Bondia machachari raia wa Ufilipino, Manny Pacquiao amepigwa marufuku kuingia katika duka kubwa maarufu la manunuzi (shopping mall) *la ‘The Grove’ lililoko Los Angeles nchini Marekani.

Marufuku hiyo imetokana na tamko lake dhidi ya watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja alilolitoa hivi karibuni akidai kuwa wanazidiwa utashi na wanyama.

PEP News imeripoti kuwa mmliki wa duka hilo kubwa, Rick Caruso ametangaza uamuzi huo akidai kuwa watu wengi wanaojihusisha na ushoga ni wateja wakubwa wa duka hilo hivyo hawatajisikia vizuri kumuona bondia huyo ndani ya duka hilo.

“Manny Pacquiao hakaribishwi tena kwenye duka hili,” alikaririwa mmiliki huyo.Hata hivyo, hii sio mara ya kwanza kwa duka hilo kubwa kumpiga marufuku Pacquiao, mwaka 2012 aliwahi kuzuiwa kutokana na kunukuu kifungu cha Biblia (Mambo ya Walawi 20: 13) kinachoeleza kuwa watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja wanapaswa kuuawa.