Mlinganisho wa meli zilizotia nanga, na zinazotarajia kutia nanga bandari za Durban, Mombasa na Dar es Salaam leo.

Mpaka dakika hii ninavyoandika kwa mwezi mmoja yaani toka 05/8/2016 hadi leo 05/9/2016 Meli zilizoingia katika bandari ya Durban Afrika Kusini ni 65 na Meli zinazotarajiwa kuingia bandarini hapo ni 98.

Mpaka dakika hii ninavyoandika leo kwa mwezi mzima yaani toka 05/8/2016 hadi leo tarehe 05/9/2016 Meli zilizoingia Bandari ya Mombasa ni 29 na zinazotarajiwa kuingia hapo ni 26.

Mpaka hivi ninavyoandika dakika hii kwa mwezi mmoja yaani toka 05/8/2016 hadi leo 05/9/2016 Meli zilizotia nanga bandari ya Dar es Salaam ni 13 tu hii ni pamoja na zile zilizosimama kule karibu na Masaki zikisubiri kuingia gatini, zinazotarajiwa kutua ni 8 yani zile zitokazo huko ughaibuni.

Kwamjibu wa Takwimu za TRA, Bandari huchangia 58% ya mapato ya TRA kwa ujumla, na husababisha sekta nyingine kustawi kiuchumi kwa 80%.

Baada ya kuona mlinganisho huu, endeleeni kuimba hapa kazi tu mpaka nchi ishindwe kujiendesha ndipo mtaamka nakutafuta suluhisho...