Bodi ya Uendeshaji au kama inavyojulikana Bodi ya Utawala ya Chuo cha Ufundi Arusha inaendelea/inafanya maandalizi ya kikao chake cha 33 leo tarehe 17-03-2016. Kwa utaratibu uliopo Kikao cha Bodi kitakaa kesho tarehe 18-03-2016
Bodi hii inaendelea na vikao vyake licha ya kutokuwa na Mwenyekiti wa Bodi. Bodi kwa sasa haina Mwenyekiti kwa kuwa muda wa mwenyekiti wa Bodi aliyekuwepo ulikwisha kisheria. Aliyekuwa mwenyekiti wa Bodi hiyo Bwana Abraham Nyanda, alimaliza muda wake baada ya kuitumikia Bodi hiyo kwa mihula mitatu au kwa muda wa miaka 9 mfululizo.
Kama ilivyo kisheria, mwenyekiti wa Bodi ya Uongozi wa Chuo huteuliwa na Rais. Inavyofahamika Mwenyekiti wa Bodi ndiye mhimili wa Bodi na hivyo kutokuwepo kunafanya Bodi isiwepo kisheria. Haifahamiki ni mamlaka gani iliyoidhinisha Bodi ya Chuo cha Ufundi Arusha ambayo haipo kisheria kukutana na kuendelea na vikao vya Bodi bila kuwa na Mwenyekiti wa Bodi. Inafahamika kwamba vipindi vya mpito, wakati Bodi ikisubiri kuundwa, mambo ya Taasisi zinazoendeshwa na Bodi, hupitishwa na wizara husika. Kwanini hapa iwe tofauti au je Vikao hivi vina kibali cha Waziri mwenye dhamana ya Elimu?
Bodi hii ya Chuo imekuwa ikilalamikiwa sana na wafanyakazi wa chuo kwa kuendelea kufumbia macho au kuwa sehemu ya ubadhirifu na ufujaji wa pesa ya umma. Kuwepo kwa vikao vya Bodi hii huvuta hisia za wafanyakazi kwa sababu Bodi ya Uongozi wa chuo huwa inajadili mambo ambayo wafanyakazi hawana habari nayo kabisa.
Ni mazoea mazuri kwamba Bodi ingejadili mambo ya wafanyakazi yaliyotokana na Baraza la Wafanyakazi lakini kwa Chuo cha Ufundi Arusha mijadala ya Bodi ni siri mithili ya njama za kutaka kupindua nchi.
Ukiachilia mjadala wa kupitisha matokeo ya wanafunzi, kimsingi hakuna jambo lingine lolote linalopaswa kujadiliwa na Bodi bila kujadiliwa na Baraza la wafanyakazi. Huwa tunashanga na kujiuliza, Bodi ya chuo hiki huwa inajadili mambo yaliyotokea wapi?
Bodi hiyo inaundwa na wajumbe wafuatao:
Mkuu wa Chuo Richard J Mushi Masika (Katibu)
Abrahamu Nyanda (Mwenyekiti aliyemaliza muda wake)
Christian Wambura Nyahumwa (Makamu M/Kiti)
Suzan Mnafe Mosha
Lyne Ukio
Hyacintha Makileo
Karoli Njau
Benedict Lema
Namnyaki Mattasia (Haijulikani
Thomas Katebalirwe (Mwakilishi wa Wizara)
Mbitila Shija (Mwakilishi wa wafanyakazi) na
Pius Paul (Mwakilishi wa wanafunzi)
Connect With Us