Close

Page 1 of 2 12 LastLast
Results 1 to 25 of 42
 1. #1
  Junior Member
  Join Date
  Mar 2016
  Posts
  26
  Rep Power
  0
  Likes Received
  0
  Likes Given
  0

  JIPU LAKATAA KUJITUMBUA WALA KUTUMBULIWA

  Click image for larger version. 

Name:	Masika.jpg 
Views:	211 
Size:	12.7 KB 
ID:	1452 Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha, Dkt Richard Masika Mushi

  Hivi ndivyo inavyoweza kusemwa maana hakika habari za ufisadi na matumizi mabaya ya ofisi yanayofanywa na Menejimenti ya Chuo cha Ufundi Arusha (ATC) ni mambo yanayofahamika kwa wanajumuiya ya chuo na pia yameripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari.

  Si jambo la siri kwamba Menejimenti ya chuo (ATC) imefanikiwa kufanya chuo hiki ambacho ni mali ya serikali chini ya Wizara ya Elimu kama shamba la bibi. Hivi sasa zinafanyika jitihada kubwa ili kuweza kufukia baadhi ya maeneo yanayoweza kufukiwa kwa kupika mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na taarifa ya idadi ya wanafunzi pamoja na idadi ya wafanyakazi katika vipindi tofauti tofauti.

  Katika hali ya usiri mkubwa, kuna jitihada kubwa sana zinafanywa za kununua risiti za malipo mbalimbali kuanzia mwaka 2010/11 ili zitumike kujazia maeneo yenye mashaka. Kuna mashaka makubwa kwa uongozi wa chuo kuwa kampuni ya ukaguzi ya MM Micro Business Consultants waliokuwa wakifanya kazi za ukaguzi wa hesabu za Chuo kwa muda wa miaka 6 mfululizo inaweza isiendelee na kazi ya ukaguzi wa hesabu za chuo kuanzia mwaka huu wa fedha 2016/17 kama ilivyokuwa imezoeleka.

  Katika kipindi cha kuanzia mwaka 2010 mpaka sasa kuna hujuma, ufisadi na matumizi mabaya ya ofisi yamekuwa yanafanyika lakini hakuna hatua za makusudi zilizochukuliwa kurekebisha hali hiyo kwa kuwa inafahamika kwamba kwa kiwango kikubwa Bodi ya chuo ni sehemu ya ufisadi huu unaolalamikiwa na wafanyakazi wengi.

  Kwa kutambua kwamba sehemu kubwa ya hesabu za chuo haijakaa vizuri na kwa kutambua kwamba Mkaguzi wa hesabu za chuo anaweza kubadilika na kwa kutambua kwamba Serikali ya Rais Magufuli haina mchezo na watendaji wanaoonesha dalili za tabia mbaya ya wizi wa mali za serikali risiti za kufukia mashimo yaliyopo zinatafutwa kwa nguvu kubwa.

  Pamoja na kutumia ujanja huu pamoja na kufanya ushawishi wa kulainisha baadhi ya watendaji wasio waaminifu kwa njia ya kutumia fedha hiihii iliyopatikana kwa njia ya ufisadi lakini bado uongozi wa chuo una hofu ya kutumbuliwa na Serikali makini ya Rais Magufuli. Hata hivyo huenda mbinu za menejimenti hii zikafanikiwa na hivyo kutoguswa licha ya ukweli unaojulikana kwamba kuna ufisadi uliofanywa chuoni. Hili ni tatizo kubwa kwani licha ya kuliingizia Taifa hasara, Ustawi wa chuo unazidi kudorora siku hadi siku hasa ikizingatiwa kwamba mishahara ya watumishi wapatao 25 ilitumika au ililiwa kwa njia ya kifisadi katika mazingira yenye utata mkubwa.

  Menejimenti inayotuhumiwa na kulalamikiwa kwa kujichotea fedha za umma bila kujali imekataa kuwajibika walao kupisha uchunguzi. Pia Bodi ya chuo imeshindwa kuchukua hatua zozote licha ya taarifa kusambaa chuoni kwamba kuna kila dalili kwamba viongozi watatu wa juu wa chuo ni majipu. Zaidi ya kiasi cha Tsh 3,600,000,000/= kinakadiriwa kuliwa kwa njia za kifisadi. Hiki ni kiasi kikubwa sana cha fedha ya walipa kodi, na ni kiasi kikubwa sana kwa kuzingatia kwamba wanafunzi wengi wanataabika kwa kukaa mitaani kwa kukosa mabweni ya kulala.

  Mmoja wa watuhumiwa wanaodaiwa kuwa ni majipu, alisikika akijitapa kwamba “ukiwa mtu wa mfumo hupati shida hata siku moja. Tumepiga mahela ya nguvu hapa lakini TAKUKURU wanatuamkia Shikamoo, kuna hata bosi wao mmoja alihamishwa alipewa kiasi cha kutosha kujenga nyumba, hao bwana wadogo watapiga kelele tu”. Mkuu wa Chuo pale, ana network kubwa ukienda ofisini kwake ana picha alizopiga na waheshimiwa kibao, unafanya mchezo, alisikika akijigamba bosi huyo.

  Mtuhumiwa huyo aliendelea kusema “ukiona watu wakitangaza kwenye vyombo vya habari wametumbua majipu elewa kuna chuki binafsi bradha, hakuna cha majipu wala nini” Unategemea mtu mwenye mtandao mpana kama Masika atumbuliwe? Aliuliza BOSI huyo anayependa sana kuitwa BOSI. Huenda maneno ya BOSI huyu yakawa na ukweli fulani. Ikiwa kuna ukweli kwa aliyosema bosi huyu, basi Serikali ya Mh Rais Magufuli itakuwa na kazi ya ziada ya kupiga vita na kuondokana na UFISADI serikalini.

  Pamoja na maneno ya BOSI huyu, bado wanajumuiya wengi wa chuo pamoja na wananchi wengi wana imani na kazi nzuri anayoifanya Rais Magufuli na pia kazi nzuri inayofanywa na Waziri wa Elimu Profesa Ndalichako. Hatua kwa hatua watafika Chuo cha Ufundi Arusha na hapo watapata kujua ukweli wote na kurekebisha kila kinachofaa kurekebishwa.
  Last edited by Juma Joseph; 21-07-2016 at 21:03.

 2. #2
  Senior Member
  Join Date
  Aug 2015
  Posts
  2,802
  Rep Power
  7
  Likes Received
  89
  Likes Given
  66

  Re: JIPU LAKATAA KUJITUMBUA WALA KUTUMBULIWA

  Ukiona kama Serikali inashindwa kuchukua hatua jua basi kuna kigogo hapo anahusika na huo ufisadi

 3. #3
  TUA
  TUA is offline
  Senior Member
  Join Date
  Oct 2014
  Posts
  677
  Rep Power
  6
  Likes Received
  32
  Likes Given
  0

  Re: JIPU LAKATAA KUJITUMBUA WALA KUTUMBULIWA

  Inawezekana Francis, hii ni kwa sababu mwaka 2013 menejiment ya Chuo hiki iliripotiwa katika vyombo vya habari kufuja kwa njia ya malipohewa na kuingiza mifukoni mwao zaidi ya shilingi 290,000,000/= lakini hakuna hatua yeyote iliyochukuliwa. Ni hivi majuzi tena imeripotiwa na vyombo vya habari jinsi jengo la madarasa lilivyotafuna kwa njia za ufisadi kiasi cha shilingi bilioni 1.4 kwa kile kinachoitwa ni variations za jengo hilo. Variations hizo ziliripotiwa kufikia kiasi cha 52% ambazo ni kinyume kabisa na sheria ya manunuzi ya umma ya mwaka 2011, inayosema kuwa gharama kwenye mradi wowote wa serikali isizidi 20%. Inawezekana ni kweli kuna kigogo anahusika pia na ulaji wa hela hapo, na mara nyingi imedaiwa kuwa menejiment ya Chuo hicho imesikika hata ikibeza taasisi za serikali za uchunguzi kama vile TAKUKURU kuwa hawana lolote, wakifuatwa na vyombo hivyo watawapa tu hela wataondoka. Ni jambo la kujiuliza, kama kwenye ujenzi sheria ya manunuzi imekiukwa kiasi hiki alafu wahusika wawe na kiburi hivi kuna nini? Kuna kitu!

