Close

Results 1 to 5 of 5
 1. #1
  Junior Member
  Join Date
  Feb 2015
  Posts
  25
  Rep Power
  0
  Likes Received
  0
  Likes Given
  0

  VIONGOZI WANAPOAMUA KUFANYA KAZI YA UMMA KAMA MALI YAO

  Imekuwa kama jambo la kawaida kwa Menejimenti ya Chuo cha Ufundi Arusha kufanya mambo yoyote watakayo kana kwamba chuo hiki ni mali yao. Mara kwa mara wamekuwa wakisikika kusema kwamba chuo ni mali yao na mfanyakazi ambaye hakubaliani na wanachofanya mlango uko wazi aondoke awaachie chuo chao.

  Malalamiko ya Ajira za upendeleo ni mengi ila wenye chuo chao hawasikii kelele za chura. Malalamiko ya Ufisadi ni nyingi sana ila wenye chuo chao wamekataa kusikiliza kelele za chura. Uonevu wa aina mbalimbali unafanywa kwa wafanyakazi ila wenye chuo chao wamekataa kusikiliza kelele za chura.

  Wakati Chuo kikiwa na hali mbaya kifedha wenye chuo chao wasomi wa shahada za udakitari wa falsafa Dkt Richard Masika na Dkt Masudi Senzia watakuwa safarini kuanzia tarehe 26/04/2015 mpaka tarehe 30/04/2015 kula maisha Jijini Dar es Salaam na pengine watakuwa na viburudisho vyao.

  Haya yanafanyika wakati ambapo Mkuu wa Nchi na Serikali Rais Magufuli amepiga marufuku safari zisizo na tija na kutaka fedha ya umma kutumika kwa uangalifu ili mwananchi wa kawaida aweze kupata ahueni ya maisha. Waku hawa wenye chuo chao wamepuuza Amri ya Rais, lakini zaidi ni kwamba Chuo kina mzigo mkubwa wa madeni ambayo haijulikani yatalipwa lini na kwa namna gani.

  Kitendo cha Serikali kuacha kuchukua hatua kutafuta suluhisho la kudumu katika chuo linaweza kusababisha madhara makubwa sana siku za mbeleni. Wafanyakazi wasiokuwa na furaha na kazi yao na hasa waalimu ambao wanafundisha mamia ya wanafunzi, katika nyanja mbalimbali za utaalamu wakifanya kazi chini ya kiwango kwa sababu ya morali kuwa chini ni kuuwa kizazi na Taifa.

  Hali hii haina tofauti na kutaka kuleta hujuma ya kujitakia. Wafanyakazi wana haki ya kujaliwa, Menejimenti isitegemee tija kwa kuburuza wafanyakazi. Mbaya zaidi ni pale ambapo wachache wanajinufaisha binafsi kwa kutumia nafasi zao vibaya kwa kufanya ufisadi na kunyanyasa wafanyakazi wenzao
  Last edited by SUBIRA; 22-04-2016 at 07:54.

 2. #2
  Member
  Join Date
  Dec 2014
  Posts
  78
  Rep Power
  6
  Likes Received
  3
  Likes Given
  1

  Re: VIONGOZI WANAPOAMUA KUFANYA KAZI YA UMMA KAMA MALI YAO

  Ufisadi umewanogea mpaka wanavunja amri ya Rais?

  Hata hivyo sishangai, maana imeelezwa kwamba Menejimenti ya Chuo iliwahi hata kuingilia Madaraka/Mamlaka ya Rais kwa kukaimisha Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo kwa Rafiki yao ili tu aweze kulinda masilahi yao. Baada ya kukaimisha Mwenyekiti wa Bodi vikao vya Bodi viliendelea kama kawaida.

  Wafanyakazi walijiuliza sana, kama Menejimenti inaweza kukaimisha Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo na vikao vikaendelea, ni nini maana au nafasi ya Rais kuteua Mwenyekiti wa Bodi?

  Mkuu wa Chuo na Msaidizi wake wote watakuwa na safari ya Dar kwenda wapi au kufanya nini? Wanakwenda kufanya kazi maalumu?

