Nilikuwa ninashangaa sikufahamu rushwa ya ngono ni kitu gani. Lakini hatimaye nimefahamu hivi karibuni kwamba kumbe rushwa ya ngono ni pale ambapo mtu anatoa mwili wake ili kupata manufaa fulani (Kazi, Cheo, upendeleo wa kupelekwa masomoni nk.).
Yanayokuwepo mpaka yakatungiwa sheria kweli utafiti wa kina unakuwa umefanywa. Ni jambo ambalo ukilisikia juu-juu mtu hawezi kujua ni nini na linafanyika wapi. Kumbe ni tatizo ambalo lipo mahali kwingi tu.
Yako maeneo ambayo mtu wa jinsia ya kike hawezi kupata kazi mpaka Bosi apewe rushwa ya ngono. Yapo maeneo vyuoni ambayo mwanafunzi wa kike mwenye sura ya kuvutia hawezi kufaulu mtihani mpaka atoe rushwa ya ngono.
Mambo yanayohusishwa na rushwa ya ngono yameshamiri sana katika Chuo cha Ufundi Arusha imefahamika. Katika hali isiyoweza kufahamika na ambayo inahusishwa na rushwa ya ngono ni pale ambapo mfanyakazi mmoja wa jinsia ya kike (jina linahifadhiwa kwa sasa) alipoajiriwa kwa upendeleo maalumu. Baada tu ya kuajiriwa alipelekwa masomoni na kuchukua nafasi ya wafanyakazi aliowakuta. Zaidi ni pale ambapo mteule huyu anaposomea kitu tofauti na matakwa ya ajira yake. Inaelezwa kwamba mlengwa huyu aliweza kutimiza masharti ya wakubwa wa Chuo ndio maana yeye anapeta tu.
Kadhalika, katika Bodi ya utawala ya Chuo mambo ni vilevile. Katika Bodi hiyo yuko mjumbe mmoja wa jinsia ya kike (jina linahifadhiwa kwa sasa) ambaye amekuwa kama mjumbe wa kudumu katika Bodi ya Chuo. Katika kile kinachoitwa kutokuwa na idadi ya kutosha ya wajumbe wa jinsia ya kike, mjumbe mmoja (jina linahifadhiwa kwa sasa) ameongezwa kwa mamlaka ya Mkuu wa Chuo. Taarifa zinasema wawili hawa katika Bodi ya Chuo wamekuwepo kwa kukidhi mahitaji ya Mkuu wa Chuo.
Ikumbukwe kwamba Mkuu wa chuo kwa kile kinachoitwa kutotii Sheria na kuonesha mamlaka yake kwa wanajumuiya ya Chuo, alidiriki hata kufanya kazi ambayo ni ya mamlaka ya Mkuu wa Nchi na Serikali ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kazi hiyo ni kuteua Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo.
Mmoja wa wafanyakazi alimwambia mwandishi wa habari hii kwamba yaani, Mkuu wa Chuo ametembea koote, wanafunzi, wafanyakazi, baadhi ya wajumbe wa Bodi na sasa anataka kwenda mpaka kwa wake za wafanyakazi, atakuwa na pepo la ngono amezidi. Amesema ndio maana mke alimkimbia na akaondoka na watoto wasipate shida, maana huyu ni mhuni kabisa alisema.
Alidokeza kwamba kuna mfanyakazi wa kike (jina linahifadhiwa kwa sasa) ambaye amekataa kabisa kufanya upuuzi huo. Kilichotokea ni kwamba mfanyakazi huyo amechanganywa na hao wanaoitwa wakubwa wa chuo mpaka sasa ameamua kuacha kazi. Hata kuacha kazi kwake imekuwa ngumu, eti anatakiwa kuwalipa wakubwa wa chuo kwa usumbufu. Ni mambo ya ajabu sana na yanatendeka chini ya Serikali hihi ya Mh. Magufuli. Binadamu wawili wanaweza kutesa mamia ya wafanyakazi kiasi hiki aliuliza mfanyakazi huyo?
Wakubwa wa Chuo wamefanya ufisadi wa pesa mpaka wamechoka, sasa wanaendelea na ufisadi wa ngono
Na Mwandishi Maalumu
Connect With Us