Close

Results 1 to 14 of 14
 1. #1
  Member
  Join Date
  Feb 2015
  Posts
  32
  Rep Power
  0
  Likes Received
  0
  Likes Given
  0

  Kuna haja ya kufuatilia kwa karibu taaluma inayotolewa katika chuo hiki

  Wadau wote wa Eimu wanatakiwa kufuatilia kwa karibu mtiririko mzima wa namna taaluma inavyotolewa katika Chuo cha Ufundi Arusha. Ni jambo la kawaida kabisa kwa mhula kumalizika bila kununuliwa kwa vifaa vya kufundishia na kujifunzia.

  Ni jambo la kawaida kabisa kwa waalimu kutoingia darasani kwa sababu mbalimbali zitokanazo Uongozi wa chuo kuwapangia majukumu mengine ya kufanya huku ikifahamika kwamba wanatakiwa kufundisha wanafunzi. Suala la taaluma kwa chuo hiki halipewi umuhimu unaostahili.

  Wakati taaluma ikichukuliwa kama siyo kipaumbele cha Chuo, kwa upande mwingine inaonekana kuwa namna ya Uongozi wa juu kujipatia fedha ndio kipaumbele cha kwanza katika chuo hiki.

  Huku ikiwa Mheshimiwa Rais amepiga marufuku safari za nje ya nchi zisizo na manufaa kwa Taifa, viongozi wa juu wa chuo kwa sasa wako nje ya nchi ikiwa ni njia mojawapo ya kujipatia fedha. Mkuu wa chuo yuko ziarani Brazil, na Makamu wake wawili nao wako ng’ambo kwa sababu hizohizo za kujipatia kipato nje ya mshahara. Mmoja yuko Jamhuri ya Czech na mwingine yuko Jamhuri ya Kenya.

  Kujipatia kipato kwa njia hii ya kubuni safari za kikazi ni mbali na ufisadi mbalimbali unaofanywa kwa kupitia kandarasi za ujenzi, na miradi ya ujenzi inayofanyika chuoni, chakula cha wanafunzi, mishahara ya wafanyakazi, fedha ya mafunzo viwandani, malipo hewa n.k. hali ambayo imeonekana kukisababishia hasara Chuo na Taifa.

  Kuna kila sababu kwa Serikali kufuatilia mambo yote yanayofanyika chuoni kwa jicho la karibu kwa kuwa ni kama vile Uongozi wa chuo umejisahau kufanya kazi inayowahusu kufanya na kujikuta ukifikiria zaidi jinsi ya kujipatia fedha kwa njia zisizo halali.

  Imekuwa vigumu kuweza kupata ufanisi unaohitajika na chuo kupata ufanisi unaotakiwa kwa kuwa pia kuna aina mbalimbali za uonevu kwa baadhi ya wafanyakazi kutoka kwa uongozi wa juu katika chuo. Hali hii isipo angaliwa inaweza kusababisha migogoro isiyoisha na hivyo kudumaza chuo.

  Kila mara kumekuwa na vikao vya kuongelea madhaifu haya baina ya wafanyakazi na Menejimenti na hata kufikia kuona mapungufu hayo yakielemea upande mmoja wa uongozi lakini inaonekana kama Menejimenti haina nia ya dhati ya kuacha kinacholalamikiwa na wafanyakazi.
  Last edited by KAYUMBA; 23-09-2016 at 08:46.

 2. #2
  Member
  Join Date
  Jan 2015
  Posts
  44
  Rep Power
  0
  Likes Received
  0
  Likes Given
  1

  Re: Kuna haja ya kufuatilia kwa karibu taaluma inayotolewa katika chuo hiki


 3. #3
  Junior Member
  Join Date
  Mar 2016
  Posts
  28
  Rep Power
  0
  Likes Received
  1
  Likes Given
  0

  Re: Kuna haja ya kufuatilia kwa karibu taaluma inayotolewa katika chuo hiki

  Mke wa Rais wa awamu ya Nne Mama Salma Kikwete anao usemi wake mzuri sana kwamba "MTOTO WA MWENZIO NI MTOTO WAKO". Amekuwa akitumia sana usemi huo pale ambapo wazazi wengine walipowafanyia watoto wa wazazi wenzao mambo mabaya yasiyofaa. Baadhi ya wazazi wamekuwa wakifanyia watoto wa wenzao mambo mabaya bila kujali kwamba mtoto wa mwenzako ni sawa na mtoto wako.

