHESHIMIWA RAIS WANANCHI WA KINONDONI WAMEKUKOSEA NINI?

  Wewe mahakama ya kadhi unajiropokea tu na hizi ni athari za kutumika kinyume na maumbile.

Posting Permissions

 • You may not post new threads
 • You may not post replies
 • You may not post attachments
 • You may not edit your posts
 •