Close

Results 1 to 10 of 10
 1. #1
  Junior Member
  Join Date
  Feb 2015
  Posts
  25
  Rep Power
  0
  Likes Received
  0
  Likes Given
  0

  BARUA YA WAZI KWA MHESHIMIWA JOHN POMBE MAGUFULI - RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO

  Mheshimiwa Rais,
  Mimi ni Raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ninakupongeza sana kwa kazi nzuri unayofanya kuhakikisha kwamba wananchi wote wa Tanzania wanafaidi matunda ya Uhuru.

  Mheshimiwa Rais,
  Ninakupongoza na ninakuombea kwa Mwenyezi Mungu ili uendelee kutimiza ahadi yako ya kutumbua majipu kwa kupambana na rushwa, ubadhirifu wa mali za umma na ufisadi nchini kama ulivyolitangazia Taifa kupitia Bunge tarehe 20-11-2015. Ni imani yangu kuwa kama ulivyoahidi katika hotuba yako, ufisadi, ubadhirifu wa mali za umma na rushwa serikalini vitageuka kuwa wimbo uchukizao badala ya wimbo ufurahishao kama ilivyokuwa imezoeleka hapo awali.

  Mheshimiwa Rais,
  Pia ninapenda kuchukua nafasi hii kumpongeza na kumwombea Waziri Mkuu, Mheshimiwa Kassim Majaliwa kwa kazi nzuri sana anayofanya. Kadhalika napongeza watendaji wote uliowateua kuunda Serikali yako katika Wizara mbalimbali ili kukusaidia kufanikisha malengo yako ya kuleta hali bora zaidi kwa wananchi wote wa Tanzania katika maisha yetu ya kila siku.

  Mheshimiwa Rais,
  Ni vigumu kuweza kutimiza ahadi yako ya kupambana na rushwa, ubadhirifu wa mali za umma na ufisadi nchini kama hutapata taarifa sahihi za ni nini kinatendeka katika maeneo mbalimbali ya nchi. Kama Raia wa kawaida tunao wajibu wa kutoa taarifa sahihi za kila jambo lisilo la kizalendo lenye nia ya kuharibu ustawi wa jamii na Taifa. Kwa mujibu wa Ibara ya 27 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ni wajibu wa kila mtu kulinda mali asilia ya Jamhuri ya Muungano, mali ya Mamlaka ya Nchi na mali yote inayomilikiwa kwa pamoja na wananchi.

  Mheshimiwa Rais,
  Chuo cha Ufundi Arusha ni mali ya Mamlaka ya Nchi. Chuo hiki kina dhamana ya kutoa mafunzo bora kwa wananchi wote wa Tanzania. Katika kutekeleza majukumu yake, chuo kimekumbwa na matatizo mbalimbali. Miongoni mwa matatizo yaliyopo ni upatikanaji wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia, upungufu wa malazi kwa wanafunzi, Ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka.

  Mheshimiwa Rais,
  Kutokana na upungufu wa malazi wanafunzi wengi wa kike wanakaa nyumba za kupanga mitaani. Matokeo yake wanafunzi wengi wamepata ujauzito na wengine wengi wameshindwa masomo yao kwa kukosa mazingira rafiki ya kujisomea. Wanafunzi wanaoathirika zaidi ni wanafunzi wanaosoma ngazi ya cheti na stashahada ambao wengi wanatokea kidato cha nne (4) na wengi wana umri wa chini ya miaka 18.

  Mheshimiwa Rais,
  Chuo kingeweza kuondokana na tatizo la upungufu wa malazi kama kungekuwa na nia hiyo. Chuo kilikuwa na matofali zaidi ya 20,000, Chuo kinapata simenti kutoka kiwanda cha Tanga simenti na wanafunzi huwa wanafanya mazoezi ya kujifunza kujenga chuoni. Ni kiasi kidogo sana cha rasilimali fedha kingeweza kutumika kuondokana na tatizo la malazi chuoni.