  Ni jambo la kutia huzuni sana ikiwa wazazi watatuma watoto wao kwa wazazi wenzao walio Chuo cha Ufundi Arusha kwa nia ya kupatiwa elimu na malezi bora lakini wazazi wenzao ambao ni viongozi wa chuo, wakawafanyia tofauti na malengo ya wazazi wao halisi. Fikiria mzazi masikini wa Kitanzania ambaye wakati mwingine mlo wa siku unampa shida, anauza mifugo yake au kipande cha ardhi yake, au mazao yake ya shamba ili kupata ada ya mtoto wake alafu mtoto huyo asipate elimu iliyotarajiwa anapokuwa chuoni?

  Fikiria ikiwa ada iliyolipwa na mzazi huyu baada ya kuuza sehemu ya mali zake chache anajinyima kula lakini ikachukuliwa na mjanja fulani tena kwa ajili ya kupita na dadapoa ni dhambi mbaya kiasi gani? Zipo taarifa kwamba kiongozi wa juu wa chuo hicho hana mke wala familia, kwamba aliamua tu kutelekeza familia yake mwenyewe akaona njia nyepesi kwake ni kupita na dadapoa.

  Pengine siyo kosa la bosi huyo kutoweza kujali na kutoa malezi bora kwa watoto wa wenzake kwa kuwa yeye alishindwa kufanya hivyo kwa watoto na familia yake mwenyewe. Kama mtu ameshindwa mambo yake mwenyewe haitashangaza akishindwa ya wenzake. Hali hiyo inachukuliwa na wengi kama pengine ndio sababu ya kutoweza kujali watoto wa wenzake kwa kuwa ameshindwa kujali hata watoto wake mwenyewe.

  Moyo wa Upendo na wa kujali huanzia ngazi ya familia. Ikiwa mtu hana watoto wala familia ni vigumu kujua familia inahitaji malezi ya namna gani. Ikiwa mtu mzima ataamua kutelekeza watoto na familia yake na kuamua kupitapita na dadapoa na kuchukulia jambo hilo kama sehemu ya maisha, ni tatizo kubwa. Tena inakuwa ni tatizo kubwa zaidi pale ambapo mtu huyo anapotumia vibaya rasilimali za umma ili tu kujipatia fedha chafu kwa ajili ya kuonekana wa maana mbele ya dadapoa.

  Hapa kuna tatizo kubwa kuliko inavyoweza kufikiriwa na mtu wa kawaida.

 4. #4
  Member
  Join Date
  Jan 2015
  Posts
  44
  Rep Power
  0
  Likes Received
  0
  Likes Given
  1

  Re: Kuna haja ya kufuatilia kwa karibu taaluma inayotolewa katika chuo hiki

  TAARIFA KWA UMMA
  UWEPO WA TAARIFA ZA UPOTOSHAJI
  KUHUSU CHUO CHA UFUNDI ARUSHA


  Uongozi wa Chuo cha Ufundi Arusha (ATC) unautaarifu umma wa Watanzania na Wadau mbalimbali wa Chuo kuwa, hivi karibuni kumekuwepo na taarifa za tuhuma mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii dhidi ya Menejimenti ya Chuo, Mkuu wa Chuo, Baadhi ya Watumishi na Mamlaka za Serikali.
  Aidha, Uongozi wa Chuo unapenda kukanusha na kueleza Umma kuwa, taarifa hizo hazina chembe zozote za ukweli na zinazushwa na baadhi ya Watu wachache kwa lengo la kupotosha Umma na kwa nia ya kudhoofisha ustawi mzuri wa Chuo.
  Vile vile tuhuma hizo zimeeleza kuwepo uonevu kwa baadhi ya Watumishi wa Chuo. Tunapenda Umma ufahamu kuwa, Chuo hakijawahi kumwonea Mtumishi yeyote na maswala yote yanayohusu watumishi hushughulikiwa kwa mujibu wa sheria na kanuni za Utumishi wa Umma na nchi ikiwa ni pamoja na wafanyakazi watatu (03) waliofukuzwa kazi kwa kukiuka sheria hizo na shauri lao liko kwenye Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA).
  Mwisho tunapenda kuufahamisha Umma kuwa, wakati wowote Chuo kipo tayari kutoa taarifa sahihi kwa Mamlaka zilizoko kisheria.
  Imetolewa na:
  Ofisi ya Uhusiano Chuo cha Ufundi Arusha (ATC)
  S.L.P 296, Arusha.
  Barua pepe: pro@atc.ac.tz, tovuti: www.atc.ac.t

 5. #5
  Junior Member
  Join Date
  Mar 2016
  Posts
  26
  Rep Power
  0
  Likes Received
  0
  Likes Given
  0

  Re: Kuna haja ya kufuatilia kwa karibu taaluma inayotolewa katika chuo hiki

  Mpango wa Serikali kuanzisha Chuo cha ufundi Arusha ulijadiliwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lililoketi katika vikao vyake Mwezi Februari/Machi 2007. Hatimaye Bunge lilipitisha mpango huo, na hatimaye lilitoka Agizo la kuanzisha Chuo cha Ufundi Arusha na kutangazwa kwenye Tangazo la Serikali Namba 78 la 30 Machi 2007.

