Vibonzo vya Gado katika kipindi cha XYZ


Mchora vibonzo maarufu nchini Kenya Godfrey Mwapembwa anayejulikana kwa jina Gado,ameiambia BBC kwamba alifutwa kazi na mojawapo ya magazeti maarufu nchini humo The Daily Nation bila sababu.

Gado amesema kwamba alikuwa ametoka likizo alipogundua kwamba amepoteza kazi yake bila ya kupewa sababu za kufutwa kwake.
Mwapembwa ni mchora vibonzo maarufu nchini Kenya ambaye huwachekesha wasomaji wengi kwa uchoroji wake.
Mtandao wake unaomtaja kuwa mchoraji vibonzo hodari wa kisiasa katika eneo la mashariki na Afrika ya kati,anasema kuwa vibonzo vyake huangazia kila swala kutoka ugaidi,ukataji miti,ukimwi na ufisadi na vibonzo vyake vimekuwa vikizua mjadala mkubwa.