Close

Results 1 to 3 of 3
 1. #1
  TUA
  TUA is offline
  Senior Member
  Join Date
  Oct 2014
  Posts
  677
  Rep Power
  6
  Likes Received
  32
  Likes Given
  0

  MKUU WA CHUO CHA UFUNDI ARUSHA ABADILI SHERIA ILIYOANZISHA CHUO

  Ni katika hali inayowashangaza wafanya kazi wengi hapa Chuoni pale Mkuu wa Chuo hiki Dr Richard Masika Mushi, alipoamua kujipa Cheo tofauti na kile kilichotamkwa katika sheria iliyoanzisha Chuo cha Ufundi Arusha yaani THE NATIONAL COUNCIL FOR TECHNICAL EDUCATION (ARUSHA TECHNICAL COLLEGE) ESTABLISHMENT ORDER, GN 78/2007.

  Sheria hii iliyoanzisha Chuo ambayo ilipitishwa na Bunge la Jamhuri ya Tanzania, march 2007 inatamka wazi kuwa Mkuu wa Chuo atajulikana kama PRINCIPAL. Katika hali isiyotarajiwa mkuu huyu alipoamia tu Chuo Cha Ufundi Arusha akitokea Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam, aliamua kujiita RECTOR akimaanisha Mkuu wa Chuo tofauti na inavyotaka sheria hiyo iliyoandikwa hapo juu ambayo ndiyo iliyoanzisha Chuo.
  Mara nyingi mkuu huyu wa Chuo anapoulizwa vigezo vya yeye kujipachika Cheo ambacho hakipo katika sheria iliyoanzisha Chuo, ameshindwa kutoa maelezo na mara nyingi hugeuka mbogo, na kuwashambulia baadhi ya wafanyakazi ambao wanahoji uhalali wa jambo hili na kuwatishia kuwafukuza kazi. Mara nyingi amekuwa akijitapa kuwa yeye anaweza kufanya jambo lolote, bila kuulizwa na mtu yeyoye kwani yeye ndiye mkuu wa Chuo. Na hutishia kuwa akishamfukuza mtu, hata akishinda mahakamani atamrudisha kule wizara ya Elimu.

  Ni kweli hata wafanyakazi kada ya wanataaluma wameamini anachosema Masika kwani, yeye na menejimenti ya Chuo wamekuwa wakiwaongezea wanafunzi maksi kiholela kiasi kwamba waalimu hawathaminiki tena na wanafunzi kwa maana kwamba baadhi ya wanafunzi wanapoona wamefeli masomo huenda kuwashtaki waalimu hao kwa menejimenti na kutaka kuongezwa alama za ufaulu ambapo mara nyingi wamekuwa wakiongezewa alama za ufaulu na menejimenti. Mara nyingi mkuu huyu wa Chuo na Makamu wake wa Taaluma Ndugu Masudi Senzia wamekuwa wakiwabeza waalimu wanaokuwa na msimamo kuhusu wanafunzi waliofeli kwa kuwaambia kwa sasa Serikali inajali QUANTITY na sio QUALITY.

  Mkuu huyu wa Chuo na makamu wake bila kujali wameweza na kudiriki kuendesha taaluma kwa mitaala iliyopitwa na wakati na mingine ambayo haina ubora na ambayo haitambuliki na Baraza la Elimu ya Ufundi, NACTE. Kutokana na hali hii waalimu wengi wamekuwa wakifundisha bila kufuata miongozo ya baraza la elimu ya ufundi yaani NACTE, hali ambayo imechangia kiwango cha kufeli kwa wanafunzi. Kwa lugha nyingine ni kwamba waalimu walio wengi hufundisha jinsi wanavyojua wao na siyo jinsi ambavyo miongozo ya NACTE (CURRICULUMS) zinataka kwa kuwa Chuo hakina approved curriculums za NACTE, zaidi ya zile za mwaka 2005.