  Ni kupitia mamlaka hiyo iliyowekwa kisheria, Bodi ya Uongozi wa chuo ilianzishwa. Kadhalika ni kupitia mamlaka hiyo nafasi ya Mkuu wa chuo ilianzishwa. Mpaka sasa Bunge halijawahi kufuta au kubadilisha sehemu yoyote ya Agizo la kuanzisha Chuo cha Ufundi Arusha [The National Council for Technical Education (Arusha Technical College) Establishment Order, 2007].

  Kulitokea mpango usio wa Serkali ulioaminika kuwa na nia ovu ulipangwa kwa ushirikiano wa Mkuu wa Chuo Mr./Dkt. Richard Masika Mushi, aliyekuwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Elimu ya Ufundi (NACTE) Mr./Dkt Primus Nkwera na Kaimu Mkurugenzi wa Elimu ya Ufundi katika Wizara ya Elimu Mr. Thomas Katebalirwe. Katika mkakati huo wa Mkuu wa chuo wenye kila dalili za kuwa na nia ovu, NACTE ilitoa Tangazo kwenye gazeti la Serikali mwezi Julai 2015 kuwa sheria/Agizo iliyoanzisha Chuo cha Ufundi Arusha yaani GN 78/2007 imefutwa yote.

  Mwezi Septemba 2015, Mkuu wa Chuo Mr./Dkt Richard Masika Mushi kama Katibu wa Bodi ya Chuo aliwasilisha mbele ya kikao cha Bodi Taarifa kuwa Chuo kimepata sheria mpya baada ya sheria iliyokuwepo kufutwa yote. Haikuweza kufahamika mara moja kama sheria iliyotakiwa kufutwa ilikuwa na mapungufu gani.

  Nia ovu iliyokuwa imejificha katika mpango wa Mkuu wa chuo ni kutaka kuficha udhaifu kwa kushindwa kutekeleza sheria iliyoanzisha chuo inavyotakiwa. Mkuu wa Chuo na Bodi ya chuo walishindwa kutekeleza sehemu kubwa na za muhimu hivyo kulazimu mbinu ya kutaka sheria yote kufutwa bila sababu. Kwa ufupi baadhi ya yaliyoshindikana kutekelezwa ni kama ifuatavyo:
  a)Sheria inataka Bodi kwa kupata ushauri kutoka kwa Waziri wa Elimu kutengeneza kanuni kwa ajili ya uendeshaji mzuri wa chuo. Sheria husika ilihitaji kuwa kanuni zozote zitakazotengenezwa kutokana na sheria hiyo zitangazwe kwenye gazeti la Serikali. Hili halikuweza kufanyika.
  b)Sheria inataka Bodi ya chuo kuunda kamati mbalimbali kama Bodi itakavyoona inafaa, kamati hizo zikishaundwa pamoja na kazi zake ziwekwe kwenye kanuni za chuo ambazo ni lazima zitangazwe kwenye gazeti la serikali. Hili halikufanyika.
  c)Sheria inataka fedha zozote zinazolipwa chuoni kuwa mali ya chuo na kutumika katika utaratibu unaotambulika wa matumizi ya fedha za Serikali. Haifanyiki hivyo.
  d)Sheria inataka Katibu wa Bodi ya chuo kuwapa wajumbe wa Bodi taarifa na makabrasha ya kikao cha Bodi wiki mbili (2) kabla ya tarehe ya kikao cha Bodi. Haifanyiki hivyo.
  e)Sheria ninataka mmoja wa wajumbe wa Bodi ateuliwe kutoka Bodi yoyote inayofaa ya kitaalamu katika Nyanja za Sayansi na Teknolojia. Hili halifanyiki hivyo na mbaya zaidi ujumbe wa Bodi umekuwa ukitolewa kama zawadi kutoka kwa Mkuu wa chuo kwa wajumbe kujipatia fedha.

  Ikiwa mambo ya msingi kabisa yaliyotakiwa kisheria hayafanyiki, na ikiwa taratibu za kutengeneza mitaala zinafahamika vizuri lakini nazo hazifuatwi, na ikiwa inafahamika vizuri kuwa wanafunzi wa chuo wanahitaji kufundishwa sawasawa na haifanyiki hivyo na ikiwa stahili mbalimbali za wafanyakazi zinafahamika lakini hazilipwi na ikiwa hata pale ambapo kuna changamoto ya fedha safari zisizo za lazima kwa Mkuu wa chuo haziepukiki, hakuna muonekano kwamba kuna nia njema ya kuleta manufaa kwa chuo na Taifa kutoka kwa Uongozi huu wa chuo.

