Rais wa Marekani Barack Obama amewahimiza wanafunzi 2,000, wengi wao weusi kuimarisha juhudi za kupambana na ubaguzi wa rangi aliosema umebakia nchini humo.
Akizungumza katika Chuo Kikuu cha Howard mjini Washington, Bw Obama alisema hali ya Wamarekani wenye asili ya Kiafrika imeimarika sana tangu yeye atoke chuo kikuu mwaka 1983.

Obama amesema licha ya yeye kuwa rais mwenye asili ya afrika bado hakujapunguza ubaguzi wa rangi