 4. #4
  Senior Member
  Join Date
  Sep 2014
  Posts
  468
  Rep Power
  6
  Likes Received
  28
  Likes Given
  17

  Re: JIPU LAKATAA KUJITUMBUA WALA KUTUMBULIWA

  Quote Originally Posted by Juma Joseph View Post
  Hivi ndivyo inavyoweza kusemwa maana habari za ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka yanayofanywa na Menejimenti ya Chuo cha Ufundi Arusha (ATC) zimeripotiwa Serikalini mara kwa mara.

  Ni dhahiri kwamba licha ya kashifa nyingi za ufisadi uliofanywa na kuendelea kufanywa na Menejimenti ya Chuo cha Ufundi Arusha hakuna hatua zozote zilizochukuliwa au zinazopangwa kuchukuliwa ili kutatua kero hiyo. Hii ni kero kubwa kwani licha ya kuliingizia Taifa hasara, Ustawi wa chuo unazidi kudorora siku hadi siku.

  Menejimenti inayolaumiwa na kulalamikiwa kwa kujichotea fedha za umma bila kujali imekataa kuwajibika walao kupisha uchunguzi. Pia mamlaka za juu zimeshindwa kuchukua hatua zozote baada ya tetesi kusambaa kwamba majipu hayo yamejiimarisha sana na mfumo wa Serikali ya JPM.

  Moja ya walalamikiwa hao alisikika akijitapa kwamba “ukiwa mtu wa mfumo hupati shida hata siku moja. Tumepiga mahela ya nguvu hapa lakini TAKUKURU wanatuamkia Shikamoo, hao bwana wadogo watapiga kelele tu”. Mkuu wa Chuo pale, ukienda ofisini kwake ana picha alizopiga na mheshimiwa Rais, unafanya mchezo, alisikika akijigamba mlalamikiwa huyo.

  Mlalamikiwa huyo aliendelea kusema kwamba “ukiona watu wakitangaza kwenye vyombo vya habari wametumbua majipu elewa wana chuki binafsi bradha, hakuna cha majipu wala nini” Unategemea mtu mwenye mtandao mpana kama Masika atumbuliwe? Aliuliza BOSI huyo anayependa sana kuitwa bosi.

  Huenda maneno ya BOSI huyu yana ukweli. Ikiwa ni kweli, basi Serikali ya Mh Rais itakuwa na safari ndefu sana kupiga vita na kuondokana na UFISADI Serikalini
  Hii ni kali, katika awamu hii bado kuna watendaji wenye kiburi kiasi hicho? Ikiwa hivyo ndivyo ilivyo, basi mwendo wa KUJUANA kutalimaliza TAIFA na kusonga mbele itaweza kuwa ndoto

 5. #5
  Member
  Join Date
  Dec 2014
  Posts
  78
  Rep Power
  6
  Likes Received
  3
  Likes Given
  1

  Re: JIPU LAKATAA KUJITUMBUA WALA KUTUMBULIWA

  Matumizi ya fedha za mafunzo viwandani (IPT) kiasi cha TZS 320,000,000/= zina utata. Utata wa fedha za mafunzo viwandani ni kuanzia 2011/12 – 2014/2015. Kwa miaka minne mfululizo kiasi cha 80,000,000/= zimekua hazijulikani zimefanyia kitu gani au zimekwenda wapi.

  Kwa mfano:
  Katika mwaka wa masomo 2011/12 Serikali kupitia Wizara ya Elimu ilipeleka Chuoni kiasi cha Tsh 546,743,000/= kwa ajili ya Mafunzo viwandani kwa wanafunzi na waalimu kwenda kuwakagua viwandani. (Zaidi ya Tsh 80,000,000/= zilitokomea kusikojulikana)

  Katika mwaka wa masomo 2012/13 Serikali kupitia Wizara ya Elimu ilipeleka Chuoni kiasi cha Tsh 559,860,000/= kwa ajili ya Mafunzo viwandani kwa wanafunzi na waalimu kwenda kuwakagua viwandani.(Zaidi ya Tsh 80,000,000/= zilitokomea kusikojulikana)

  Hayo ndio mambo ya menejimenti ya chuo na wajumbe wa Bodi yake ambao kwa sura na mtazamo ni sehemu ya familia ya Mkuu wa Chuo.
  Last edited by Tembo; 06-05-2016 at 19:18.

 6. #6
  Member
  Join Date
  Dec 2014
  Posts
  78
  Rep Power
  6
  Likes Received
  3
  Likes Given
  1

  Re: JIPU LAKATAA KUJITUMBUA WALA KUTUMBULIWA

  Pengine sababu za Mkuu Chuo kuitwa JIPU ni hizi:

  1) Matumizi ya fedha za mafunzo viwandani (IPT) kiasi cha TZS 320,000,000/= zina utata.
  Utata wa fedha za mafunzo viwandani ni kuanzia 2011/12 – 2014/2015. Kwa miaka minne mfululizo kiasi cha 80,000,000/= kila mwaka hazijulikani zilikwenda wapi au zilifanya nini.

  2) Matumizi ya fedha za mishahara ya wafanyakazi mwezi Januari 2014 kwa wafanyakazi walioajiriwa Desemba 2013. Wastani wa TZS 30,000,000/= za mishahara hazijulikani zilikwenda wapi au zilifanya nini

  3) Miradi hewa ya ujenzi ililipwa wastani wa TZS 400,000,000/=

  4)Matumizi ya malipo hewa ya miradi ya ujenzi kupitia ATC-PCB, wastani wa TZS 250,000,000/=

  5) Matumizi ya upanuzi wa jengo la Utawala, wastani wa TZS 700,000,000/=

  6) Matumizi ya ujenzi wa jengo la Umwagiliaji lililogharimu TZS 4,000,000,000/=. Wastani wa TZS 2,500,000,000/= zinakadiriwa kutosha kujenga jengo hili na hasa ikizingatiwa kwamba matofali na shughuli nyingine kama paa na madirisha zilifanywa kwa rasilimali za Chuo. Wastani wa TZS 1,500,000,000/= zinadaiwa kutumika kifisadi. Kadhalika zaidi ya matofali 20,000 yalichukuliwa na Uongozi kwa matumizi binafsi.

  7) Matumizi ya fedha za msaada shamba la Oljoro wastani wa TZS 400,000,000/=

  8) Matumizi ya fedha zinazokatwa kutoka mishahara ya wafanyakazi kwa ajili ya ukarabati wa nyumba wastani wa TZS 300,000,000/=

  Kwa wastani, zaidi ya TZS 3.5 Billioni hazijulikani ziko wapi au zilifanyia nini
  Last edited by Tembo; 06-05-2016 at 19:42.

 7. #7
  TUA
  TUA is offline
  Senior Member
  Join Date
  Oct 2014
  Posts
  677
  Rep Power
  6
  Likes Received
  32
  Likes Given
  0

  Re: JIPU LAKATAA KUJITUMBUA WALA KUTUMBULIWA

  Kipekee nimefurahishwa sana na kauli ya Mh. Waziri Mkuu alipokuwa kwenye mkutano wa Kupambana na Rushwa huko LONDON ambako alimwakilisha Mh. Rais. Napata Faraja sana kwani hata nchi kama Uingereza wameonyesha kuridhika jinsi ambavyo Serikali ya JPM inavyoshughulika na ulaji rushwa. Amesema Serikali itawachukulia hatua kali wote waliokula mishahara hewa na waliosababisha hiyo mishahara hewa. Sisi wafanyakazi wa Chuo Cha ufundi Arusha tunachomuomba Mh. Waziri mkuu ni kushughulikia na kuwachukulia hatua kali uongozi wa Chuo cha Ufundi Arusha kwa kitendo Chao cha kula mishahara ya wafanyakazi wapatao 25. Mishahara hii ni ya January, 2014.
  Kama Kiongozi wa Taasisi anaweza kunyima mishahara ya Watumishi wenzake na akaamua kuitumia kibabe aidha yeye mwenyewe au kwa matumizi mengine ya Chuo, huyu si kwamba ni mwizi bali anadhalilisha pia serikali. Kama Mkuu wa Taasisi anaweza kutumia mishahara ya wafanyakazi waliopo kazini si kuwanyanyasa huko? Je uongozi wa aina hii ni mishahara mingapi hewa wamekula?
  Uongozi huu pamoja na bodi ya Chuo umelitia hasara kubwa taifa kwa kitendo cha kufanya ufisadi ambao kila mfanyakazi anajiuliza, inakuwaje wapo ofisini mpaka sasa hivi, baada ya kufanya wizi wa wazi wa kiasi cha Tsh 1.5 bilioni katika mradi wa ujenzi wa Jengo la umwagiiaji. Halafu haikutosha wakachukua matofali yapatayo 20,000 kwenda kujengea nyumba zao binafsi. Hii ni fedhea kwa Serikali, Mh. JPM na Mh Waziri mkuu, wafanyakazi tunaona uchungu sana hasa pale tunapoona bado Chuo hakina mabweni kwa ajili ya wanafunzi, na watu kuchota hela kiasi hiki huku wakiendelea kudunda kwenye ofisi za umma.
  Tunaomba Serikali ichukue hatua, wafanyakazi tunaendelea kuona uchungu pale waaribifu wanapoendelea kukaa ofisini na kuendelea kufanya udanganyifu kwa mambo yaliyo wazi.