  Ni vigumu sana kufikia malengo ya Mheshimiwa Rais ikiwa aina hii ya uongozi unaohitaji kufuatiliwa kwa karibu na mamlaka za juu zitaendelea kuwepo.

 6. #6
  TUA
  TUA is offline
  Senior Member
  Join Date
  Oct 2014
  Posts
  677
  Rep Power
  6
  Likes Received
  32
  Likes Given
  0

  Re: Kuna haja ya kufuatilia kwa karibu taaluma inayotolewa katika chuo hiki

  Ninavyoona, serikali imepata hasara kubwa kupitia huyu Mr/Dr Richard Masika Mushi. Kitendo tu cha kutokea upotevu wa Tsh 1.5 bilioni katika jengo lililojengwa lijulikanalo kama jengo la irrigation, na ambalo mpaka sasa halijaisha ni maumivu makubwa kwa Serikali. Pia kitendo cha kampuni ya Chuo ya ushauri ijulikanayo kama ATC-PCB kuonekana ina upotevu wa mamilioni ya fedha ni maumivu makubwa kwa serikali. Kitendo cha huyu bwana kujipa mshahara wa profesa ilhali yeye ni lecturer ni maumivu tosha kwa Serikali.

  Kitendo cha Mkuu wa Chuo Mr/Dr Richard Masika Mushi na msaidizi wake Dr Masudi Senzia kuchukua matofali yapatayo 20,000 yaliyobaki katika jengo hilo hapo juu na kwenda kujengea nyumba zao binafsi bila hata kukumbuka kuwa watoto wa maskini hawana madarasa sehemu zingine ni maumivu tosha kwa Serikali. Matofali haya yangeweza kujenga Sekondari yeyote ile na watoto wa maskini wakasoma.

  Kitendo cha Mkuu huyu wa Chuo kupendekeza majina zaidi ya nusu ya wajumbe wa Bodi ambao ni kabila lake na ndugu zake kwa waziri wa wakati huo (Dr Shukuru Kawambwa) na ikakubalika ni fedheha kwani ndio maana Bodi hii haifanyi chochote, licha ya matatizo makubwa yaliyokikumba Chuo. Najiuliza hivi bodi hii imeshindwa hata kujua kuwa Chuo hakina Curriculums? Au waalimu walikuwa wanatumia curriculums ambazo hazijakuwa approved na NACTE? Mbona kwenye Bodi kuna kamati inayoshughulikia ACADEMICS? Wajumbe hawa wa bodi walipewa ulaji na Mr/Dr Richard Masika Mushi hivyo hawako kwa manufaa ya Taifa ndilo jibu. Na hawawezi kumwambia kitu kwa kuwa anawakirimu kwa hela.

  Hebu angalia, hawa wajumbe wa Bodi.
  1 Abraham Nyanda- Mwenyekiti (Marehemu kwa sasa)
  2 Prof Christian W. Nyahumwa
  3 Suzane Mnafe Mosha ---Mchagga
  4 Mr Thomas Katebalirwe
  5 Eng Benedict Lema--- Mchagga
  6 Ms Lyne T.H. Ukio--- Mchagga
  7 Ms Hycinta B. Makileo---Mchagga
  8 Pius Paul---Mwanafunzi
  9 Hon Rashid Mfutakamba (MP)
  10 Prof Karoli Njau--- Mchagga
  11 Augustile S Mbitila
  12 Mr/Dr Richard Masika Mushi--- MKUU WA CHUO--- Mchagga

  Unategemea Bodi hiyo ifanye kazi kwa ufanisi? Tujiulize maswali machache. Waziri wa Wakati huo hakuwa wa Kabila hilo. Katika hali ya kawaida tufikirije? Kwa sasa hata wanafunzi wenyewe malalamiko yao wanapeleka wizarani ilhali kuna bodi, ambayo ndani yake kuna mwakilishi wa wanafunzi. Hii inaashiria nini? Kuonyesha tu jinsi ambavyo, mambo ni ya ajabu, mjumbe mmoja hapo juu, jina namba tatu (3) amekuwepo kwenye bodi toka bodi ya kwanza mwaka 2009. Hakuna watanzania wengine? Sijui lakini napata maswali mengi hapa, je katika bodi za Taasisi zingine ndivyo ilivyo?
  Inakuwaje wajumbe 6 kati ya 12 wawe jamaa wa kabila moja? kuna kitu

 7. #7
  Senior Member
  Join Date
  Sep 2014
  Posts
  468
  Rep Power
  6
  Likes Received
  28
  Likes Given
  17

  Re: Kuna haja ya kufuatilia kwa karibu taaluma inayotolewa katika chuo hiki

  Usaili huwa una maana kubwa sana. Kwamba Yule/wale wanaoonekana kuwa na uwezo zaidi ya wenzao ndio hupewa kazi. Kanuni hiyo haikufuatwa katika kumpata Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha nap engine ndiyo maana kila kitu kinakwenda kwa jinsi ya alimradi liende. Katika orodha ya waombaji wanne walioomba na kufanya usaili wa nafasi ya Mkuu wa chuo namba 3 na 4 zilichukuliwa na Masika Mushin na Masudi Senzia. Kwa maana hiyo, nafasi mbili za mwisho zilichukuliwa na ambao leo ndio viongozi wa juu kabisa wa chuo.

