Close

Results 1 to 2 of 2
 1. #1
  Moderator
  Join Date
  Apr 2015
  Posts
  1,067
  Rep Power
  6
  Likes Received
  21
  Likes Given
  0

  Kesi ya David Kafulila Yapigwa Tarehe  Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Tabora imeahirisha kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi Jimbo la Kigoma Kusini iliyofunguliwa na aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo, David Kafulila, kupitia chama cha NCCR-Mageuzi akipinga ushindi wa Mbunge Hasna Mwilima, wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

  Kesi hiyo iliahirishwa jana na Jaji wa mahakama hiyo, Ferdinand Wambali, baada ya Wakili wa kujitegemea, Profesa Abdallah Safari, anamtetea mlalamikaji kuomba mahakama hiyo impatie saa 48 ili akamilishe hati za kiapo za mashahidi wake watano na baada ya hapo mahakama ipange tarehe nyingine ya kutajwa kwa ajili ya kuanza kusikiliza.

  Jaji Wambali alikubaliana na ombi hilo na kusema hati za mashahidi zipelekwe kwa Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Tabora, Shanmillah Sanwatt, zikiwa zimefungwa kwenye bahasha Machi 18, mwaka huu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Kigoma.
  hakikisha hupitwi na habari

 2. #2
  Senior Member
  Join Date
  Jun 2015
  Posts
  722
  Rep Power
  5
  Likes Received
  23
  Likes Given
  1

  Re: Kesi ya David Kafulila Yapigwa Tarehe

  kafulila hii kesi umefungua sawa ila kumbuka hakimu ni fisi huwezi kutendewa haki jipange tunyakue ushindi 2020
  punda hajasoma lakini kazi hakosi

Posting Permissions

 • You may not post new threads
 • You may not post replies
 • You may not post attachments
 • You may not edit your posts
 •