Close

Results 1 to 3 of 3
 1. #1
  Member
  Join Date
  Feb 2015
  Posts
  32
  Rep Power
  0
  Likes Received
  0
  Likes Given
  0

  CHUO CHA UFUNDI ARUSHA KUFANANISHWA NA SHAMBA LA BIBI

  TAARIFA ZINAONESHA MAMILIONI YAZIDI KUCHUKULIWA KIFISADI

  Miradi mingi ya kifisadi ilibuniwa na Menejimenti ya chuo kwa lengo la kujipatia fedha kwa njia ya kifisadi imegundulika. Baadhi ya miradi iliyotafuna mamilioni ya fedha za umma kifisadi chuoni hapo katika kipindi cha 2010 - 2015 ni kama ifuatavyo:

  a) Kilichoitwa Consultancy to undertake Architectural design of four storey Staff Residential Blocks kilitafuna kiasi cha TZS 87,408,677.00. Taarifa za uhakika chuoni hapo zinasema hakuna kilichofanyika. Hivyo fedha hizo zilipotea

  b) Kinachoitwa Consultancy to undertake Architectural design of two storey lecture theatre kilitafuna kiasi cha TZS 46,940,400.00. Hakuna kilichofanyika. Baada ya malalamiko ya wakaguzi (Audit query) Menejimenti ya Chuo imeamua kuvunja madarasa yaliyokuwepo ili kujenga kitu kinachofanana na hicho. Chuo kina eneo kubwa tu la kujenga, haifahamiki ni kwanini Menejimenti iliamua kuvunja madarasa ili kujenga madarasa. Kwa kuwa kinachofanyika sicho kilichokuwa kimepangwa, fedha hizo zilipotea.

  c) Kinachoitwa Construction of Demonstration Scheme ambacho baadaye kilibadilishwa na kuitwa shamba darasa ambalo mtu yeyote akiliona ni sawa na bustani ya kawaida, ilitafuna kiasi cha TZS 60,000,000.00

  d) Kinachoitwa Master Plan of the College and Title Deed kiliteketeza TZS 59,000,000.00 huku kukiwa na michoro yote ya master plan ya Chuo iliyoandaliwa na Wajerumani

  e) Kinachoitwa Repair and modernization of workshop machines and equipments kiliteketeza kiasi cha TZS 182,000,000.00. Taarifa za uhakika chuoni hapo zinaonesha, hakuna kitu cha thamani hiyo kilichofanywa kwenye karakana za Chuo.

  Ikiangaliwa, katika utaratibu huu wa kutengeneza kazi hewa, zaidi ya TZS 435,349,000.00 ziliteketea na kupotea kama mali isiyokuwa na mwenyewe katika kipindi cha 2010-2015.

  Fedha hii zaidi ya TZS 435,349,000.00 iliyoteketea ni nje ya fedha za umma kiasi cha TZS 1.4 bilioni zinazodaiwa kuchukuliwa kifisadi kupitia kilichoitwa variation katika jengo la Umwagiliaji zilizoripotiwa katika vyombo vya habari hivi karibuni. Pia, fedha hii zaidi ya TZS 435,349,000.00 ni nje ya malipo hewa yaliyowahi kuripotiwa katika vyombo vya habari yanayokadiriwa kufikia 214,000,000.00. Malipo hayo pia yalifanyika katika kipindi hichohicho cha 2010-2015.

  Je, ni kweli kwamba Chuo hiki hakina mwenyewe hivyo mali zake zichukuliwe kama za bibi, kwa kuwa kachoka na kushindwa kufuatilia mali zake kwa sababu ya uzee?
  Last edited by KAYUMBA; 07-04-2016 at 08:37.

 2. #2
  TUA
  TUA is offline
  Senior Member
  Join Date
  Oct 2014
  Posts
  677
  Rep Power
  6
  Likes Received
  32
  Likes Given
  0