  Hali ya upatikanaji wa Training materials ni ya kubabaisha sana hasa kwa upande wa karakana za kufundishia wanafunzi hali ambayo imeshusha sana ufundishaji wa vitendo katika karakana zote. Hali hii imesababisha wanafunzi wengi kufeli sana mitihani ya Practicals. Je Serikali imekuwa mwiba tu kwa vile vyuo Binafsi kama vile ST JOSEPH na vinginevyo, ilhali Taasisi zake zingine kama hizi ni vioja?

 2. #2
  Member
  Join Date
  Jan 2015
  Posts
  44
  Rep Power
  0
  Likes Received
  0
  Likes Given
  1

  Re: MKUU WA CHUO CHA UFUNDI ARUSHA ABADILI SHERIA ILIYOANZISHA CHUO

  TAARIFA KWA UMMA
  UWEPO WA TAARIFA ZA UPOTOSHAJI
  KUHUSU CHUO CHA UFUNDI ARUSHA

  Uongozi wa Chuo cha Ufundi Arusha (ATC) unautaarifu umma wa Watanzania na Wadau mbalimbali wa Chuo kuwa, hivi karibuni kumekuwepo na taarifa za tuhuma mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii dhidi ya Menejimenti ya Chuo, Mkuu wa Chuo, Baadhi ya Watumishi na Mamlaka za Serikali.
  Aidha, Uongozi wa Chuo unapenda kukanusha na kueleza Umma kuwa, taarifa hizo hazina chembe zozote za ukweli na zinazushwa na baadhi ya Watu wachache kwa lengo la kupotosha Umma na kwa nia ya kudhoofisha ustawi mzuri wa Chuo.
  Vile vile tuhuma hizo zimeeleza kuwepo uonevu kwa baadhi ya Watumishi wa Chuo. Tunapenda Umma ufahamu kuwa, Chuo hakijawahi kumwonea Mtumishi yeyote na maswala yote yanayohusu watumishi hushughulikiwa kwa mujibu wa sheria na kanuni za Utumishi wa Umma na nchi ikiwa ni pamoja na wafanyakazi watatu (03) waliofukuzwa kazi kwa kukiuka sheria hizo na shauri lao liko kwenye Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA).
  Mwisho tunapenda kuufahamisha Umma kuwa, wakati wowote Chuo kipo tayari kutoa taarifa sahihi kwa Mamlaka zilizoko kisheria.
  Imetolewa na:
  Ofisi ya Uhusiano Chuo cha Ufundi Arusha (ATC)
  S.L.P 296, Arusha.
  Barua pepe: pro@atc.ac.tz, tovuti: www.atc.ac.t


 3. #3
  Junior Member
  Join Date
  Mar 2016
  Posts
  26
  Rep Power
  0
  Likes Received
  0
  Likes Given
  0

  Re: MKUU WA CHUO CHA UFUNDI ARUSHA ABADILI SHERIA ILIYOANZISHA CHUO

  Mpango wa Serikali kuanzisha Chuo cha ufundi Arusha ulijadiliwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lililoketi katika vikao vyake Mwezi Februari/Machi 2007. Hatimaye Bunge lilipitisha mpango huo, na hatimaye lilitoka Agizo la kuanzisha Chuo cha Ufundi Arusha na kutangazwa kwenye Tangazo la Serikali Namba 78 la 30 Machi 2007.

  Ni kupitia mamlaka hiyo iliyowekwa kisheria, Bodi ya Uongozi wa chuo ilianzishwa. Kadhalika ni kupitia mamlaka hiyo nafasi ya Mkuu wa chuo ilianzishwa. Mpaka sasa Bunge halijawahi kufuta au kubadilisha sehemu yoyote ya Agizo la kuanzisha Chuo cha Ufundi Arusha [The National Council for Technical Education (Arusha Technical College) Establishment Order, 2007].

