Close

Results 1 to 4 of 4
 1. #1
  Junior Member
  Join Date
  Mar 2016
  Posts
  28
  Rep Power
  0
  Likes Received
  1
  Likes Given
  0

  NATAMANI KAZI YA UKUU WA CHUO KAMA WA CHUO CHA UFUNDI ARUSHA

  Nimetafakari sana na kuona kama kazi pekee nzuri isiyokuwa na matatizo ni kuwa Mkuu wa Chuo kama Chuo cha ufundi Arusha. Nimetamani sana kupata kazi kama hiyo, ila sijui sifa inayotakiwa kupata kazi kama hiyo.

  Nikiwa Mkuu wa Chuo kama Chuo cha ufundi Arusha ninaweza kutengeneza Bodi yangu mwenyewe. Katika kutengeneza bodi yangu nitaweza kuweka hawara, rafiki na hata ndugu zangu.

  Nikiwa na ndugu, wajomba, shangazi, binamu na hata jamaa za rafiki zangu nitaweza kuagiza wakaajiriwa na kulipwa na Serikali bila shida yoyote.

  Nikitaka kupata pesa ya mara moja nitabuni safari, katika safari hiyo nitachukua fedha nyingi kuliko mahitaji lakini nikirudi nitaagiza risiti zitapatikana za kuonesha fedha yote ilitumika.

  Likitokea jambo nisilotaka nitawaita wajumbe wa Bodi yangu ambao ni jamaa zangu waje mara moja. Wakifika, nitawaambia waendelee kupata chakula na mapochopocho mengine yaliyoandaliwa kwa ajili yao huku bahasha zao za kaki zikiwa zinaandaliwa. Zikiwa tayari nitawaambia wajumbe kwamba mambo tuliyokubaliana atasaini Mwenyekiti kwa niaba yao. hapo tutaagana na kikao cha Bodi kitakuwa kimekwisha. Kikubwa nitahakikisha kila mmoja amesaini katika kitabu cha mahudhurio ya wajumbe wa Bodi, basi!

  Nitaandika chochote ninachotaka, baadaye nitampa mwenyekiti anasaini hatimaye wazo langu linakuwa azimio la Bodi. Mapato na matumizi ni mimi peke yangu ninayeyajua. Nikitaka pesa za haraka naagiza tu Mhasibu ananipatia, maana pesa zote za chuo ni kama za kwangu.

  Nikitaka pesa nyingi ninabuni mradi hewa pesa inalipwa najichukulia tu

  Akifanikiwa kuajiriwa mfanyakazi wa kike asiye ndugu yangu ni lazima afike nyumbani kwangu kama atataka kuendelea na kazi. Wakati huo sitakuwa na mke kwa kuwa atanikimbia baada ya kuwa mkuu wa chuo kama Chuo cha ufundi Arusha. Mke atanikimbia kwa sababu jeuri yangu wakati huo itakuwa kubwa, nitakuwa na pesa nyingi nitatembeatembea hovyo mpaka mke atajua na kuona hawezi kuvumilia ni bora aondoke aniache nikiponda maisha na kila mrembo atakayepita mbele yangu, kwani ni nini, pesa iko.

  Baada ya kutengeneza kila kitu kama ninavyotaka itabaki kazi moja tu kwangu, kuiba na kufanya kila aina ya ufisadi, na kuponda maisha nani ataniuliza?!
  Last edited by CHUNDA; 28-04-2016 at 11:59.

 2. #2
  Member
  Join Date
  Dec 2014
  Posts
  78
  Rep Power
  6
  Likes Received
  3
  Likes Given
  1

  Re: NATAMANI KAZI YA UKUU WA CHUO KAMA WA CHUO CHA UFUNDI ARUSHA

  Hiyo ni kazi nzuri sana ya kusomea.

  Sifa ya kuwa Mkuu wa Chuo kama hicho ni lazima uwe umesoma kuanzia shahada ya Kwanza mpaka shahada ya Uzamivu katika Chuo kikuu kimoja chenye jina la nchi unayosoma. Kwa mfano usome kuanzia shahada ya kwanza mpaka shahada ya Uzamivu katika Chuo kikuu cha Urusi, Yugoslavia, Hungary, Poland, Uholanzi nk.

  Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha alisoma kuanzia Shahada ya kwanza mpaka shahada ya Uzamivu Chuo kikuu cha Hungary, unafanya mchezo, kabukua huyu si mchezo. (Bachelor, Master, PhD vyote from University of Hungary) Kwanini usiwe na kiburi?!

