Close

Results 1 to 5 of 5
 1. #1
  TUA
  TUA is offline
  Senior Member
  Join Date
  Oct 2014
  Posts
  677
  Rep Power
  6
  Likes Received
  32
  Likes Given
  0

  BODI YA CHUO CHA UFUNDI ARUSHA HAINA UWEZO WA KIUTENDAJI

  Kiuhalisia Bodi ya Chuo cha Ufundi Arusha ni Bodi ambayo haina uwezo wa Kiutendaji na iko kwa maslahi ya Mkuu wa Chuo hiki Dr Richard Masika Mushi. Hii ni baada ya mambo mengi ya kifisadi na ya matumizi mabaya ya madaraka kuripotiwa katika Chuo hiki lakini bodi hii hakuna hata kimoja imeweza kushughulikia.
  Wafanyakazi tunabaki kujiuliza maswali mengi juu ya bodi hii kutokana na kwanza, kuwa na idadi ya wajumbe ambao zaidi ya nusu ni wa kabila moja (Wachagga), na pili ni pale ambapo imeshindwa kabisa kufuatilia matatizo yaliyopo hapa Chuo cha Ufundi Arusha, ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua Mkuu wa Chuo hiki ambaye ametajwa na kuhusishwa na mambo ya kifisadi na pahali pengine amehusika moja kwa moja katika matatizo na matumizi mabaya ya madaraka, mojawapo likiwa ni kujiongezea mshahara kinyemela na kujipa mshahara wa profesa ilhali yeye siyo profesa, na kubwa zaidi ni pale inapoonekana kuna upotevu wa kiasi cha Tsh 1.5 bilioni katika mradi wa ujenzi wa jengo la umwagiliaji.
  Imetufanya tuamini kuwa itakuwa ni kweli hawa wajumbe kwa namna moja au nyingine uteuzi wao unatokana na uwepo wa Mkuu huyu wa Chuo Dr Richard Masika Mushi, kwani katika hali ya kawaida ni kitu ambacho hakiwezekani katika bodi wajumbe zaidi ya 50% kuwa wa kabila moja. Tumeshuhudia bodi nyingi zikiwachukulia hatua watendaji wake ambao wamejikuta wakifedhehesha Serikali kwa namna moja au nyingine.
  Si jambo la kawaida kwa Mkuu wa Chuo, Mkuu wa Idara na Waalimu wote wa Idara kuondoka na kujilipa mahela kwenda Morogoro kuhudhuria kile walichokiita semina kwa wiki tatu na kuwaacha wanafunzi wiki tatu nzima bila kufundishwa. Haieleweki hizi wiki tatu ambazo wanafunzi hawa hawajafundishwa watatainiwa vipi. Mara nyingi Serikali ya awamu ya Tano imekuwa ikisisitiza uwepo wa usimamiaji wa elimu bora inayokidhi viwango. Ni ukweli usiopingika kuwa wanafunzi mara nyingi wamekuwa wakilalamikia hali ya Taaluma hapa Chuo cha Ufundi Arusha inavyopuuzwa lakini, si bodi wala menejimenti ya Chuo inayojali.
  Kuna habari kuwa Wanafunzi wamefikia hatua ya kupeleka malalamiko yao Wizarani wakilalamikia hali ya Taaluma hapa Chuoni. Tunajiuliza iweje wanafunzi wapeleke malalamiko wizarani ilhali kuna Bodi? Jibu hapa ni Rahisi tu kuwa Bodi haiwezi kumwambia Dr Richard Masika Mushi kitu kwani ndiye aliyewapendekeza na kuwapa ulaji. Tunaomba mamlaka husika ziweze kutazama bodi kama hizi ambazo haziko kwa maslahi ya Taifa, kwani bodi kama hii ndiyo inayofifisha nia ya Rais wetu JPM katika ile azma yake ya kuona Tanzania ya Viwanda inafanikiwa. Hapa hakuna bodi bali ni kikundi cha marafiki na wanafamilia.

 2. #2
  Member
  Join Date
  Feb 2015
  Posts
  56
  Rep Power
  6
  Likes Received
  0
  Likes Given
  0

  Re: BODI YA CHUO CHA UFUNDI ARUSHA HAINA UWEZO WA KIUTENDAJI

  Hiki ni kikundi cha kifamilia na cha kikabila. Hieleweki nani aliwateua, maana hakijawahi kutokea kitu cha namna hii. Hakuna kinachoendelea, kwani ni muda sasa bodi hii haina hata mwenyekiti lakini huwa wanakaa vikao kama kawaida na kulipana posho. Wafanyakazi na wanafunzi tunalalamika juu ya menejimenti ya Chuo hiki lakini hakuna kinachoendelea.
  Wanafunzi wameona njia sahihi ni kupeleka malalamiko yao wizarani kama vile hakuna bodi. Wajumbe wengine wamegeuka wa kudumu katika bodi hii mfano ni huyu Suzan Mnafe Mosha ambaye amekuwapo kwenye bodi hii kwa vipindi vyote vitatu mfululizo yaani yapata miaka 9 sasa. Hivi hakuna watanzania wengine wanaoweza zaidi ya hawa? Je Kama hakuna Mwenyekiti wa bodi kuna bodi hapo?

