Close

Results 1 to 7 of 7
 1. #1
  Senior Member
  Join Date
  Jan 2014
  Posts
  2,867
  Rep Power
  7
  Likes Received
  76
  Likes Given
  130

  Zitto Kabwe ashtakiwe kutokana na ufisadi huu wa NSSF

  Wakati Ufisadi wa viwanja Kigamboni unafanyika, Zitto Kabwe alikuwa Mwenyekiti wa PAC. Iweje Zitto asione madudu hayo ambayo hayakuhitaji darubini kuyaona?

  Wakati Ufisadi wa viwanja kigamboni unafanyika, Ramadhan Dau, swahiba na mfadhili mkubwa wa Zitto na ACT ndiye aliyekuwa Mkurugenzi wa NSSF. Unafikiri Zitto alishindwa kuuona ufisadi kwa bahati mbaya, kukosa uelewa ama aliona lakini akapuuzia kwa vile tu ulihusu wafadhili wake?

  Iweje Zitto Kabwe aone ufisadi kwenye mambo mengine kama ule wa Meremeta lakini asione hili la Vianja vya Kigamboni?

  Yapo maswali ya kumuuliza Zitto Kabwe juu ya sakata hili. Nikiangalia kwa jicho la tatu sioni ataponea wapi. Sasa ndio najua kwa nini kulikuwa na sekeseke kubwa wakati wa uundwaji wa kamati za bunge.

  Zitto my brother. Kwa hili umechemsha na umeharibu kabisa taswira yako. Hakuna atakayekuamini tena utakapojenga hoja zako uchwara. Vyombo vya dola mchukulieni hatua huyu Zitto Kabwe. Kwa kuanzia, anzeni pale alipopendekeza Ole Sendeka. Chunguzeni mali zote za Zitto na aeleze amezipataje. Kwa bahati nzuri zinafahamika mpaka zile alizoandikisha umiliki kwa majina mengine. Anzieni hapo.

  Ahsante Ole Sendeka kwa kutuzindua juu ya hili. Kumbe hawa wanaopiga kelele dhidi ya Rais Magufuli ni wale ambao mirija yao imekatwa! Kama ni hivyo ni bora Rais wetu awe na maadui wengi katika kusimamia haki kuliko kuwa na marafiki wengi katika kufisidi nchi.

 2. #2
  Senior Member KISIKI's Avatar
  Join Date
  May 2014
  Posts
  2,831
  Rep Power
  7
  Likes Received
  171
  Likes Given
  339

  Re: Zitto Kabwe ashtakiwe kutokana na ufisadi huu wa NSSF

  Mzee wa minyoo hana ishu alikua anatoa mvuke tu, lipeni mishara ya UPL kwanza.

 3. #3
  Senior Member
  Join Date
  Aug 2014
  Posts
  2,379
  Rep Power
  7
  Likes Received
  144
  Likes Given
  164

  Re: Zitto Kabwe ashtakiwe kutokana na ufisadi huu wa NSSF

  Zitto yupi?.Huyu aliyekuwa anawasaidia(CCM) kuiangamiza Chadema.Kweli shukrani ya PUNDA NI MATEKE.Hiyo PAC yenyewe mlimpandikiza wenyewe?.Sasa mnalia lia nini?.

  Mbwiga nyie.

 4. #4
  Senior Member GURU's Avatar
  Join Date
  Aug 2014
  Location
  Gangstarr
  Posts
  906
  Rep Power
  5
  Likes Received
  26
  Likes Given
  41

  Re: Zitto Kabwe ashtakiwe kutokana na ufisadi huu wa NSSF

  KINYONGA asubiri kukatiwa utepe kwenye Mahakama yetu Pendwa ya Mafisi Mafisadi. Stay tuned

 5. #5
  Senior Member
  Join Date
  Aug 2015
  Posts
  2,802
  Rep Power
  6
  Likes Received
  89
  Likes Given
  66

  Re: Zitto Kabwe ashtakiwe kutokana na ufisadi huu wa NSSF

  Yaani leo hii mnataka mmgeuke kibaraka wenu Zitto ...... hama kweli mafisiem hamna maana

 6. #6
  Senior Member
  Join Date
  Aug 2014
  Posts
  2,379
  Rep Power
  7
  Likes Received
  144
  Likes Given
  164

  Re: Zitto Kabwe ashtakiwe kutokana na ufisadi huu wa NSSF

  Quote Originally Posted by GURU View Post
  KINYONGA asubiri kukatiwa utepe kwenye Mahakama yetu Pendwa ya Mafisi Mafisadi. Stay tuned
  Hizo hela walimpa wenyewe.Kwa kutumia tu akili za chekechea,inawezekana vipi Chama(ACT-Wazalendo)kichanga kikaingia kwenye Uchaguzi Mkuu halafu kikaweka wagombea ubunge nchi nzima.Hizo hela walizipata wapi?.Labda wangeanza kuhoji kipindi hicho tungewaelewa.Hizo kelele kuhusu Zitto sasa,ni matokeo ya KUSHINDWA KWA MRADI WAO wa kuiangamiza Chadema kupitia Zitto.Wameona hana faida kwao.WANAMLIPUA KWA HELA WALIZOMPA WAO WENYEWE.

  Wapeleke huo UPUUZI WAO HUKO LUMUMBA.

 7. #7
  Senior Member mahakama ya kadhi's Avatar
  Join Date
  Jan 2014
  Posts
  993
  Rep Power
  5
  Likes Received
  31
  Likes Given
  31

  Re: Zitto Kabwe ashtakiwe kutokana na ufisadi huu wa NSSF

  Zitto na Lowasa hawataweza kuchomoka kwenye ufisadi huu sasa imefika wakati wa kutandikana bila aibu zitto lazima awajibike tu.

Posting Permissions

 • You may not post new threads
 • You may not post replies
 • You may not post attachments
 • You may not edit your posts
 •