  Kulitokea mpango usio wa Serkali ulioaminika kuwa na nia ovu ulipangwa kwa ushirikiano wa Mkuu wa Chuo Mr./Dkt. Richard Masika Mushi, aliyekuwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Elimu ya Ufundi (NACTE) Mr./Dkt Primus Nkwera na Kaimu Mkurugenzi wa Elimu ya Ufundi katika Wizara ya Elimu Mr. Thomas Katebalirwe. Katika mkakati huo wa Mkuu wa chuo wenye kila dalili za kuwa na nia ovu, NACTE ilitoa Tangazo kwenye gazeti la Serikali mwezi Julai 2015 kuwa sheria/Agizo iliyoanzisha Chuo cha Ufundi Arusha yaani GN 78/2007 imefutwa yote.

  Mwezi Septemba 2015, Mkuu wa Chuo Mr./Dkt Richard Masika Mushi kama Katibu wa Bodi ya Chuo aliwasilisha mbele ya kikao cha Bodi Taarifa kuwa Chuo kimepata sheria mpya baada ya sheria iliyokuwepo kufutwa yote. Haikuweza kufahamika mara moja kama sheria iliyotakiwa kufutwa ilikuwa na mapungufu gani.

  Nia ovu iliyokuwa imejificha katika mpango wa Mkuu wa chuo ni kutaka kuficha udhaifu kwa kushindwa kutekeleza sheria iliyoanzisha chuo inavyotakiwa. Mkuu wa Chuo na Bodi ya chuo walishindwa kutekeleza sehemu kubwa na za muhimu hivyo kulazimu mbinu ya kutaka sheria yote kufutwa bila sababu. Kwa ufupi baadhi ya yaliyoshindikana kutekelezwa ni kama ifuatavyo:
  a)Sheria inataka Bodi kwa kupata ushauri kutoka kwa Waziri wa Elimu kutengeneza kanuni kwa ajili ya uendeshaji mzuri wa chuo. Sheria husika ilihitaji kuwa kanuni zozote zitakazotengenezwa kutokana na sheria hiyo zitangazwe kwenye gazeti la Serikali. Hili halikuweza kufanyika.
  b)Sheria inataka Bodi ya chuo kuunda kamati mbalimbali kama Bodi itakavyoona inafaa, kamati hizo zikishaundwa pamoja na kazi zake ziwekwe kwenye kanuni za chuo ambazo ni lazima zitangazwe kwenye gazeti la serikali. Hili halikufanyika.
  c)Sheria inataka fedha zozote zinazolipwa chuoni kuwa mali ya chuo na kutumika katika utaratibu unaotambulika wa matumizi ya fedha za Serikali. Haifanyiki hivyo.
  d)Sheria inataka Katibu wa Bodi ya chuo kuwapa wajumbe wa Bodi taarifa na makabrasha ya kikao cha Bodi wiki mbili (2) kabla ya tarehe ya kikao cha Bodi. Haifanyiki hivyo.
  e)Sheria ninataka mmoja wa wajumbe wa Bodi ateuliwe kutoka Bodi yoyote inayofaa ya kitaalamu katika Nyanja za Sayansi na Teknolojia. Hili halifanyiki hivyo na mbaya zaidi ujumbe wa Bodi umekuwa ukitolewa kama zawadi kutoka kwa Mkuu wa chuo kwa wajumbe kujipatia fedha.

  Ikiwa mambo ya msingi kabisa yaliyotakiwa kisheria hayafanyiki, na ikiwa taratibu za kutengeneza mitaala zinafahamika vizuri lakini nazo hazifuatwi, na ikiwa inafahamika vizuri kuwa wanafunzi wa chuo wanahitaji kufundishwa sawasawa na haifanyiki hivyo na ikiwa stahili mbalimbali za wafanyakazi zinafahamika lakini hazilipwi na ikiwa hata pale ambapo kuna changamoto ya fedha safari zisizo za lazima kwa Mkuu wa chuo haziepukiki, hakuna muonekano kwamba kuna nia njema ya kuleta manufaa kwa chuo na Taifa kutoka kwa Uongozi huu wa chuo.

  Utendaji wa aina hii, unaohitaji kufuatiliwa kwa karibu na mamlaka za juu huenda ukaisumbua Serikali ya Mheshimiwa Magufuli

Posting Permissions

 • You may not post new threads
 • You may not post replies
 • You may not post attachments
 • You may not edit your posts
 •