Close

Results 1 to 3 of 3
 1. #1
  TUA
  TUA is offline
  Senior Member
  Join Date
  Oct 2014
  Posts
  677
  Rep Power
  6
  Likes Received
  32
  Likes Given
  0

  KUIBIA JAMII NI SAWA NA KUMWIBIA MUNGU: WANAFUNZI HEWA CHUO CHA UFUNDI ARUSHA

  Amani iwe nanyi Watanzania. Kwanza kabisa nampongeza rais JPM kwa jitihada zake za kupambana na rushwa, ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka. Hakika jambo hili limeleta tija kwani jitihada zake zinaonekana wazi na kila aliyehusika na ufisadi, rushwa na uharibifu wa mali ya Umma tumeshuhudia sheria ikichukua mkondo wake, na wale ambao waliharibu kwa njia moja au nyingine wasifikiri hizi ni nguvu za soda, watapata haki yao, ni suala la muda tu.

  Nimewiwa kutoa yangu maoni kwamba, sasa hivi kote nchini, waalimu wakuu wa Shule za Sekondari na Msingi ambao wameonekana kuongeza wanafunzi ( Wanafunzi hewa) kinyemela ili kujinufaisha na pesa ya Serikali wamechukuliwa hatua na tayari wengine wamesimamishwa kazi na kazi hii ya kuwabaini wengine ingali inaendelea. Tunaipongeza sana Serikali kwa jambo hili, ila binafsi napenda kutoa wito kwa mamlaka husika kwamba tukiwabana waalimu wakuu wa Sekondari na shule za Msingi tu, tutakuwa hatutendi haki, msumeno huu ukate kote mpaka Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu, huku ndiko suala la wanafunzi hewa lilikoanzia. Sehemu ambako hela ya Serikali imechezewa bila huruma ni huku, waliohusika wawajibishwe sawa sawa na wanavyowajibishwa wa Sekondari na Msingi. Naweza kusema kwa upande wa Vyuo vikuu na Taasisi za Elimu ya juu huu ulikuwa ni wizi wa maksudi.

  Kwa Upande wa hapa Chuo cha Ufundi Arusha, inashangaza kwa sababu idadi ya Wanafunzi wa Shahada ni wachache kiasi kwamba ni vigumu kuamini kuwa hapa pia wanafunzi hewa zaidi ya Kumi (10) inasemekana wamebainika kuwepo. Kikawaida wanafunzi wa Shahada (Bachelor) sio zaidi ya 120 ikiwa ni kuanzia mwaka wa kwanza hadi wa Tatu, hivyo ni jambo lisilo la kawaida kujitokeza wanafunzi hewa. Inaaminika na kusadikika kuwa huu ni mpango mzima wa menejimenti ya Chuo hiki na Afisa wa Mikopo wa Chuo (Jina linahifadhiwa) katika jitihada zao za kujinufaisha na hela hizi. Ni hivi majuzi Waziri wa Elimu Prof. Ndalichako aliagiza Vyuo vyote vilivyohusika na suala hili kurejesha fedha zilizokwapuliwa kwa mtindo huu, na kuagiza wote waliohusika wachukuliwe hatua. Tunasubiri kusikia, kwa upande wa Vyuo vikuu na Taasisi za elimu ya Juu waliohusika wakichukuliwa hatua, kama ambavyo, tunasikia TAMISEMI, kupitia halmashauri mbalimbali na Wakuu wa Wilaya wakiwachukulia wahusika hatua. Naomba kuwasilisha.

 2. #2
  Member
  Join Date
  Jan 2015
  Posts
  44
  Rep Power
  0
  Likes Received
  0
  Likes Given
  1

  Re: KUIBIA JAMII NI SAWA NA KUMWIBIA MUNGU: WANAFUNZI HEWA CHUO CHA UFUNDI ARUSHA


 3. #3
  Senior Member
  Join Date
  Mar 2015
  Posts
  441
  Rep Power
  6
  Likes Received
  4
  Likes Given
  0

  Re: KUIBIA JAMII NI SAWA NA KUMWIBIA MUNGU: WANAFUNZI HEWA CHUO CHA UFUNDI ARUSHA

  teeeteteteteeheteteteee kazi ipo Tuamini wapi JUU chini
  shida za watanzania nina zijua

Posting Permissions

 • You may not post new threads
 • You may not post replies
 • You may not post attachments
 • You may not edit your posts
 •