 3. #3
  Junior Member
  Join Date
  Jan 2015
  Posts
  29
  Rep Power
  0
  Likes Received
  1
  Likes Given
  1

  Re: NATAMANI KAZI YA UKUU WA CHUO KAMA WA CHUO CHA UFUNDI ARUSHA

  Hungary ina idadi ya watu wanaokadiriwa 9.9 millioni kwa sensa iliyofanyika 2013. Nchi ya Hungaru ina vyuo vya elimu ya juu vyapatao 45.

  Katika vyuo hivyo hakuna Chuo kinachoitwa Hungary University. Kuna Chuo kinachoitwa University of West Hungary.

  Mambo ya Kihiyo yalianza hivihivi, angalieni, usije ukakuta Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha ni Kihiyo! Hii ni kazi kwa TCU kufuatilia uhalali wa elimu ya msomi huyo. Maana Kihiyo kusimamia Taaluma, ni jambo la ajabu, inaweza kuingizwa kwenye kumbukumbu ya maajabu ya Dunia ikiwa hivyo.

 4. #4
  TUA
  TUA is offline
  Senior Member
  Join Date
  Oct 2014
  Posts
  677
  Rep Power
  6
  Likes Received
  32
  Likes Given
  0

  Re: NATAMANI KAZI YA UKUU WA CHUO KAMA WA CHUO CHA UFUNDI ARUSHA

  Quote Originally Posted by CHUNDA View Post
  Nimetafakari sana na kuona kama kazi pekee nzuri isiyokuwa na matatizo ni kuwa Mkuu wa Chuo kama Chuo cha ufundi Arusha. Nimetamani sana kupata kazi kama hiyo, ila sijui sifa inayotakiwa kupata kazi kama hiyo.

  Nikiwa Mkuu wa Chuo kama Chuo cha ufundi Arusha ninaweza kutengeneza Bodi yangu mwenyewe. Katika kutengeneza bodi yangu nitaweza kuweka hawara, rafiki na hata ndugu zangu.

  Nikiwa na ndugu, wajomba, shangazi, binamu na hata jamaa za rafiki zangu nitaweza kuagiza wakaajiriwa na kulipwa na Serikali bila shida yoyote.

  Nikitaka kupata pesa ya mara moja nitabuni safari, katika safari hiyo nitachukua fedha nyingi kuliko mahitaji lakini nikirudi nitaagiza risiti zitapatikana za kuonesha fedha yote ilitumika.

  Likitokea jambo nisilotaka nitawaita wajumbe wa Bodi yangu ambao ni jamaa zaangu waje mara moja. Wakifika, nitawaambia waendelee kupata chakula na mapochopocho mengine yaliyoandaliwa kwa ajili yao huku bahasha zao za kaki zikiwa zinaandaliwa. Zikiwa tayari nitawaambia wajumbe kwamba mambo tuliyokubaliana atasaini Mwenyekiti kwa niaba yao. hapo tutaagana na kikao cha Bodi kitakuwa kimekwisha. Kikubwa nitahakikisha kila mmoja amesaini katika kitabu cha mahudhurio ya wajumbe wa Bodi, basi!

  Nitaandika chochote ninachotaka, baadaye nitampa mwenyekiti anasaini hatimaye wazo langu linakuwa azimio la Bodi. Mapato na matumizi ni mimi peke yangu ninayeyajua. Nikitaka pesa naagiza tu Mhasibu ananipatia, maana pesa zote za chuo ni za kwako.

  Akifanikiwa kuajiriwa mfanyakazi wa kike asiye ndugu yangu ni lazima afike nyumbani kwangu kama atataka kuendelea na kazi. Wakati huo sitakuwa na mke kwa kuwa atanikimbia baada ya kuwa mkuu wa chuo kama Chuo cha ufundi Arusha. Mke atanikimbia kwa sababu jeuri yangu wakati huo itakuwa kubwa, nitakuwa na pesa nyingi nitatembeatembea hovyo mpaka mke atajua na kuona hawezi kuvumilia ni bora aondoke aniache nikiponda maisha na kila mrembo atakayepita mbele yangu, kwani ni nini, pesa iko.

  Baada ya kutengeneza kila kitu kama ninavyotaka itabaki kazi moja tu kwangu, kuiba na kufanya kila aina ya ufisadi, na kuponda maisha nani ataniuliza?!
  Pia nitahakikisha kuwa katika kuwalipa wajumbe wa bodi, kila mmoja atasaini katika karatasi yake ili asiwepo yeyote atakayejua mwenzake amelipwa ngapi. Sasa hapo ni rahisi hata huyo mpenzi wangu kupata bulungutu ambapo haitajulikana. Ubosi bwana, raha tu!

Posting Permissions

 • You may not post new threads
 • You may not post replies
 • You may not post attachments
 • You may not edit your posts
 •