  Matokeo ya kukiuka kanuni za kutafuta watu bora ili wapewe kazi yamejionesha wazi kivitendo na siyo kinadharia. Chuo cha Ufundi Arusha kinayo mamlaka ya kutengeneza mitaala, kutahini na kutoa vyeti kwa wahitimu wake kuanzia ngazi ya cheti hadi shahada ya kwanza kiliyopewa na NACTE. Hiki ni kitu cha kawaida kwa vyuo vilivyopimwa Mamlaka zinazohusika na kuonekana vina UWEZO wa kufanya hivyo. Kuna changamoto kwamba mitaala inayotumika katika chuo hiki ni ya siku nyingi na haijawahi kufanyika juhudi za makusudi ili kuweza kuihuisha mitaala husika. Kuna changamoto kwamba, kuna baadhi ya mitaala inayodaiwa kuhuishwa lakini haikuzingatia njia sahihi ya kuhuisha mitaala kwa kushirikisha wataalamu wa mitaala na wadau muhimu wanaohusika. Kuna changamoto kwamba, leo mwanafunzi au mwalimu asipoingia darasani hakuna anayeweza kujua kwa kuwa hakuna ufuatiliaji. Kuna changamoto kuwa vifaa vya kufundishia na kujifunzia vinaweza kutonunuliwa kabisa au vikanunuliwa vichache na maisha ya kitaaluma yakasonga mbele. Kuna changamoto ya zoezi zima la kuanzia pale MTIHANI unapotungwa mpaka unapofanyika na mpaka matokeo yanapotoka. Kuna changamoto ya mafunzo viwandani kwa wanafunzi wa shahada ya kwanza, wanahitajika kwenda mafunzo kwa wiki kumi (10), lakini wanalipwa kwa wiki nane (8). Kuna changamoto kwamba wanafunzi wa kike wa ngazi ya cheti na stashahada wamekuwa wakipata uja uzito na wengine wamepoteza hata maisha kwa matatizo ya ujauzito katika umri mdogo.

  Katika kukabiliana na changamoto kama zilivyo hapo juu, njia moja tu imekuwa kama ndio suluhisho la changamoto hizo iliyofikiriwa na Uongozi kwamba inafaa. Waswahili wanasema penye udhia, penyeza rupia. Ili kufunika mambo yote yanayoonekana kama ni changamoto japo ni kama za kutengeneza wanafunzi WANAONGEZEWA MAKSI ILI WAFAULU. Kwa kawaida, mwanafunzi akishafaulu vizuri bila kujali kama anazo stadi na maarifa sahihi halalamiki. Wakifeli au wasipofaulu vizuri, ili kuondoa malalamiko, Uongozi unaongeza maksi.

  Suala la TAALUMA ni suala linalotakiwa kuangaliwa kama mboni ya jicho. ELIMU ni kila kitu. SAYANSI NA TEKNOLOJIA ni ELIMU inayopaswa kupewa uzito unaostahili kama TAIFA linahitaji kusonga mbele kimaendeleo na kiuchumi. Maksi za DEZO ili kuondoa udhia wa wanafunzi kulalamikia changamoto za utoaji ELIMU katika chuo hiki hazitalifikisha TAIFA kuwa la wiwanda kama ilivyo azma ya Mhe Rais. Viwanda hivyo navyo vinatakiwa kuwa endelevu kwa kuwa na wataalamu mbalimbali wa kuviangalia.

  Pengine wangepatikana waliokuwa na nafasi ya 1 na 2 kuwa viongozi wa juu kiuongozi chuoni changamoto hizi na mbinu zake za utatuzi ungekuwa tofauti. Kila siku ni ya kujifunza, hapa napo kuna la kujifunza.

