Close

Results 1 to 4 of 4
 1. #1
  Junior Member
  Join Date
  Mar 2016
  Posts
  26
  Rep Power
  0
  Likes Received
  0
  Likes Given
  0

  MADARAKA YA RAIS YAINGILIWA KWA SABABU ZA KIFISADI

  Kama inavyofahamika, Wenyeviti wa Bodi za mashirika na Taasisi za Umma wanateuliwa na Rais. Lakini katika hali isiyo ya kawaida, Menejimenti ya Chuo cha Ufundi Arusha ilimteua Profesa Christian Nyahumwa wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam kuwa kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Uongozi wa Chuo cha Ufundi Arusha

  Kuteuliwa kwa Profesa Nyahumwa kukaimu nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Ufundi Arusha ni kutaka kuweka muendelezo wa kufisidi mali ya umma kama ilivyoripotiwa katika vyombo vya habari.

  Haya yanafanyika Baada ya aliyekuwa mwenyekiti wa Bodi hiyo Bwana Abrahamu Nyanda kumaliza muda wake kisheria. Hata hivyo Bwana Nyanda alimaliza muda wake baada ya kudumu kwenye Bodi hiyo kwa muda wa miaka tisa mfululizo.

  Wakati Profesa Nyahumwa anateuliwa na Menejimenti ya chuo kukaimu nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Uongozi wa Chuo, tayari alikuwa Mjumbe wa Bodi ya Chuo hicho kwa mihula miwili.

  Inaaminika kwamba kitendo cha Menejimenti ya Chuo kuteua Kaimu Mwenyekiti wa Bodi na Bodi chini ya uenyekiti wa Kaimu mwenyekiti kuendelea na vikao vyake kama kawaida ni kudharau Mamlaka ya Rais kama Mkuu wa Nchi na Serikali. Nia kubwa mpaka kupelekea kuingilia madaraka ya Rais ni ili tu kutaka kuendelea na biashara kama kawaida (Business as usual) ya kuliibia Taifa rasilimali chache zilizopo kwa faida ya watu wachache.

  Ufisadi wa mali ya Umma umekuwa ukipingwa na kila mwananchi mwenye mapenzi mema na hata Rais wa Nchi

  Jambo hili la Menejiment ya Chuo cha Ufundi Arusha kuingilia madaraka ya Rais ili kutaka kutimiza malengo yao binafsi, ni kuvunja sheria na kuenda kinyume cha Katiba ya Nchi. Rais amepewa Madaraka na Mamlaka aliyonayo kisheria na kikatiba.

  Kama kuna mwenye maoni tofauti ayaweke jamvini tujadili
  Last edited by Juma Joseph; 09-04-2016 at 17:34.

 2. #2
  Senior Member
  Join Date
  Aug 2015
  Posts
  2,802
  Rep Power
  7
  Likes Received
  89
  Likes Given
  66

  Re: MADARAKA YA RAIS YAINGILIWA KWA SABABU ZA KIFISADI

  Usitegemee Mabadiliko kupitia Mfumo wa CCM na Raisi wa Ccm na Serikali ya Ccm

 3. #3
  Member
  Join Date
  Dec 2014
  Posts
  78
  Rep Power
  6
  Likes Received
  3
  Likes Given
  1

  Re: MADARAKA YA RAIS YAINGILIWA KWA SABABU ZA KIFISADI

  Rais wetu mpendwa ameonesha nia ya kutaka kufanya mabadiliko makubwa serikalini. Mheshimiwa Rais Mwenyewe aliahidi mabadiliko.

  Kinachoonekana Katika hili la kudiriki kuingilia madaraka ya Rais lina nia ya nibebe na mimi nijekukubeba.
  Inasemekana kwamba Mkuu wa chuo ni School mate wa Profesa Nyahumwa aliyeteuliwa na Mkuu wa Chuo
  kukaimu nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo.

  Mwenye mamlaka ya kukaimisha nafasi ya mteule wa Rais ni Rais mwenyewe.

 4. #4
  Senior Member
  Join Date
  Jun 2015
  Posts
  722
  Rep Power
  5
  Likes Received
  23
  Likes Given
  1

  Re: MADARAKA YA RAIS YAINGILIWA KWA SABABU ZA KIFISADI

  unajua watanzania tuna pepo la kusahau na ndio maana waliamua kuwaletea Prfs wakijua mtasahau na kusema mmpe muda kweli hizi ni komedi
  punda hajasoma lakini kazi hakosi

Posting Permissions

 • You may not post new threads
 • You may not post replies
 • You may not post attachments
 • You may not edit your posts
 •