 8. #8
  Member
  Join Date
  Feb 2015
  Posts
  56
  Rep Power
  6
  Likes Received
  0
  Likes Given
  0

  Re: JIPU LAKATAA KUJITUMBUA WALA KUTUMBULIWA

  Quote Originally Posted by Tembo View Post
  Pengine sababu za Mkuu Chuo kuitwa JIPU ni hizi:

  1) Matumizi ya fedha za mafunzo viwandani (IPT) kiasi cha TZS 320,000,000/= zina utata.
  Utata wa fedha za mafunzo viwandani ni kuanzia 2011/12 – 2014/2015. Kwa miaka minne mfululizo kiasi cha 80,000,000/= kila mwaka hazijulikani zilikwenda wapi au zilifanya nini.

  2) Matumizi ya fedha za mishahara ya wafanyakazi mwezi Januari 2014 kwa wafanyakazi walioajiriwa Desemba 2013. Wastani wa TZS 30,000,000/= za mishahara hazijulikani zilikwenda wapi au zilifanya nini

  3) Miradi hewa ya ujenzi ililipwa wastani wa TZS 400,000,000/=

  4)Matumizi ya malipo hewa ya miradi ya ujenzi kupitia ATC-PCB, wastani wa TZS 250,000,000/=

  5) Matumizi ya upanuzi wa jengo la Utawala, wastani wa TZS 700,000,000/=

  6) Matumizi ya ujenzi wa jengo la Umwagiliaji lililogharimu TZS 4,000,000,000/=. Wastani wa TZS 2,500,000,000/= zinakadiriwa kutosha kujenga jengo hili na hasa ikizingatiwa kwamba matofali na shughuli nyingine kama paa na madirisha zilifanywa kwa rasilimali za Chuo. Wastani wa TZS 1,500,000,000/= zinadaiwa kutumika kifisadi. Kadhalika zaidi ya matofali 20,000 yalichukuliwa na Uongozi kwa matumizi binafsi.

  7) Matumizi ya fedha za msaada shamba la Oljoro wastani wa TZS 400,000,000/=

  8) Matumizi ya fedha zinazokatwa kutoka mishahara ya wafanyakazi kwa ajili ya ukarabati wa nyumba wastani wa TZS 300,000,000/=

  Kwa wastani, zaidi ya TZS 3.5 Billioni hazijulikani ziko wapi au zilifanyia nini
  Du! sasa hii kweli ni kufuru. Mheshimiwa Rais wafanyakazi tunaomba uchukue hatua. Bodi hii na menejiment hii inatia Serikali aibu. Pia wafanyakazi tuna fikia hatua ya kukata tamaa sana kiuwajibikaji kwani haiwezekani mahela yote haya yaingie mifukoni mwa watu binafsi ilhali wengine tunateseka. Miradi mingi ya Ujenzi hapa Chuoni imekuwa inajengwa Chini ya kiwango kwa sababu ya watu kutafuna mapesa huku serikali ipo.
  Lakini jingine ambalo Wafanyakazi tunajiuliza ni kwamba kwa nini sehemu zingine walioleta hasara hivi wamesimamishwa na uchunguzi kuendelea,je hapa Chuo cha Ufundi Arusha kuna nini? Mbona menejiment ya Chuo hiki imejihusisha na wizi wa Waziwazi hasa katika mradi wa jengo la umwagiliaji ambapo kiasi cha Tsh 1.4 bilioni zimeibwa mchana kweupe lakini wahusika hawachukuliwi hatua?
  Mbona mishahara ya wafanyakazi imeliwa waziwazi na menejiment ya Chuo hiki lakini hawachukuliwi hatua? Mheshimiwa Rais, tunapongeza sana kazi yako, lakini tutapongeza zaidi pale utakapotupa jicho hapa Chuo cha Ufundi Arusha.

 9. #9
  Member
  Join Date
  Dec 2014
  Posts
  78
  Rep Power
  6
  Likes Received
  3
  Likes Given
  1

  Re: JIPU LAKATAA KUJITUMBUA WALA KUTUMBULIWA

  kama inavyofahamika Mkuu wa Chuo ni Mchaga. Mkuu kwa kutumia madaraka yake alipendekeza na hivyo kuweza kumshauri vibaya Waziri (mislead) na hivyo kuteua wajumbe wa Bodi kwa kuangalia maslahi ya Mkuu wa chuo.

  Wajumbe wa Bodi ya chuo ni Abrahamu Nyanda (Family friend); Christian Nyahumwa (School mate); Suzan Mnafe (Mchaga & girlfriend); Lyne Ukio (Mchaga); Hyacintha Makileo (Mchaga); Karoli Njau (Mchaga); Benedict Lema (Mchaga & School mate); Namnyaki Mattasia (Girlfried); Thomas Katebalirwe (Mwakilishi wa Wizara/amekuwa akilainishwa kwa bahasha iliyonona); Mbitila Shija (Mwalimu/mfanyakazi wa chuo) na Pius Paul (Mwanafunzi/serikali ya wanafunzi)

  Sasa hivi inasemekana Abrahamu Nyanda amemaliza muda wake na hivyo, Mkuu wa Chuo alimteua Christian Nyahumwa (School mate) kuwa Kaimu Mwenyekiti wa Bodi na kwa maana hiyo Bodi kuendelea na majukumu yake kama kawaida. Ikumbukwe kwamba, nafasi ya Mwenyekti wa Bodi ya chuo huteuliwa na Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Kutokana na miongozo ya NACTE, Mkuu wa chuo alitakiwa kulipwa mshahara kwa ngazi ya PHTS 12 katika mwaka 2011 mpaka 2014. Lakini kwa kutumia madaraka hayohayo, Mkuu alkulipwa kama ifuatavyo:

  Mwaka 2011/12 alitakiwa kulipwa Tsh 3,330,700/=, lakini alilipwa kiasi cha Tsh 4,303,400/= kwa mwezi

  Mwaka 2012/13 alitakiwa kulipwa Tsh 3,697,000/=, lakini alilipwa kiasi cha Tsh 4,734,000/= kwa mwezi

  Mwaka 2013/14 alitakiwa kulipwa Tsh 3,837,000/=, lakini alilipwa kiasi cha Tsh 4,823,000/= kwa mwezi

  Tanzania bila ufisadi inawezekana. Tushirikiane kutokomeza ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka nchini ili kama Taifa tuweze kupata maendeleo. Tumsaidie Rais kupiga vita ufisadi Tanzania.
  Last edited by Tembo; 16-05-2016 at 08:52.

 10. #10
  TUA
  TUA is offline
  Senior Member
  Join Date
  Oct 2014
  Posts
  677
  Rep Power
  6
  Likes Received
  32
  Likes Given
  0

  Re: JIPU LAKATAA KUJITUMBUA WALA KUTUMBULIWA

  Wakati anahamia Arusha, bahati nzuri tulishasikia kwamba huko DIT alikuwa anasumbua sana wafanyakazi, fitna na majungu. Alipofika Arusha akiwa mgeni akaanza kutengeneza makundi, kugawa watu na hata kukosanisha wafanyakazi. Leo wadau nimefanikiwa kukumbuka moja ya Kauli zake alipoulizwa swali zuri sana na mdau mmoja. Nanukuu!
  MDAU: "Mheshimiwa, lakini tunasikia huko unakotokea DIT umekuwa mara nyingi na uhusiano mbaya na wafanyakazi wenzako", hili unalionaje?
  MASIKA: "Unajua bwana wizara ya Elimu iko pale karibu na DIT hivyo watu wote walioshindikana pale Wizarani huwa wanaletwa DIT, na hivyo kuwaongoza ni vigumu sana". Mwisho wa kunukuu.
  Sasa najiuliza Hapa Chuo cha Ufundi Arusha ambako amegeuza wafanyakazi kada ya waalimu kuwa maadui zake karibu wote, hawa nao wametoka wizarani?
  Kwa kweli Richard Masika anashangaza wafanyakazi wengi kwa sasa. Amefanikiwa kujilipa mshahara wa Profesa, bado haridhiki, bado akala mishahara ya wafanyakazi waliokuja kuanza kazi januari, 2014. Huu ni ubinafsi mmbaya sana.
  Hapa itafika wakati kama Serikali haimchukulii hatua, basi hata ufanisi wa kazi kwa wafanyakazi utashuka sana, kwa kuwa kwa sasa wafanyakazi wamekata tamaa baada ya yeye (Masika) kujihusisha na vitendo vya ufisadi ambavyo vimerudisha Chuo nyuma sana. Miradi mingi ya hapa Chuoni imegubikwa na kashfa za ufisadi na 10% na mingi ya miradi hii imegundulika kujengwa chini ya viwango.
  Bodi aliyoiteuwa ya wachagga wenzake na wengine classmate wameonyesha kuwa wao wanachojua ni hela tu, hakuna wanachosimamia.