 3. #3
  Member
  Join Date
  Feb 2015
  Posts
  56
  Rep Power
  6
  Likes Received
  0
  Likes Given
  0

  Re: VIONGOZI WANAPOAMUA KUFANYA KAZI YA UMMA KAMA MALI YAO

  JPM AKIJA HIVI, NAO WANAKUJA VILE. NILIINGIA OFISI MOJA NYETI NIKAKUTA MAANDALIZI YA SAFARI YAO YAKISHUGHULIKIWA, LAKINI KWA USIRI. HAYA BANA!

 4. #4
  Senior Member
  Join Date
  Jun 2015
  Posts
  722
  Rep Power
  5
  Likes Received
  23
  Likes Given
  1

  Re: VIONGOZI WANAPOAMUA KUFANYA KAZI YA UMMA KAMA MALI YAO

  hayo yanafanywa kufuatia mauzauza ya serikali ya awamu ya tano kuonekana kuwavalia njuga mafisadi kumbe kinyume chake wanawapa ahueni kabla ya hiyo mahakama ya mafisadi haijaanza wanafungulia wahalifu na kuwa acha huru nisawa na "Askari kumfungulia muhalifu na kuanza kumkimbiza na pale anapo mkaribia anamwambia ongeza mwendo" kwahiyo hao viongozi wa chuo hicho wanajua rais anaweza kuwatumbua tuu nasio kuwachukulia hatua ndio maana wanakuwa na jeuri
  punda hajasoma lakini kazi hakosi

 5. #5
  Junior Member
  Join Date
  Mar 2016
  Posts
  28
  Rep Power
  0
  Likes Received
  1
  Likes Given
  0

  Re: VIONGOZI WANAPOAMUA KUFANYA KAZI YA UMMA KAMA MALI YAO

  MKUU WA CHUO NI KAMA AMEAMUA KWAMBA SASA ATALII TU. NI JANA TU ALIREJEA KUTOKA ZIARANI ZANZIBAR NA DAR ES SALAAM. ATAKUWA OFISINI JUMATATU TAREHE 25/04/2016, LAKINI, JUMATANO TAREHE 27/04/2016 ATAONDOKA KURUDI DAR. SAFARI HII MKUU WA CHUO ATAAMBATANA NA MSAIDIZI WAKE WA KARIBU. HUYU MSAIDIZI WAKE WA KARIBU NI DKT MASUDI SENZIA YULE WALIYEGAWANA NA MKUU WA CHUO ZAIDI YA MATOFALI 20,000.

  MATOFALI HAYA YANA UTATA KWA KUWA IKIANGALIWA YALIVYOPIGWA NI KAMA MALI YA CHUO, UKIANGALIA KWA UPANDE MWINGINE NI KAMA MALI YA MKANDARASI. SASA NI KAMA WALIPEWA NA MKANDARASI NA WAO VI VIONGOZI NI SAWA NA RUSHWA YA MOJA KWA MOJA. KAMA NI MALI YA CHUO BASI WATAKUWA WAMETUMIA MADARAKA YAO KUCHUKUA MALI YA UMMA.

  MATOFALI 20,000 YANATOSHA KUJENGA MADARASA 20 AU SHULE MBILI ZA KATA PAMOJA NA NYUMBA ZA WAALIMU. KAMA AMBAVYO ILIKWISHAELEZWA MATOFALI HAYO YALITUMIKA KUJENGA NYUMBA YA MKUU WA CHUO ILIYOKO KARIBU NA TEMDO NJIRO ARUSHA NA MABANDA ENEO LA VIWANJA VYA GHALI VILIVYO USA PAMOJA NA NYUMBA YA DKT MASUDI ILIYOKO USA ARUSHA.

  HUKU IKIWA RAIS AMEPIGA MARUFUKU SAFARI ZA KUJIPATIA VIPATO KWA HASARA YA SERIKALI, WENZETU HAWA WAMEAMUA KUPUUZA NA KUAMUA KUSAFIRI MARA KWA MARA ILI KUENDELEA KUPATA VIPATO MAANA WALIKWISHAZOEA KUPATA PESA ZISIZO NA JASHO KILA SIKU. TUNASUBIRI TUONE MAMBO YATAKWENDA KWA JINSI YA NAMNA HII MPAKA LINI!

Posting Permissions

 • You may not post new threads
 • You may not post replies
 • You may not post attachments
 • You may not edit your posts
 •