 8. #8
  TUA
  TUA is offline
  Senior Member
  Join Date
  Oct 2014
  Posts
  677
  Rep Power
  6
  Likes Received
  32
  Likes Given
  0

  Re: Kuna haja ya kufuatilia kwa karibu taaluma inayotolewa katika chuo hiki

  Mbunga, mimi binafsi nashangazwa na jinsi ambavyo hapa Chuoni, watu wanajali zaidi kuhudhuria vikao vya Mkuu wa Chuo kuliko kuingia Darasani. Hii ni baada ya Mkuu wa Chuo Mr/Dr Richard Masika Mushi kujitengenezea Sheria zake zijulikanazo kama ATC STAFF REGULATIONS, 2013, na kuweka kipengele kinachosema kuwa Mkuu wa Chuo akiitisha kikao usipokwenda ni INSURBODINATION, kwamba adhabu yake ni kufukuzwa kazi. Tumeshuhudia watu wengi ambao kwa njia moja au nyingine wamepewa barua za warning kwa kutohudhuria vikao hivyo. Cha ajabu hiyo staff regulation, ambayo hata siyo document inayotambulika kisheria, haikusema mwalimu asipoingia darasani atapewa adhabu gani. Hii ndio maana taaluma imedorora sana hapa Chuoni kwani hakuna anayefuatilia hata kama wanafunzi hawakufundishwa semester nzima. Mfano mzuri ni pale ambapo mkuu wa Chuo Mr/Dr Richard Masika Mushi alipoamua kuchukua idara nzima ya Ujenzi na kwenda nayo morogoro akidai wanahudhuria semina kwa muda wa wiki tatu. Sasa tunajiuliza wanafunzi hao watatainiwaje, ikiwa hizo wiki tatu zilipotea. Kuna haja ya Wizara kutupia mambo haya macho.

 9. #9
  Member
  Join Date
  Jan 2015
  Posts
  44
  Rep Power
  0
  Likes Received
  0
  Likes Given
  1

  Re: Kuna haja ya kufuatilia kwa karibu taaluma inayotolewa katika chuo hiki

  TAARIFA KWA UMMA
  UWEPO WA TAARIFA ZA UPOTOSHAJI
  KUHUSU CHUO CHA UFUNDI ARUSHA


  Uongozi wa Chuo cha Ufundi Arusha (ATC) unautaarifu umma wa Watanzania na Wadau mbalimbali wa Chuo kuwa, hivi karibuni kumekuwepo na taarifa za tuhuma mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii dhidi ya Menejimenti ya Chuo, Mkuu wa Chuo, Baadhi ya Watumishi na Mamlaka za Serikali.
  Aidha, Uongozi wa Chuo unapenda kukanusha na kueleza Umma kuwa, taarifa hizo hazina chembe zozote za ukweli na zinazushwa na baadhi ya Watu wachache kwa lengo la kupotosha Umma na kwa nia ya kudhoofisha ustawi mzuri wa Chuo.
  Vile vile tuhuma hizo zimeeleza kuwepo uonevu kwa baadhi ya Watumishi wa Chuo. Tunapenda Umma ufahamu kuwa, Chuo hakijawahi kumwonea Mtumishi yeyote na maswala yote yanayohusu watumishi hushughulikiwa kwa mujibu wa sheria na kanuni za Utumishi wa Umma na nchi ikiwa ni pamoja na wafanyakazi watatu (03) waliofukuzwa kazi kwa kukiuka sheria hizo na shauri lao liko kwenye Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA).
  Mwisho tunapenda kuufahamisha Umma kuwa, wakati wowote Chuo kipo tayari kutoa taarifa sahihi kwa Mamlaka zilizoko kisheria.
  Imetolewa na:
  Ofisi ya Uhusiano Chuo cha Ufundi Arusha (ATC)
  S.L.P 296, Arusha.
  Barua pepe: pro@atc.ac.tz, tovuti: www.atc.ac.t 10. #10
  Member
  Join Date
  Feb 2015
  Posts
  56
  Rep Power
  6
  Likes Received
  0
  Likes Given
  0

  Re: Kuna haja ya kufuatilia kwa karibu taaluma inayotolewa katika chuo hiki

  WADAU AMANI IWE NANYI. BAADA YA MUDA MREFU SANA NIMEKUWA NAJIULIZA KUHUSU MAJIBU AU MAELEZO YANAYOJITOKEZA KATIKA BANGO, ANDIKO NA PIA KLIPU HIYO HAPO JUU AMBAYO KIMSINGI INAONEKANA KUWEKWA NA MENEJIMENTI YA CHUO. KINACHONISHANGAZA NI PALE AMBAPO BANGO, ANDIKO AU KLIP HIYO HAIJIBU HOJA BALI IMEISHIA KUTOA TUHUMA JUU YA WATU WALIOFUKUZWA KAZI. MARA NYINGI MENEJIMENTI YA CHUO IMETUHUMIWA KWA MAMBO MAZITO KIASI KWAMBA KAMA TUHUMA HIZO NI ZA KWELI ILITAKIWA MAMLAKA ZINAZOHUSIKA ZIMEKWISHA CHUKUA HATUA. PIA KINACHOSHANGAZA WENGI NI PALE AMBAPO TANGAZO HILI, BANGO AU KLIPU HII NI YA TOKA MWAKA 2013. NINACHOJIULIZA NI KWAMBA WATU WALIOFUKUZWA KAZI SIKU NYINGI HIZO WANAWEZAJE KUFAHAMU MAMBO/TUHUMA NZITO HIVYO WAKATI HAWAPO HAPO? NAPENDA KUNUKUU BAADDHI YA MAELEZO YANAYONISHANGAZA KATIKA BANGO AU KLIPU HII