 11. #11
  Member
  Join Date
  Dec 2014
  Posts
  78
  Rep Power
  6
  Likes Received
  3
  Likes Given
  1

  Re: JIPU LAKATAA KUJITUMBUA WALA KUTUMBULIWA

  Kuna mnada wa magari ulifanyika hivi karibuni kwa ajili ya kuchukua gari la chuo aina ya Toyota Double Cabin 4WD kinyemela. Chuo kina kozi za kufundisha ufundi magari. Kikiwa na changamoto za upatikanaji wa vifaa vya kufundishia gari hilo lilichukuliwa kwa njia ya mnada bila kujali kwamba gari hilo lingeweza kutumika kwa ajili ya mafunzo kwa wanafunzi.

  Kadhalika kuna Lori aina ya Mesedes Benz limeachwa kwa makusudi ili lizidi kuharibika au lizidi kuonekana limechakaa ili na lenyewe liuzwe kwa mnada ili linufaishe Mkuu wa chuo. Lori hili ni zima ila kwa makusudi haliendeshwi ili lionekane ni bovu na hatimaye lipate kuuzwa.

 12. #12
  Senior Member GURU's Avatar
  Join Date
  Aug 2014
  Location
  Gangstarr
  Posts
  906
  Rep Power
  6
  Likes Received
  26
  Likes Given
  41

  Re: JIPU LAKATAA KUJITUMBUA WALA KUTUMBULIWA

  Hili jipu limeandikwa sana humu, inabidi mpeleke taarifa Tukukuru.

 13. #13
  Junior Member
  Join Date
  Mar 2016
  Posts
  28
  Rep Power
  0
  Likes Received
  1
  Likes Given
  0

  Re: JIPU LAKATAA KUJITUMBUA WALA KUTUMBULIWA

  Quote Originally Posted by Tembo View Post
  Pengine sababu za Mkuu Chuo kuitwa JIPU ni hizi:

  1) Matumizi ya fedha za mafunzo viwandani (IPT) kiasi cha TZS 320,000,000/= zina utata.
  Utata wa fedha za mafunzo viwandani ni kuanzia 2011/12 – 2014/2015. Kwa miaka minne mfululizo kiasi cha 80,000,000/= kila mwaka hazijulikani zilikwenda wapi au zilifanya nini.

  2) Matumizi ya fedha za mishahara ya wafanyakazi mwezi Januari 2014 kwa wafanyakazi walioajiriwa Desemba 2013. Wastani wa TZS 30,000,000/= za mishahara hazijulikani zilikwenda wapi au zilifanya nini

  3) Miradi hewa ya ujenzi ililipwa wastani wa TZS 400,000,000/=

  4)Matumizi ya malipo hewa ya miradi ya ujenzi kupitia ATC-PCB, wastani wa TZS 250,000,000/=

  5) Matumizi ya upanuzi wa jengo la Utawala, wastani wa TZS 700,000,000/=

  6) Matumizi ya ujenzi wa jengo la Umwagiliaji lililogharimu TZS 4,000,000,000/=. Wastani wa TZS 2,500,000,000/= zinakadiriwa kutosha kujenga jengo hili na hasa ikizingatiwa kwamba matofali na shughuli nyingine kama paa na madirisha zilifanywa kwa rasilimali za Chuo. Wastani wa TZS 1,500,000,000/= zinadaiwa kutumika kifisadi. Kadhalika zaidi ya matofali 20,000 yalichukuliwa na Uongozi kwa matumizi binafsi.

  7) Matumizi ya fedha za msaada shamba la Oljoro wastani wa TZS 400,000,000/=

  8) Matumizi ya fedha zinazokatwa kutoka mishahara ya wafanyakazi kwa ajili ya ukarabati wa nyumba wastani wa TZS 300,000,000/=

  Kwa wastani, zaidi ya TZS 3.5 Billioni hazijulikani ziko wapi au zilifanyia nini
  Wengine wanalala na chatu au nyoka ndani katika harakati za kufanya mambo yao yawe safi na ubaya wao usionekane. Hayo yanafanyika ili anayetaka kutumbua asiweze kufahamu kama ni jipu au ni kipele. Kadhalika anaweza kutotambua kama ni jipu, limeiva au bado ni bichi.

  Kwa kitendo cha mtumbuaji kubaki akijiuliza kama ni jipu au siyo na kama liveiva au hapana, jipu linaendelea kukua na kuwa tatizo zaidi.

 14. #14
  Junior Member
  Join Date
  Jan 2015
  Posts
  29
  Rep Power
  0
  Likes Received
  1
  Likes Given
  1

  Re: JIPU LAKATAA KUJITUMBUA WALA KUTUMBULIWA

  Quote Originally Posted by Tembo View Post
  kama inavyofahamika Mkuu wa Chuo ni Mchaga. Mkuu kwa kutumia madaraka yake alipendekeza na hivyo kuweza kumshauri vibaya Waziri (mislead) na hivyo kuteua wajumbe wa Bodi kwa kuangalia maslahi ya Mkuu wa chuo.

  Wajumbe wa Bodi ya chuo ni Abrahamu Nyanda (Family friend); Christian Nyahumwa (School mate); Suzan Mnafe (Mchaga & girlfriend); Lyne Ukio (Mchaga); Hyacintha Makileo (Mchaga); Karoli Njau (Mchaga); Benedict Lema (Mchaga & School mate); Namnyaki Mattasia (Girlfried); Thomas Katebalirwe (Mwakilishi wa Wizara/amekuwa akilainishwa kwa bahasha iliyonona); Mbitila Shija (Mwalimu/mfanyakazi wa chuo) na Pius Paul (Mwanafunzi/serikali ya wanafunzi)

  Sasa hivi inasemekana Abrahamu Nyanda amemaliza muda wake na hivyo, Mkuu wa Chuo alimteua Christian Nyahumwa (School mate) kuwa Kaimu Mwenyekiti wa Bodi na kwa maana hiyo Bodi kuendelea na majukumu yake kama kawaida. Ikumbukwe kwamba, nafasi ya Mwenyekti wa Bodi ya chuo huteuliwa na Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Kutokana na miongozo ya NACTE, Mkuu wa chuo alitakiwa kulipwa mshahara kwa ngazi ya PHTS 12 katika mwaka 2011 mpaka 2014. Lakini kwa kutumia madaraka hayohayo, Mkuu alkulipwa kama ifuatavyo:

  Mwaka 2011/12 alitakiwa kulipwa Tsh 3,330,700/=, lakini alilipwa kiasi cha Tsh 4,303,400/= kwa mwezi

  Mwaka 2012/13 alitakiwa kulipwa Tsh 3,697,000/=, lakini alilipwa kiasi cha Tsh 4,734,000/= kwa mwezi

  Mwaka 2013/14 alitakiwa kulipwa Tsh 3,837,000/=, lakini alilipwa kiasi cha Tsh 4,823,000/= kwa mwezi

  Tanzania bila ufisadi inawezekana. Tushirikiane kutokomeza ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka nchini ili kama Taifa tuweze kupata maendeleo. Tumsaidie Rais kupiga vita ufisadi Tanzania.
  Nimeipenda hiyo Bodi ile mbaya, maana yenyewe ni kichekesho tosha.