  Re: CHUO CHA UFUNDI ARUSHA KUFANANISHWA NA SHAMBA LA BIBI

  Tuna imani serikali ya Mheshimiwa Rais Magufuli itafanyia kazi mambo yote yanayozungumzwa katika chuo cha Ufundi Arusha. Lakini pia hii ikiwa ni Taasisi ya Serikali ijulikane tu kuwa kama kuna matatizo ni vyema yakashughulikiwa mapema kwani kama kweli uongozi wa Chuo hiki umehusika na ufisadi mkubwa uliofanyika Chuo hiki, basi ni aibu kwa Serikali. Hawa ni aina ya watendaji ambao Mheshimiwa Rais alisema Serikali yake haitawavumilia. Ukiachilia mengine, suala la ufisadi katika jengo la madarasa lijulikanalo kama Jengo la umwagiliaji, ni jambo ambalo halivumiliki. Halafu mimi nafikiri hapa hapaitaji kujiuliza, issue ni kuangalia kama Variations zimevuka kiwango cha sheria ya manunuzi ya Umma ya mwaka 2011, basi watu wapumzishwe kama wengine tunavyosikia. Hapa hamna mjadala. Inakuwaje mkataba wa kujenga jengo uwe Tsh 2.68 bilioni halafu kwa ujanjaujanja tu variations zifanye gharama ya jengo iwe Tsh 4.0 bilioni? Watanzania wanahitaji kusikia waliohusika na mambo haya wanapigwa chini kama wengine. Kwa kweli sasa tunaomba serikali iangalie kwa macho mapana uongozi wa Chuo hiki. Wametajwa kwenye malipo hewa, wakavumiliwa. Inasemekana wamekula mishahara ya watumishi, lakini wapo tu. Wanaharibu taswira nzima ya serikali ya mheshimiwa JPM.

 3. #3
  Junior Member
  Join Date
  Mar 2016
  Posts
  28
  Rep Power
  0
  Likes Received
  1
  Likes Given
  0

  Re: CHUO CHA UFUNDI ARUSHA KUFANANISHWA NA SHAMBA LA BIBI

  Quote Originally Posted by KAYUMBA View Post

  a) Kilichoitwa Consultancy to undertake Architectural design of four storey Staff Residential Blocks kilitafuna kiasi cha TZS 87,408,677.00. Taarifa za uhakika chuoni hapo zinasema hakuna kilichofanyika. Hivyo fedha hizo zilipotea

  b) Kinachoitwa Consultancy to undertake Architectural design of two storey lecture theatre kilitafuna kiasi cha TZS 46,940,400.00. Hakuna kilichofanyika. Baada ya malalamiko ya wakaguzi (Audit query) Menejimenti ya Chuo imeamua kuvunja madarasa yaliyokuwepo ili kujenga kitu kinachofanana na hicho. Chuo kina eneo kubwa tu la kujenga, haifahamiki ni kwanini Menejimenti iliamua kuvunja madarasa ili kujenga madarasa. Kwa kuwa kinachofanyika sicho kilichokuwa kimepangwa, fedha hizo zilipotea.

  c) Kinachoitwa Construction of Demonstration Scheme ambacho baadaye kilibadilishwa na kuitwa shamba darasa ambalo mtu yeyote akiliona ni sawa na bustani ya kawaida, ilitafuna kiasi cha TZS 60,000,000.00

  d) Kinachoitwa Master Plan of the College and Title Deed kiliteketeza TZS 59,000,000.00 huku kukiwa na michoro yote ya master plan ya Chuo iliyoandaliwa na Wajerumani

  e) Kinachoitwa Repair and modernization of workshop machines and equipments kiliteketeza kiasi cha TZS 182,000,000.00. Taarifa za uhakika chuoni hapo zinaonesha, hakuna kitu cha thamani hiyo kilichofanywa kwenye karakana za Chuo.

  Ikiangaliwa, katika utaratibu huu wa kutengeneza kazi hewa, zaidi ya TZS 435,349,000.00 ziliteketea na kupotea kama mali isiyokuwa na mwenyewe katika kipindi cha 2010-2015.

  Fedha hii zaidi ya TZS 435,349,000.00 iliyoteketea ni nje ya fedha za umma kiasi cha TZS 1.4 bilioni zinazodaiwa kuchukuliwa kifisadi kupitia kilichoitwa variation katika jengo la Umwagiliaji zilizoripotiwa katika vyombo vya habari hivi karibuni. Pia, fedha hii zaidi ya TZS 435,349,000.00 ni nje ya malipo hewa yaliyowahi kuripotiwa katika vyombo vya habari yanayokadiriwa kufikia 214,000,000.00. Malipo hayo pia yalifanyika katika kipindi hichohicho cha 2010-2015.

  Je, ni kweli kwamba Chuo hiki hakina mwenyewe hivyo mali zake zichukuliwe kama za bibi, kwa kuwa kachoka na kushindwa kufuatilia mali zake kwa sababu ya uzee?
  Hii nchi si masikini, tatizo ni uzembe/kufumbia macho wa kufuatilia mali ya nchi inapotelea wapi! Ni wachache sana wanaofaidi Keki ya Taifa

Posting Permissions

 • You may not post new threads
 • You may not post replies
 • You may not post attachments
 • You may not edit your posts
 •