Mgombea wa Republican nchini, Marekani Donald Trump.

Mgombea anayeongoza katika chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump, amejiongezea ushawishi kama mgombea mkuu kufuatia ushindi wake katika majimbo ya Michigan na Mississippi.
Wadadisi wanasema kuwa ushindi huo mara mbili umezima uvumi wa mwishoni mwa wiki kuwa kampeni yake Trump ilikuwa imepoteza kasi.Wagombea wa Democratic Bernie Sanders na Hillary Clinton.

Baada ya kupata ushindi huo , Trump alisema kuwa anakiongezea umaarufu chama cha Republican. Mshindani wake mkuu Seneta Ted Cruz naye alipata ushindi katika jimbo dogo la Idaho.

Kwa upande wa chama cha Democratic inaripotiwa kuwa Bernie Sanders ameshinda mchujo katika jimbo la Michigan huku naye Hillary Clinton akiibuka mshindi katika jimbo la Mississipi.