 15. #15
  Member
  Join Date
  Feb 2015
  Posts
  56
  Rep Power
  6
  Likes Received
  0
  Likes Given
  0

  Re: JIPU LAKATAA KUJITUMBUA WALA KUTUMBULIWA

  Hatimaye hii bodi ya Ukabila, ya Familia na marafiki itakaa tena wiki ijayo kuanzia tarehe 16, 17 na 18 Juni 2016. Hamna la maana ni kugawana hela za walipa kodi tu. Haileweki nani anaitisha bodi hii kwani haina Mwenyekiti. Safi sana, serikali kama vile haipo.

 16. #16
  Member
  Join Date
  Dec 2014
  Posts
  78
  Rep Power
  6
  Likes Received
  3
  Likes Given
  1

  Re: JIPU LAKATAA KUJITUMBUA WALA KUTUMBULIWA

  Inafahamika kwa wafanyakazi kwamba Bodi ya Uongozi ya Chuo imemaliza muda wake kwa kuwa haina Mwenyekiti wa Bodi. Lakini kwa upande mwingine Bodi hii imekuwa ikiendelea na vikao vyake kama kawaida. Haifahamiki uhalali wa Bodi kuendelea kufanya vikao vya Bodi wakati Bodi haina mwenyekiti umepatikana wapi.

  Mkuu wa chuo kama Katibu wa Bodi aliitisha kikao cha Bodi ya Uongozi ya chuo tarehe 17 na 18 Machi 2016. Pamoja na mambo mengine Bodi ilijadili na kuandaa majibu ya tuhuma mbalimbali zinazohusu chuo ikiwepo ufisadi katika ujenzi wa jengo la Umwagiliaji la chuo.

  Kikao cha 33 cha Bodi kilikaa tarehe 18 Machi 2016 chini ya uenyekiti wa Profesa Christian Nyahumwa. Haifahamiki ni lini Mheshimiwa Rais alimteua Profesa Nyahumwa kuwa Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Chuo cha Ufundi Arusha. Katika kikao hiki Bodi imetetea ufisadi mwingi wa chuo. Bodi ilikubali kutetea kibanda cha mlinzi ambacho hakijawahi kuwa katika mpango wa chuo na kugharimu Tsh 42,223,173.00. Ujenzi wa kibanda hiki ulifichwa kwenye mabadiliko ya gharama (variation) za jengo la Umwagiliaji la chuo.

  Mabadiliko ya gharama za ujenzi wa jengo la Umwagiliaji la chuo, ambayo Bodi ya chuo imejipanga kutetea kwa nguvu zote ni kiasi cha Tsh 1.4 Bilioni. Baadhi ya kazi zinazodaiwa kuleta mabadiliko (variations) na kuongeza gharama za jengo hili ni kama ifuatavyo:

  Nondo za ujenzi wa jengo hilo zina mabadiliko (variation) ya kiasi cha Tsh 81,655,200.00; Ukuta wa kuzuia udongo wa jengo hilo una mabadiliko (variation) ya kiasi cha Tsh. 62,318,000.00; Tangi la kuhifadhia maji chini ya jengo hilo lina mabadiliko (variation) ya kiasi cha Tsh 48,936,000.00. Crane ya jengo hilo ina mabadiliko (variation) ya kiasi cha Tsh 40,000,000.00.

  Ukuta wa geti la jengo hilo una mabadiliko (variation) ya kiasi cha Tsh 22,804,000.00; Madirisha ya jengo hilo yana mabadiliko (variation) ya kiasi cha Tsh 53,818,040.00; Milango ya jengo hilo ina mabadiliko (variation) ya kiasi cha Tsh 86,627,500.00; Rampu ya jengo hilo ina mabadiliko (variation) ya kiasi cha Tsh 21,501,000.00; Paa la jengo hilo lina mabadiliko (variation) ya kiasi cha Tsh 33,065,000.00; Ufundi wa bomba wa jengo hilo una mabadiliko (variation) ya kiasi cha Tsh 38,560,000.00 na Lifti ya jengo hilo ina mabadiliko (variation) ya kiasi cha Tsh 120,000,000.00.

  Gharama za mkataba wa ujenzi wa jengo hili ni Tsh 2.68 Bilioni lakini kutokana na ufisadi, kama unavyoonekana hapo juu, jengo hili limeshagharimu Tsh 4.0 Bilioni. Mabadiliko ya gharama yamefikia 52% ambayo ni zaidi ya mara mbili ya kiwango kinachokubalika kisheria (Sheria ya manunuzi). Sheria inatambua gharama ya mabadiliko isiyozidi 20% ya gharama ya mkataba. Lakini ili mabadiliko hayo yakubalike ni lazima kuwe na sababu za msingi na za kweli. Pamoja na ufisadi huo hapo juu, pia zaidi ya matofali 20,000 yalichukuliwa na uongozi wa chuo kutoka chuoni kwa ajili ya shughuli binafsi.

  Ifahamike kwamba hizi ni mali/fedha za umma, na hivyo kama zingeweza kuokolewa kutokana na matumizi yasiyoeleweka, yaliyofanywa kwa NIA OVU, zingeweza kufanya mambo mengine yenye manufaa zaidi kwa TAIFA.

  Katika harakati za kuficha ufisadi huu, Mkuu wa chuo aliamua kuita kikao cha Bodi ilikusaidia kuandaa majibu ya tuhuma zinazohusu chuo. Mkuu wa chuo aliita Bodi hiyo imsaidie baada ya kuwa na taarifa kwamba Mheshimiwa Waziri Mkuu atafika Arusha wakati wowote. Haifahamiki Mkuu wa chuo alipata wapi taarifa hizo, lakini Mkuu wa chuo aliitisha kikao cha wafanyakazi wote wa chuo tarehe 10 Machi 2016 na kusema kwa wafanyakazi kuwa Waziri Mkuu angekuwa na ziara ya kikazi Mkoa wa Arusha kuanzia tarehe 14 Machi 2016.

  Katika kuendesha utawala Bora serikalini, kumekuwepo na sheria mbalimbali ili kuweza kuendesha shughuli za Serikali vizuri na kwa uwazi. Moja ya sheria hizo ni Sheria ya Majadiliano ya Pamoja katika Utumishi wa umma 2003. Sheria hii ilitoa nafasi ya kuunda mabaraza ya wafanyakazi katika sehemu za kazi. Shiria husika imetengeneza kanuni na hivyo kazi za Mabaraza ya wafanyakazi zinafahamika kisheria.

  Kadhalika sheria zilizoanzisha taasisi na mashirika mbalimbali ya umma zimeweka Bodi za uendeshaji wa taasisi au mashirika hayo. Sheria hizo pia zimeweka uwezo na kazi za Bodi hizo. Inashangaza kwamba katika Chuo cha Ufundi Arusha chombo kimoja kilichoanzishwa kwa sheria (BODI) huona kipo juu ya kingine kilichoanzishwa kwa sheria pia (BARAZA).

  Uongozi wa Chuo cha Ufundi aRUSHA ulikwepa kuunda Baraza la wafanyakazi kwa muda mrefu. Mheshimiwa Waziri Mkuu aliyestaafu (Mh Pinda) alitoa kauli kali kuwa anataka majina ya Taasisi za umma ambazo hazikuwa na Baraza la wafanyakazi. Baada ya kauli hiyo, Mkuu wa chuo haraka aliwezesha chuo kuwa na Baraza la wafanyakazi. Lakini hata baada ya kuwepo Baraza la Wafanyakazi chuoni, Mkuui wa Chuo kwa sababu anazozijua mwenyewe, huwa hajadili jambo lolote na Baraza la wafanyakazi la Chuo, haifahamiki kwanini inakuwa hivyo na BARAZA liliundwa kwa kusudi gani.

  Baraza la wafanyakazi la chuo liliundwa rasmi Februari 2014. Cha ajabu baraza hili limebaki kuwa jina tu, kwa kuwa tangu lianzishwe Baraza hili limewahi kukutana na kufanya vikao mara mbili tu. Mara ya mwisho Baraza la wafanyakazi la Chuo lilikaa kikao chake Septemba 2014. Uongozi wa Chuo unafanya kazi na Bodi ya uongozi ya chuo hata kwa mambo ambayo kisheria yalitakiwa kwanza yajadiliwe na Baraza la wafanyakazi kabla ya kupelekwa BODI kwa ajili ya kupata Baraka za BODI.

  Uongozi wa chuo umekuwa ukikwepa kufanya kazi (kujadiliana) na Baraza la Wafanyakazi kwa kuwa BARAZA la Wafanyakazi linafahamu ufisadi anaofanywa na Uongozi wa Chuo, hivyo Uongozi wa chuo hukwepa maswali kutoka kwa wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi kama ungefanya vikao vya Baraza la Wafanyakazi wa Chuo.