  “Vile vile tuhuma hizo zimeeleza kuwepo uonevu kwa baadhi ya Watumishi wa Chuo. Tunapenda Umma ufahamu kuwa, Chuo hakijawahi kumwonea Mtumishi yeyote na maswala yote yanayohusu watumishi hushughulikiwa kwa mujibu wa sheria na kanuni za Utumishi wa Umma na nchi ikiwa ni pamoja na wafanyakazi watatu (03) waliofukuzwa kazi kwa kukiuka sheria hizo na shauri lao liko kwenye Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA)”.

  Swali langu ni kwamba, kama tangazo hili lillianza kuwekwa humu tangu mwaka 2013, likidai kuna wafanyakazi waliofukuzwa na kesi zao ziko CMA, ingekuwa vizuri basi, CMA au hiko CHUO wakaueleza umma hizo kesi za toka 2013 mbona haziishi? Lakini la pili ni kwamba, mbona katika tuhuma zinazotolewa dhidi ya menejimenti ya Chuo hiki hazijawahi kuzungumzia uonevu wa baadhi ya watumishi waliofukuzwa kazi? Sidhani kama tuhuma zinazotolewa dhidi ya menejimenti ya Chuo zinazungumzia wafanyakazi waliofukuzwa kazi, zimejikita zaidi kwenye ufisadi, matumizi mabaya ya fedha za umma, na matumizi mabaya ya madaraka yanayofanywa na menejimenti ya Chuo. Kwa mfano, hoja iliyoletwa na Kayumba inazungumzia jinsi Taaluma ilivyoshuka, Chuo kukosa mitaala (curriculums), wanafunzi kuongezewa maksi na menejimenti ya Chuo nk. Mbona hakuna malalamiko juu ya watu waliofukuzwa kazi? Na kama wafanyakazi hao walifukuzwa muda mrefu yapata miaka mitatu au miwili hizi habari za wanafunzi kuongezewa maksi na menejimenti, au Chuo kukosa mitaala wanajuaje? Naona majibu yanayotolewa hayajibu hoja.

 11. #11
  Junior Member
  Join Date
  Mar 2016
  Posts
  28
  Rep Power
  0
  Likes Received
  1
  Likes Given
  0

  Re: Kuna haja ya kufuatilia kwa karibu taaluma inayotolewa katika chuo hiki

  Kuna jambo linalotakiwa kuingizwa kwenye kitabu cha kumbukumbu ya matukio ya ajabu ya Dunia.

  Kitendo cha Uongozi wa juu kuongezea baadhi ya wanafunzi maksi nje ya utaratibu unaofahamika umepokelewa na wengi kama uhusiano usiofaa na wa kupitiliza. Inapofikia mahali Mkuu wa chuo au Msaidizi wa Mkuu wa chuo akaitwa shemeji na wanafunzi ni jambo la ajabu kabisa. Lakini, jambo la ajabu zaidi na la kusikitisha, ni pale ambapo Mkuu wa chuo au Msaidizi wake akiwa kama shemeji wa wanafunzi anapoweza kushawishiwa na mwanafunzi akaongeza maksi kwa mwanafunzi/wanafunzi nje ya utaratibu unaoeleweka.

  Ikiwa mwanafunzi wa ngazi ya shahada ya uhandisi au stashahada ya uhandisi kama zilivyo Chuo cha Ufundi Arusha ataongezewa maksi na uongozi wa juu wa chuo kwa utaratibu wa kuwa shemeji, ni tukio la ajabu kabisa. Swali ni je, tunakwenda wapi? Tunatengeneza kizazi cha wasomi wa aina gani? Uhusiano wa Mkuu wa chuo na mwanafunzi kwa kiwango cha kuongeza maksi nje ya utaratibu unaofahamika na kukubalikaa ni wa nini?

  Uhusiano wa Mkuu wa chuo au Msaidizi wake na mwanafuzi/wanafunzi kwa kiwango cha kufikia hatua ya kuitwa shemeji na kukubali jina hilo kwa kuongezea baadhi ya wanafunzi maksi bila utaratibu unaoeleweka ni jambo ambalo halijawahi kutokea mahali pengine popote, isipokuwa hivi sasa limeanza kutokea Chuo cha Ufundi Arusha. Kama ni jambo zuri lienziwe, lakini kama ni baya, lipigwe vita na wote wenye akili timamu.

