Inawezekana mtu mmoja au kikundi cha watu wachache wakajipanga kwa nguvu kadri watakavyoweza lakini hawataweza kuficha ukweli kama ulivyo.Nazungumzia bodi ya Uongozi ya Chuo cha Ufundi Arusha ambayo imegeuka majanga kwa Chuo hiki. Mtu anaweza akafanya kila aina ya uovu na kufanya kila aina ya mbinu ili kuficha uovu huo lakini siku moja uovu huo utajulikana tu, Hii ni bodi ya Uongozi ya Chuo cha Ufundi Arusha. Hata hivyo, hebu tujiulize tunafanya uovu wote huo kwa faida ya nani? Mtu anadhulumu kutoa elimu iliyo bora kwa watanzania wenzake masikini ili apate kuwa na fedha nyingi sana ili imsaidie nini? Mtu anafikiria kuiba kila senti ya umma ili iweje? Wakati huohuo mtu huyohuyo anatumia nguvu kubwa ya kila aina ili kuficha uovu huo bila aibu.

Habari za ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka vimekuwa vikiripotiwa kwenye vyombo mbalimbali vikiwepo vyombo vya habari pamoja na mamlaka za kiserikali. Taarifa za uhakika zinaonyesha kwamba Tangu Mkuu wa chuo hicho Mr/Dr Richard Masika Mushi afike Chuo cha Ufundi Arusha amekuwa akitumia fedha ya Chuo na umma kama hazina mwenyewe. Mkuu huyu ameshangaza wafanyakazi wengi kwani amekuwa akiendesha Chuo kwa Usiri mkubwa akiwa hataki mfanyakazi yeyote atakayehoji jambo lolote analoona linaenda isivyo halali. Mfanyakazi yoyote anayetaka kujua habari za mapato na matumizi ya Chuo amekuwa adui yake na hata uongozi mzima wa Chuo kwa ujumla.

Maendeleo ya pahala popote yanahitaji collective Responsibility na uwazi ili kila mtu achangie kwa kadri ya uwezo wake. Ni mara nyingi kumekuwa na vikao vya bodi na hata siku mbili zilizopita Bodi ya Chuo ilikaa kikao lakini hakuna hata mfanyakazi mmoja anayejua nini kinachojadiliwa na Bodi hii. Cha ajabu ni kwamba hata wawakilishi wa Wafanyakazi na Wanafunzi wamekuwa wakificha yanayojadiliwa kwenye bodi pindi wenzao wanapotaka kujua yaliyojadiliwa. Kuna habari kuwa, kwa sasa Chuo kinakabiliwa na uhaba mkubwa wa fedha kiasi kwamba hata training materials zinasumbua na hata inasemekana chuo kinakabiliwa na madeni mengi ya nje na ndani, huku hela za vikao vya bodi ya Chuo (wengi wakiwa ni wachagga) zikipatikana pindi wanapokaa vikao.

Sisi wafanyakazi ambao pia ni wazazi kwa upande mmoja au mwingine, inatuuma sana. Hii ni kwa sababu tunajua kuwa hizi hela zinazoliwa kiholela ni za wazazi wasiojiweza na wanaofunga mikanda kulipia watoto wao karo hapa Chuoni. Badala ya karo hizo kufanya yaliyokusudiwa, zinatumiwa na watu wachache kukaa vikao visivyo na tija, kusafiria, kuhonga baadhi ya vyombo vinavyokuja kutaka kujua ukweli ili kuficha ukweli huo. Imefika pahala pa kutisha kwani katika kutaka kusisikike malalamiko yeyote hapa Chuoni, hadi wanafunzi wamekuwa wakiongezewa maksi na uongozi wa Chuo kwa siri isivyo halali na hivyo kuleta mtafaruku usio na lazima. Waalimu wanajiuliza, wanafunzi wanapofeli nini muafaka ni kuongeza maksi kwa siri tena kwa baadhi ya wanafunzi au ni kurudia mitihani kwa waliofeli ambapo huo ndio utaratibu katika vyuo vyote vya elimu ya juu?

Wafanyakazi tumefika pahala tumejisikia vibaya sana kwani, inatia uchungu pale tunapoona vyuo vya wenzetu vikipiga hatua, lakini Chuo Cha Ufundi Arusha ni kama vile hakiendi kwa sababu ya aidha mtu mmoja au watu watatu walioko kwenye uongozi wakishirikiana na inayoitwa Bodi ya Chuo kukwamisha kila kitu kwa ajili ya maendeleo ya Chuo na Taifa kwa ujumla wake. Haya ni baadhi ya mambo tu, yanayosikitisha na ambayo wafanyakazi tunakatishwa tamaa sana kuona kuwa yameweza kufanywa na uongozi wa Chuo kinyemela kwa nia ya kujinufaisha binafsi;

Miradi mingi ya ujenzi ilijengwa kwa gharama zaidi ya thamani halisi ya jengo. kwa mfano zaidi ya TZS 300,000,000/= zinakadiriwa kuliwa katika ukarabati wa Jengo la Utawala, Zaidi ya TZS 1,500,000,000/= zililiwa katika ujenzi wa jengo la madarasa lijulikanalo kama jengo la Ujenzi na Umwagiliaji, zaidi ya 320,000,000/= zililiwa kupitia fedha za mafunzo viwandani kwa mwaka 2011/2012 - 2014/15. Akaunti ya chuo ijulikanayo kama ATC-PCB imekula zaidi ya TZS 460,000,000/= kupitia miradi hewa iliyobuniwa na uongozi wa chuo. Fedha yote hii ingeweza kujenga madarasa mangapi au ingeweza kununua madawati mangapi?

Tangu mwaka wa fedha 2010/11 Mkuu wa chuo amekuwa akilipwa tofauti na cheo chake. Kwa mfano, katika mwaka wa fedha 2013/14 Mkuu wa chuo alilipwa kiasi cha Tsh 1,183,200/= zaidi ya alivyostahili. Kwa mwaka mmoja zililipwa kiasi cha Tsh 14,198,400 ambazo zinaweza kuchukuliwa kama malipo hewa. Hali ni hiyohiyo kwa mfano tena, mwaka 2011/12 Mkuu wa chuo alitakiwa kulipwa Tsh 3,330,700/= kwa mwezi, lakini alilipwa kiasi cha Tsh 4,303,400/= kwa mwezi na hivyo kwa mwaka huo zililipwa kiasi cha Tsh 14,006,880 kama malipo hewa kwa mkuu wa chuo. Fedha yote hiyo ingeweza kununua madawati mangapi?

Sehemu kubwa ya matumizi ya fedha za chuo ni kwa ajili ya shughuli za kuendesha chuo (malipo kwa ajili ya Bodi ya chuo, malipo ya safari za uongozi wa chuo, Mafuta na matengenezo ya magari yanayotumiwa na viongozi wa chuo allowance mbalimbali za uongozi wa chuo) na siyo kwa ajili ya kufanyia mambo ya taaluma (training materials, technical materials, teaching materials nk). Kipaumbele cha chuo ni nini?

Zaidi ya TZS 3,600,000,000/= zimeliwa kifisadi, lakini Bodi ya Chuo imekuwa sehemu ya hujuma hii. Mkuu wa Chuo na wajumbe wa Bodi ni wamoja. Bodi ina wajumbe kama Lema, Makileo, Ukio, Mosha, Njau, Richard Masika Mushi na Nyahumwa akiwa school mate. Ilikuwaje wajumbe hao wakajikuta kwenye Bodi moja huku Mkuu wa chuo ni Mushi?