  Mkuu wa chuo hutengeneza mazingira ya wajumbe wa Bodi yake kujipatia fedha kwa kuitisha vikao vya mara kwa mara.

  Kutokana na ufisadi huu na ubadhirifu mwingi unaofanywa na Uongozi wa Chuo kwa kushirikiana na BODI ya Chuo, ni dhahiri kwamba nia ya kuifanya Tanzania kuwa Taifa la uchumi wa kati inaweza kuwa jambo lisilowezekana endapo serikali haitachukua hatua za makusudi kuondokana na watendaji wa aina hii sehemu mbalimbali serikalini.
  Last edited by Tembo; 02-07-2016 at 14:34.

 17. #17
  Senior Member
  Join Date
  Sep 2014
  Posts
  468
  Rep Power
  6
  Likes Received
  28
  Likes Given
  17

  Re: JIPU LAKATAA KUJITUMBUA WALA KUTUMBULIWA

  Click image for larger version. 

Name:	IMG_0083.jpg 
Views:	92 
Size:	40.9 KB 
ID:	1499

  Click image for larger version. 

Name:	IMG_0086.jpg 
Views:	82 
Size:	37.9 KB 
ID:	1500

 18. #18
  Member
  Join Date
  Jan 2015
  Posts
  44
  Rep Power
  0
  Likes Received
  0
  Likes Given
  1

  Re: JIPU LAKATAA KUJITUMBUA WALA KUTUMBULIWA

  UWEPO WA TAARIFA ZA UPOTOSHAJI KUHUSU CHUO CHA UFUNDI ARUSHA

  Quote Originally Posted by Tembo View Post
  Inafahamika kwa wafanyakazi kwamba Bodi ya Uongozi ya Chuo imemaliza muda wake kwa kuwa haina Mwenyekiti wa Bodi. Lakini kwa upande mwingine Bodi hii imekuwa ikiendelea na vikao vyake kama kawaida. Haifahamiki uhalali wa Bodi kuendelea kufanya vikao vya Bodi wakati Bodi haina mwenyekiti umepatikana wapi.

  Mkuu wa chuo kama Katibu wa Bodi aliitisha kikao cha Bodi ya Uongozi ya chuo tarehe 17 na 18 Machi 2016. Pamoja na mambo mengine Bodi ilijadili na kuandaa majibu ya tuhuma mbalimbali zinazohusu chuo ikiwepo ufisadi katika ujenzi wa jengo la Umwagiliaji la chuo.

  Kikao cha 33 cha Bodi kilikaa tarehe 18 Machi 2016 chini ya uenyekiti wa Profesa Christian Nyahumwa. Haifahamiki ni lini Mheshimiwa Rais alimteua Profesa Nyahumwa kuwa Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Chuo cha Ufundi Arusha. Katika kikao hiki Bodi imetetea ufisadi mwingi wa chuo. Bodi ilikubali kutetea kibanda cha mlinzi ambacho hakijawahi kuwa katika mpango wa chuo na kugharimu Tsh 42,223,173.00. Ujenzi wa kibanda hiki ulifichwa kwenye mabadiliko ya gharama (variation) za jengo la Umwagiliaji la chuo.

  Mabadiliko ya gharama za ujenzi wa jengo la Umwagiliaji la chuo, ambayo Bodi ya chuo imejipanga kutetea kwa nguvu zote ni kiasi cha Tsh 1.4 Bilioni. Baadhi ya kazi zinazodaiwa kuleta mabadiliko (variations) na kuongeza gharama za jengo hili ni kama ifuatavyo:

  Nondo za ujenzi wa jengo hilo zina mabadiliko (variation) ya kiasi cha Tsh 81,655,200.00; Ukuta wa kuzuia udongo wa jengo hilo una mabadiliko (variation) ya kiasi cha Tsh. 62,318,000.00; Tangi la kuhifadhia maji chini ya jengo hilo lina mabadiliko (variation) ya kiasi cha Tsh 48,936,000.00. Crane ya jengo hilo ina mabadiliko (variation) ya kiasi cha Tsh 40,000,000.00.

  Ukuta wa geti la jengo hilo una mabadiliko (variation) ya kiasi cha Tsh 22,804,000.00; Madirisha ya jengo hilo yana mabadiliko (variation) ya kiasi cha Tsh 53,818,040.00; Milango ya jengo hilo ina mabadiliko (variation) ya kiasi cha Tsh 86,627,500.00; Rampu ya jengo hilo ina mabadiliko (variation) ya kiasi cha Tsh 21,501,000.00; Paa la jengo hilo lina mabadiliko (variation) ya kiasi cha Tsh 33,065,000.00; Ufundi wa bomba wa jengo hilo una mabadiliko (variation) ya kiasi cha Tsh 38,560,000.00 na Lifti ya jengo hilo ina mabadiliko (variation) ya kiasi cha Tsh 120,000,000.00.

  Gharama za mkataba wa ujenzi wa jengo hili ni Tsh 2.68 Bilioni lakini kutokana na ufisadi, kama unavyoonekana hapo juu, jengo hili limeshagharimu Tsh 4.0 Bilioni. Mabadiliko ya gharama yamefikia 52% ambayo ni zaidi ya mara mbili ya kiwango kinachokubalika kisheria (Sheria ya manunuzi). Sheria inatambua gharama ya mabadiliko isiyozidi 20% ya gharama ya mkataba. Lakini ili mabadiliko hayo yakubalike ni lazima kuwe na sababu za msingi na za kweli. Pamoja na ufisadi huo hapo juu, pia zaidi ya matofali 20,000 yalichukuliwa na uongozi wa chuo kutoka chuoni kwa ajili ya shughuli binafsi.

  Ifahamike kwamba hizi ni mali/fedha za umma, na hivyo kama zingeweza kuokolewa kutokana na matumizi yasiyoeleweka, yaliyofanywa kwa NIA OVU, zingeweza kufanya mambo mengine yenye manufaa zaidi kwa TAIFA.

  Katika harakati za kuficha ufisadi huu, Mkuu wa chuo aliamua kuita kikao cha Bodi ilikusaidia kuandaa majibu ya tuhuma zinazohusu chuo. Mkuu wa chuo aliita Bodi hiyo imsaidie baada ya kuwa na taarifa kwamba Mheshimiwa Waziri Mkuu atafika Arusha wakati wowote. Haifahamiki Mkuu wa chuo alipata wapi taarifa hizo, lakini Mkuu wa chuo aliitisha kikao cha wafanyakazi wote wa chuo tarehe 10 Machi 2016 na kusema kwa wafanyakazi kuwa Waziri Mkuu angekuwa na ziara ya kikazi Mkoa wa Arusha kuanzia tarehe 14 Machi 2016.

  Katika kuendesha utawala Bora serikalini, kumekuwepo na sheria mbalimbali ili kuweza kuendesha shughuli za Serikali vizuri na kwa uwazi. Moja ya sheria hizo ni Sheria ya Majadiliano ya Pamoja katika Utumishi wa umma 2003. Sheria hii ilitoa nafasi ya kuunda mabaraza ya wafanyakazi katika sehemu za kazi. Shiria husika imetengeneza kanuni na hivyo kazi za Mabaraza ya wafanyakazi zinafahamika kisheria.

  Kadhalika sheria zilizoanzisha taasisi na mashirika mbalimbali ya umma zimeweka Bodi za uendeshaji wa taasisi au mashirika hayo. Sheria hizo pia zimeweka uwezo na kazi za Bodi hizo. Inashangaza kwamba katika Chuo cha Ufundi Arusha chombo kimoja kilichoanzishwa kwa sheria (BODI) huona kipo juu ya kingine kilichoanzishwa kwa sheria pia (BARAZA).

  Uongozi wa Chuo cha Ufundi aRUSHA ulikwepa kuunda Baraza la wafanyakazi kwa muda mrefu. Mheshimiwa Waziri Mkuu aliyestaafu (Mh Pinda) alitoa kauli kali kuwa anataka majina ya Taasisi za umma ambazo hazikuwa na Baraza la wafanyakazi. Baada ya kauli hiyo, Mkuu wa chuo haraka aliwezesha chuo kuwa na Baraza la wafanyakazi. Lakini hata baada ya kuwepo Baraza la Wafanyakazi chuoni, Mkuui wa Chuo kwa sababu anazozijua mwenyewe, huwa hajadili jambo lolote na Baraza la wafanyakazi la Chuo, haifahamiki kwanini inakuwa hivyo na BARAZA liliundwa kwa kusudi gani.