  Prof Christian W. Nyahumwa
  Suzane Mnafe Mosha (Mchagga)
  Mr Thomas Katebalirwe
  Eng Benedict Lema (Mchagga)
  Ms Lyne T.H. Ukio (Mchagga)
  Pius Paul
  Ms Hycinta B. Makileo (Mchagga)
  Hon Rashid Mfutakamba (MP)
  Prof Karoli Njau (Mchagga)
  Augustile S Mbitila
  Dr Richard Masika Mushi (Mchagga)

 3. #3
  Member
  Join Date
  Jan 2015
  Posts
  44
  Rep Power
  0
  Likes Received
  0
  Likes Given
  1

  Re: BODI YA CHUO CHA UFUNDI ARUSHA HAINA UWEZO WA KIUTENDAJI

  Quote Originally Posted by TUA View Post
  Kiuhalisia Bodi ya Chuo cha Ufundi Arusha ni Bodi ambayo haina uwezo wa Kiutendaji na iko kwa maslahi ya Mkuu wa Chuo hiki Dr Richard Masika Mushi. Hii ni baada ya mambo mengi ya kifisadi na ya matumizi mabaya ya madaraka kuripotiwa katika Chuo hiki lakini bodi hii hakuna hata kimoja imeweza kushughulikia.
  Wafanyakazi tunabaki kujiuliza maswali mengi juu ya bodi hii kutokana na kwanza, kuwa na idadi ya wajumbe ambao zaidi ya nusu ni wa kabila moja (Wachagga), na pili ni pale ambapo imeshindwa kabisa kufuatilia matatizo yaliyopo hapa Chuo cha Ufundi Arusha, ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua Mkuu wa Chuo hiki ambaye ametajwa na kuhusishwa na mambo ya kifisadi na pahali pengine amehusika moja kwa moja katika matatizo na matumizi mabaya ya madaraka, mojawapo likiwa ni kujiongezea mshahara kinyemela na kujipa mshahara wa profesa ilhali yeye siyo profesa, na kubwa zaidi ni pale inapoonekana kuna upotevu wa kiasi cha Tsh 1.5 bilioni katika mradi wa ujenzi wa jengo la umwagiliaji.
  Imetufanya tuamini kuwa itakuwa ni kweli hawa wajumbe kwa namna moja au nyingine uteuzi wao unatokana na uwepo wa Mkuu huyu wa Chuo Dr Richard Masika Mushi, kwani katika hali ya kawaida ni kitu ambacho hakiwezekani katika bodi wajumbe zaidi ya 50% kuwa wa kabila moja. Tumeshuhudia bodi nyingi zikiwachukulia hatua watendaji wake ambao wamejikuta wakifedhehesha Serikali kwa namna moja au nyingine.
  Si jambo la kawaida kwa Mkuu wa Chuo, Mkuu wa Idara na Waalimu wote wa Idara kuondoka na kujilipa mahela kwenda Morogoro kuhudhuria kile walichokiita semina kwa wiki tatu na kuwaacha wanafunzi wiki tatu nzima bila kufundishwa. Haieleweki hizi wiki tatu ambazo wanafunzi hawa hawajafundishwa watatainiwa vipi. Mara nyingi Serikali ya awamu ya Tano imekuwa ikisisitiza uwepo wa usimamiaji wa elimu bora inayokidhi viwango. Ni ukweli usiopingika kuwa wanafunzi mara nyingi wamekuwa wakilalamikia hali ya Taaluma hapa Chuo cha Ufundi Arusha inavyopuuzwa lakini, si bodi wala menejimenti ya Chuo inayojali.
  Kuna habari kuwa Wanafunzi wamefikia hatua ya kupeleka malalamiko yao Wizarani wakilalamikia hali ya Taaluma hapa Chuoni. Tunajiuliza iweje wanafunzi wapeleke malalamiko wizarani ilhali kuna Bodi? Jibu hapa ni Rahisi tu kuwa Bodi haiwezi kumwambia Dr Richard Masika Mushi kitu kwani ndiye aliyewapendekeza na kuwapa ulaji. Tunaomba mamlaka husika ziweze kutazama bodi kama hizi ambazo haziko kwa maslahi ya Taifa, kwani bodi kama hii ndiyo inayofifisha nia ya Rais wetu JPM katika ile azma yake ya kuona Tanzania ya Viwanda inafanikiwa. Hapa hakuna bodi bali ni kikundi cha marafiki na wanafamilia.

 4. #4
  Senior Member
  Join Date
  Sep 2014
  Posts
  468
  Rep Power
  6
  Likes Received
  28
  Likes Given
  17

  Re: BODI YA CHUO CHA UFUNDI ARUSHA HAINA UWEZO WA KIUTENDAJI

  Tangazo la Utemi linashangaza sana. Nimeona tangazo lake tangu mwaka 2014. Najaribu kujiuliza, hizo kesi za wafanyakazi huko CMA huwa zinachukua miaka mingapi kuisha? Nahisi kuna kitu kimejificha mahali fulani. Tangazo hilo pengine lina nia ya kuiambia serikali kwamba kesi za CMA-Arusha zinachukua muda sana kuisha

 5. #5
  Junior Member
  Join Date
  Mar 2016
  Posts
  26
  Rep Power
  0
  Likes Received
  0
  Likes Given
  0

  Re: BODI YA CHUO CHA UFUNDI ARUSHA HAINA UWEZO WA KIUTENDAJI

  Quote Originally Posted by utemi View Post
  Nafikiri nia halisi ya Tangazo ilikuwa ni kuufahamisha umma kwamba kuna wafanyakazi waliokuwa wamevunja sheria kanuni na taratibu za utumishi wa umma.

  Sasa imeshaamuriwa watumishi hao kurudishwa kazini na kulipwa stahili zao. Nadhani kinachotakiwa kufuata kwa sasa ni kwa wote waliohusika kulitia Taifa hasara kuwajibika kulipa hasara hiyo. Nahisi inatakiwa kuzungumzwa kwa sauti ndogo sauti ya chini maana Rais Magufuli akiwasikia watakuwa hawana bahati.

Posting Permissions

 • You may not post new threads
 • You may not post replies
 • You may not post attachments
 • You may not edit your posts
 •