 12. #12
  Member
  Join Date
  Dec 2014
  Posts
  78
  Rep Power
  6
  Likes Received
  3
  Likes Given
  1

  Re: Kuna haja ya kufuatilia kwa karibu taaluma inayotolewa katika chuo hiki

  Tehetehetehe.

  Wapo waliosema "Elimu ni ufunguo wa maisha" wengine wakasema "Elimu ni msingi wa maendeleo" Wengine wakasema Elimu ni Bahari, haina mwisho.

  Wengine wakasema "Elimu ni taa au nuru", Wengine wakasema "Elimu huongeza Maarifa" n.k n.k

  Yeyote atakayekuwa amejibu hivyo na majibu mengine zaidi ambayo hayajawekwa hapa kutokana na swali linaloweza kuulizwa kwamba Elimu ni nini, atakuwa amepata. Jinsi Elimu inavyoonekana kuwa na majibu mengi ndivyo inavyoonesha kwamba Elimu ni kitu muhimu na siyo kitu cha kufanyia mchezo.

 13. #13
  TUA
  TUA is offline
  Senior Member
  Join Date
  Oct 2014
  Posts
  677
  Rep Power
  6
  Likes Received
  32
  Likes Given
  0

  Re: Kuna haja ya kufuatilia kwa karibu taaluma inayotolewa katika chuo hiki

  Hivi hasa nini ilikuwa nia ya Mkuu wa Chuo hiki na uongozi wake kuwaongezea maksi wanafunzi ambao hawakufaulu? Mbona vitu kama hivi havitokei katika Taasisi nyingine? Au ni katika kutafuta sifa za ziada? Najaribu kufikiri kwa kina jambo hili sipati jibu

 14. #14
  Member
  Join Date
  Feb 2015
  Posts
  50
  Rep Power
  6
  Likes Received
  0
  Likes Given
  0

  Re: Kuna haja ya kufuatilia kwa karibu taaluma inayotolewa katika chuo hiki

  Pengine sababu za Mkuu Chuo na menejimenti yake kuongeza maksi za wanafunzi waliofeli ni ili kufunga kabisa midomo ya wafanyakazi, wanafunzi na wanajamii wanaopinga ufisadi unaofanywa na uongozi wa Chuo.Pia kuwafanya Watanzania waamini kuwa kila kitu ni shwari ili Serikali isishtuke kwa yanayotokea hapa Chuoni. Na kutimiza ule msemo kuwa UKILA NA KIPOFU USIMGUZE MKONO.
  Haya ndiyo mambo machafu wafanyakazi tunayopinga;

  1) Matumizi ya fedha za mafunzo viwandani (IPT) kiasi cha TZS 320,000,000/= zina utata.
  Utata wa fedha za mafunzo viwandani ni kuanzia 2011/12 – 2014/2015. Kwa miaka minne mfululizo kiasi cha 80,000,000/= kila mwaka hazijulikani zilikwenda wapi au zilifanya nini.

  2) Matumizi ya fedha za mishahara ya wafanyakazi mwezi Januari 2014 kwa wafanyakazi walioajiriwa Desemba 2013. Wastani wa TZS 30,000,000/= za mishahara hazijulikani zilikwenda wapi au zilifanya nini

  3) Miradi hewa ya ujenzi ililipwa wastani wa TZS 400,000,000/=

  4)Matumizi ya malipo hewa ya miradi ya ujenzi kupitia ATC-PCB, wastani wa TZS 250,000,000/=

  5) Matumizi ya upanuzi wa jengo la Utawala, wastani wa TZS 700,000,000/=

  6) Matumizi ya ujenzi wa jengo la Umwagiliaji lililogharimu TZS 4,000,000,000/=. Wastani wa TZS 2,500,000,000/= zinakadiriwa kutosha kujenga jengo hili na hasa ikizingatiwa kwamba matofali na shughuli nyingine kama paa na madirisha zilifanywa kwa rasilimali za Chuo. Wastani wa TZS 1,500,000,000/= zinadaiwa kutumika kifisadi. Kadhalika zaidi ya matofali 20,000 yalichukuliwa na Uongozi kwa matumizi binafsi.

  7) Matumizi ya fedha za msaada shamba la Oljoro wastani wa TZS 400,000,000/=

  8) Matumizi ya fedha zinazokatwa kutoka mishahara ya wafanyakazi kwa ajili ya ukarabati wa nyumba wastani wa TZS 300,000,000/=

  Kwa wastani, zaidi ya TZS 3.5 Billioni hazijulikani ziko wapi au zilifanyia nini

Posting Permissions

 • You may not post new threads
 • You may not post replies
 • You may not post attachments
 • You may not edit your posts
 •