  Baraza la wafanyakazi la chuo liliundwa rasmi Februari 2014. Cha ajabu baraza hili limebaki kuwa jina tu, kwa kuwa tangu lianzishwe Baraza hili limewahi kukutana na kufanya vikao mara mbili tu. Mara ya mwisho Baraza la wafanyakazi la Chuo lilikaa kikao chake Septemba 2014. Uongozi wa Chuo unafanya kazi na Bodi ya uongozi ya chuo hata kwa mambo ambayo kisheria yalitakiwa kwanza yajadiliwe na Baraza la wafanyakazi kabla ya kupelekwa BODI kwa ajili ya kupata Baraka za BODI.

  Uongozi wa chuo umekuwa ukikwepa kufanya kazi (kujadiliana) na Baraza la Wafanyakazi kwa kuwa BARAZA la Wafanyakazi linafahamu ufisadi anaofanywa na Uongozi wa Chuo, hivyo Uongozi wa chuo hukwepa maswali kutoka kwa wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi kama ungefanya vikao vya Baraza la Wafanyakazi wa Chuo.

  Kama kawaida ya Mkuu wa chuo kutengeneza mazingira ya wajumbe wake wa Bodi kujipatia fedha Kikio cha 34 cha Bodi kitakaa tarehe 16 na 17 mwezi Machi 2016.

  Kutokana na ufisadi huu na ubadhirifu mwingi unaofanywa na Uongozi wa Chuo kwa kushirikiana na BODI ya Chuo, ni dhahiri kwamba nia ya kuifanya Tanzania kuwa Taifa la uchumi wa kati inaweza kuwa jambo lisilowezekana endapo serikali haitachukua hatua za makusudi kuondokana na watendaji wa aina hii.

 19. #19
  Member
  Join Date
  Feb 2015
  Posts
  50
  Rep Power
  6
  Likes Received
  0
  Likes Given
  0

  Re: JIPU LAKATAA KUJITUMBUA WALA KUTUMBULIWA

  Quote Originally Posted by Juma Joseph View Post
  Click image for larger version. 

Name:	Masika.jpg 
Views:	211 
Size:	12.7 KB 
ID:	1452 Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha, Dkt Richard Masika Mushi
  Hivi ndivyo inavyoweza kusemwa maana habari za ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka yanayofanywa na Menejimenti ya Chuo cha Ufundi Arusha (ATC) zimeripotiwa Serikalini mara kwa mara.

  Ni dhahiri kwamba licha ya kashifa nyingi za ufisadi uliofanywa na kuendelea kufanywa na Menejimenti ya Chuo cha Ufundi Arusha hakuna hatua zozote zilizochukuliwa au zinazopangwa kuchukuliwa ili kutatua kero hiyo. Hii ni kero kubwa kwani licha ya kuliingizia Taifa hasara, Ustawi wa chuo unazidi kudorora siku hadi siku.

  Menejimenti inayolaumiwa na kulalamikiwa kwa kujichotea fedha za umma bila kujali imekataa kuwajibika walao kupisha uchunguzi. Pia mamlaka za juu zimeshindwa kuchukua hatua zozote baada ya tetesi kusambaa kwamba majipu hayo yamejiimarisha sana na mfumo wa Serikali ya JPM.

  Moja ya walalamikiwa hao alisikika akijitapa kwamba “ukiwa mtu wa mfumo hupati shida hata siku moja. Tumepiga mahela ya nguvu hapa lakini TAKUKURU wanatuamkia Shikamoo, hao bwana wadogo watapiga kelele tu”. Mkuu wa Chuo pale, ukienda ofisini kwake ana picha alizopiga na mheshimiwa Rais, unafanya mchezo, alisikika akijigamba mlalamikiwa huyo.

  Mlalamikiwa huyo aliendelea kusema kwamba “ukiona watu wakitangaza kwenye vyombo vya habari wametumbua majipu elewa wana chuki binafsi bradha, hakuna cha majipu wala nini” Unategemea mtu mwenye mtandao mpana kama Masika atumbuliwe? Aliuliza BOSI huyo anayependa sana kuitwa bosi.

  Huenda maneno ya BOSI huyu yana ukweli. Ikiwa ni kweli, basi Serikali ya Mh Rais itakuwa na safari ndefu kupiga vita na kuondokana na UFISADI
  Mangi huenda wale wanawake uliowaoa ukazaa nao, na kuwatema na kutelekeza watoto, ulipopata hela labda ndio mizimu yao inakutesa. Nenda Moshi ukatambike babaangu.

 20. #20
  Member
  Join Date
  Dec 2014
  Posts
  78
  Rep Power
  6
  Likes Received
  3
  Likes Given
  1

  Re: JIPU LAKATAA KUJITUMBUA WALA KUTUMBULIWA

  Quote Originally Posted by utemi View Post
  UWEPO WA TAARIFA ZA UPOTOSHAJI KUHUSU CHUO CHA UFUNDI ARUSHA

  Tarehe 10-03-2016 tulikuwa na kikao cha wafanyakazi wote wa chuo, ni katika kikao hicho tuliaminishwa kuwa Mhe Waziri Mkuu angetembelea Arusha na huenda angeweza pia kufika Chuoni. Kadhalika tarehe 15-06-2016 tulikuwa na kikao kingine cha wafanyakazi wote wa chuo. Katika kikao hicho pamoja na mambo mengine tuliambiwa kwamba Mhe Waziri wetu wa Elimu angefika chuoni tarehe 18-06-2016.

  Katika vikao hivi vya wafanyakazi jambo kubwa linalosisitiziwa ni kila mfanyakazi ahakikishe amesaini karatasi ya mahudhurio. Cha ajabu vikao hivi vya Mkuu wa chuo na wafanyakazi havina minutes za kikao, hazina yatokanayo na kikao kilichotangulia wala hakina utekelezaji wa maazimio ya vikao vilivyopita kwa kuwa vikao hivi ni sawa tu na kikao cha kutoa taarifa kwa wafanyakazi.

  Ukiangalia ni kama haina maana sana kuitisha kikao cha wafanyakazi kwa ajili ya kuwapa taarifa ambayo ingeweza kuwekwa kama Tangazo na wafanyakazi wote wakapata Taarifa hiyo

  Inaonekana Menejimenti ya chuo hupenda kutumia njia hii ili kupata majina ya mahudhurio ili kuyatumia kuridhisha wageni kwamba uongozi wa chuo hufanya vikao vya mara kwa mara na wafanyakazi. Huenda minutes na yatokanayo na vikao vilivyotangulia yanaandaliwa na vyote viko kwenye mafaili kwa ajili ya kuonesha wageni kwamba mambo yanafanywa vizuri. Nakumbuka mfanyakazi mmoja mgeni aliwahi kuuliza katika kikao fulani kuwa mbona hakuna minutes za kikao kilichopita, nafikiri alichokipata anajua yeye ni Mungu wake.

  Hao wanaoombwa kufika Ofisi ya Menejimenti ili kupewa ufafanuzi wa malalamiko ya wafanyakazi ni katika kutaka kuwaonesha taarifa za kupika na pia kupata fursa ya kuweza kulainisha wahusuka kwa kadri itakavyowezekana. Inashangaza sana kwamba fedha kwa ajili ya kulainisha na kukirimu baadhi ya watu nje ya chuo huwa zipo nyingi lakini stahili mbalimbali za wafanyakazi ni matatizo.

  Wapo wafanyakazi wamepata matatizo ya misiba, wengine wanasaidiwa na chuo kwa kupewa fedha kwa kificho na wengine wanaachwa, kuwa watajua wenyewe. Imefika mahali hakuna mfanyakazi anayeamini chochote kinachosemwa na Menejimenti ya Chuo. Kiwe cha kweli au uwongo wafaanyakazi wanadhani ni uwongo tu, hiyo si taswira nzuri kwa kiongozi. Tumezoea, haya ndio maisha yetu ya kila siku, Mungu akipenda pengine ipo siku mambo haya yatabadilika.
  Last edited by Tembo; 02-07-2016 at 15:39.

 21. #21
  Member
  Join Date
  Jan 2015
  Posts
  44
  Rep Power
  0
  Likes Received
  0
  Likes Given
  1

  Re: JIPU LAKATAA KUJITUMBUA WALA KUTUMBULIWA  - - - Updated - - -

  Click image for larger version. 

Name:	7640_10153996847952487_1296214619587581403_n.jpg 
Views:	114 
Size:	28.1 KB 
ID:	1507

  Tembo a.k.a Victor Meena bado upo bize kupotosha umma. Tangu ufukuzwe kazi upo bize kwenye mitandao ukichafua Chuo na Serikali. Hongera sana lakini kumbuka kuna sheria ya makosa ya mtandao mzee. endelea na propanda zako tu. Time will tell

 22. #22
  Junior Member
  Join Date
  Mar 2016
  Posts
  26
  Rep Power
  0
  Likes Received
  0
  Likes Given
  0

  Re: JIPU LAKATAA KUJITUMBUA WALA KUTUMBULIWA

  Ufisadi ni kitu hatari sana kwa kuwa ni wizi ambao mara nyingi unafanywa kwa mtandao wa watu kadhaa. Utemi ni mtemi na anafanya utemi kwelikweli. Ukiangalia kwa makini utagundua kwamba huyu utemi ni chuo na ukiangalia kwa upande mwingine utemi ni menejimenti ya chuo.

  Ukichunguza utagundua kwamba mtandao huu haramu wa kifisadi uko tayari kufanya chochote kwa yeyote anayefikiriwa kuwa kikwazo kwa kundi la utemi kufanya ufisadi wanaotaka.

 23. #23
  Junior Member
  Join Date
  Mar 2016
  Posts
  28
  Rep Power
  0
  Likes Received
  1
  Likes Given
  0

  Re: JIPU LAKATAA KUJITUMBUA WALA KUTUMBULIWA

  Kila jambo lina principles zake: Panapokoseka haki hakuwezi kuwa na amani. Kila panapokosekana haki hakuwezi kuwa na matumaini. Kila panapokosekana haki panapoteza utulivu. Na pale panapokosekana amani utengano huongezeka na upendo hupungua. Katika mazingira ya aina hii, kazi itafanyika kwa namna gani?

 24. #24
  Member
  Join Date
  Jan 2015
  Posts
  44
  Rep Power
  0
  Likes Received
  0
  Likes Given
  1

  Re: JIPU LAKATAA KUJITUMBUA WALA KUTUMBULIWA

  Quote Originally Posted by Juma Joseph View Post
  Ufisadi ni kitu hatari sana kwa kuwa ni wizi ambao mara nyingi unafanywa kwa mtandao wa watu kadhaa. Utemi ni mtemi na anafanya utemi kwelikweli. Ukiangalia kwa makini utagundua kwamba huyu utemi ni chuo na ukiangalia kwa upande mwingine utemi ni menejimenti ya chuo.

  Ukichunguza utagundua kwamba mtandao huu haramu wa kifisadi uko tayari kufanya chochote kwa yeyote anayefikiriwa kuwa kikwazo kwa kundi la utemi kufanya ufisadi wanaotaka.
  ukiangalia kwa karibu na kusoma kwa makini. utagundua kuwa Tembo, TUA, Juma Joseph, Tunde, Mbuga, Muha na wengine ni genge ambao lipo bize kwenye mitandao kwa lengo la kupotosha umma, kuichaifua Serikali na Chuo cha Ufundi hapo Arusha. Ni genge hilo hilo ambao ipo bize kuchangia fedha kwa ajili ya kuonga waandishi wa habari kwa lengo ile ile ya kuupotosha umma dhidi ya Serikali na Chuo cha Ufundi Arusha. Ni genge ambalo linamini kuwa kwa kufanya hicho nacho fanya basi nia zao ovu zitafanikiwa. Ni genge ambalo ilinamini kuwa Nchi hii haina sheria. Ni genge ambalo ni anajua kuwa hakuna sheria ya makosa ya mitandao. ni genge ambalo siku zote linaamini kuwa Serikali inaendeshwa kwa majungu na chuki tu......

 25. #25
  TUA
  TUA is offline
  Senior Member
  Join Date
  Oct 2014
  Posts
  677
  Rep Power
  6
  Likes Received
  32
  Likes Given
  0

  Re: JIPU LAKATAA KUJITUMBUA WALA KUTUMBULIWA

  Hakuna mahali popote ambapo Serikali imechafuliwa na hao anaodai utemi. Hao wanapiga vita na kuitaarifu serikali juu ya mambo machafu na wizi unaofanywa na utemi na Genge lake la wahuni. Anayepigwa vita kwa vitendo vyake viovu ni Utemi na Genge lake, ambapo wameitia hasara Serikali tunayoitetea kwa kuiba kiasi Cha Tsh 1.4 bilioni kutoka jengo la madarasa la Umwagiliaji lililojengwa hivi karibuni. Utemi na Genge lake wamefika mahali hawatoi haki kwa wafanyakazi akina dada, mpaka waombe ngono, hii ni aibu kwa Serikali wanayoitumika ndiyo maana tunaiambia iwachukulie hatua. Bado tunaiambia Serikali kuwa Utemi na Genge lake wamevuka mipaka sasa kwa sababu wamehamishia ngono mpaka kwa wanafunzi, na tunahofia wataambukiza watoto wetu ukimwi.
  Utemi na Genge lake baada ya Ujenzi wa Jengo la umwagiliaji wamechukua matofali yapatayo 20,000 na kwenda kufanyia shughuli zao binafsi, huo ndio uungwana? Mheshimiwa Rais, anasisitiza ujenzi wa madarasa, utengenezaji wa madawati, na maabara, nyie hamna aibu kuchukua mali ya umma hadharani na kwenda kufanyia shughuli binafsi? Matofali 20,000 yangetosha kujenga maabara ngapi za Sekondari?

  Utemi na Genge lake ni hivi majuzi tu, wameitia Serikali hasara, baada ya kulipa hela zaidi ya milioni 10, kwenye akaunti ya Chuo kimoja huko Malaysia, ili mwalimu wa lapidary (Binti – mrembo) akasome lakini baada ya kuwakatalia ngono alinyimwa asiende na hiyo hela kupotea. Baada ya kumfrasteti, na baada ya kukataa hiyo tabia yao chafu, walimuandama kwelikweli, mpaka binti wa watu ameacha kazi, hii pia ni hasara kwa Serikali. Haya ndiyo matendo ambayo utemi na kundi lake yakiripotiwa anasema Serikali inachafuliwa. Hivi kumbe Utemi na kundi lao ndio Serikali? Kwa hiyo matendo yao machafu yakipigwa vita ni Serikali inachafuliwa? Serikali iko vizuri, utemi na Genge lake la wahuni ndio wanaichafua. Chuo kimepewa shamba la Oljoro, ili wanafunzi wa Civil and irrigation waweze kufanta mafunzo yao ya vitendo huko, lakini mpaka leo hakuna chochote kilichofanyika kuendeleza shamba hilo. Hata pesa wanazotoa wahisani kuendeleza shamba hilo inasemekana utemi na kundi lake wamezifuja.

  Katika usaili uliofanyika mwezi wa Tano, inasemekana utemi alimtengenezea cheti feki ndugu yake aliyemleta kutoka kijijini kwao kibosho ili apate ajira. Kama siyo Sekretarieti ya ajira, kuwa ngangari kijana huyo ambaye ni darasa la saba alishapata kazi kwa cheti feki. Haya yakipigwa vita, utemi anasema eti Serikali inachafuliwa. Mnamo January, 2014 Utemi na kudi lake walichikichia mishahara ya wafanyakazi 25, na kuwafanya wasione mishahara hiyo mpaka leo, watu waliokuwa wanaanza maisha, haya ndiyo mambo ambayo utemi na kundi lake hawataki yaripotiwe.

  Kuonyesha jinsi Utemi anavyoihujumu Serikali ni pale alipojitoa ufahamu kwa kujaza majina ya ndugu zake na wa kabila moja kwenye bodi ili aweze kuhujumu vizuri. Hapa kati ya watu 11 kwenye bodi 6 ni wa kabila lake yaani kutoka uchagani. Hapa ndipo tunapomuona Utemi kuwa haitendei haki Serikali, bali ana nia ya kujinufaisha mwenyewe na watu wa kwao. Haiingii akilini kukuta, Mkuu wa Taasisi ni Mchagga, halafu asilimia 60 ya wajumbe wa bodi hiyo ni Wachagga. Lazima kuna kitu.

Page 1 of 2 12 LastLast

Posting Permissions

 • You may not post new threads
 • You may not post replies
 • You may not post attachments
 • You may not edit your posts
 •