  Mheshimiwa Rais,
  Chuo huwa kinapata msaada wa simenti tani nane (8) kila muhula kwa ajili ya kuendesha mafunzo kutoka kiwanda cha Tanga simenti. Kadhalika chuo kilikuwa na matofali zaidi ya 20,000 yaliyopigwa chuoni na kubaki katika ujenzi wa jengo la Ujenzi na Umwagiliaji. Kutokana na mazingira yasiyoeleweka, haifahamiki inakokwenda simenti hii ya msaada na pia haikufahamika yalikokwenda matofali yale yote.

  Inavyoonekana tatizo la malazi liliachwa na kuwa kubwa ili serikali iweze kutenga mabilioni ya fedha kwa ajili ya ujenzi wa mabweni. Kutengwa kwa fedha za ujenzi wa mabweni kungeweza kupelekea kufujwa kama ilivyokuwa kwa miradi mbalimbali ya ujenzi iliyofanyika chuoni kuanzia Januari 2010. Chuo kimekua kikifuja fedha nyingi za umma kupitia kampuni ya chuo ijulikanayo kama ATC-PCB.

  Mheshimiwa Rais,
  Chuo cha ufundi Arusha kina njia mbalimbali za mapato, lakini kwa sasa chuo kinaendeshwa kwa madeni. Upande mmoja wafanyakazi wanadai chuo stahili mbalimbali na kwa upande mwingine wazabuni/wafanyabiashara nao wanadai chuo mabilioni ya fedha kwa huduma mbalimbali walizotoa kwa chuo. Sintofahamu inazidi zaidi pale ambapo haijulikani madeni haya yatalipwa lini na ni nini ilikuwa msingi wa madeni haya.

  Mheshimiwa Rais,
  Kutokana na matumizi yasiyoridhisha ya fedha za chuo, hata wanafunzi wa kozi ya Ujenzi na Umwagiliaji wameshindwa kufanya mazoezi yao inavyostahili. Wanafunzi hao wameshindwa kufanya mafunzo yao sawasawa kwa kukosekana eneo la kufanyia mazoezi (Practical practice). Wanafunzi hawa walitakiwa kuanza kufanya mazoezi hayo kwenye shamba darasa lililopo eneo la Oljoro tangu mwaka 2013.

  Wafadhili mbalimbali walitoa fedha kwa ajili ya kujenga miundombinu ya shamba hilo. Inakadiriwa kuwa kiasi cha TZS 400,000,000/= kilitolewa na wafadhili kwa ajili hiyo lakini mpaka sasa wanafunzi hawajaweza kufanya mazoezi katika shamba hilo na haijulikani ni lini wataanza kufanya mazoezi kwenye shamba hilo. Kwa sasa shamba hilo limegawanywa kwa baadhi ya wafanyakazi wa chuo kwa lengo la kujilimia.

  Mheshimiwa Rais,
  Katika mazingira yenye utata baadhi ya watumishi wa chuo walijilipa mishahara binafsi kuanzia Juni 2010 na haifahamiki ni mamlaka gani zilizowapa mishahara hiyo. Wapo wafanyakazi/watendaji wenye mishahara binafsi serikalini lakini huwa inafahamika ni mamlaka gani zimewapa watendaji hao mishahara hiyo. Kwa mtizamo huo, imefikiriwa kwamba pengine mishahara hiyo ilipatikana kwa njia ya kutumia madaraka vibaya, au kwa kujuana au kwa kuangalia sura zaidi ya sifa ya mtumishi husika. Hali hii imezua manung’uniko na huenda ari ya kazi imeshuka kwa baadhi ya watumishi na pengine utafiti ungefanyika leo ungeweza kuonesha kwamba tija chuoni imeshuka.

  Mheshimiwa Rais,
  Chuo cha Ufundi Arusha kimekuwa na bahati ya kupata vibali vingi vya ajira tangu mwaka 2010 hadi sasa. Serikali kwa nia njema imetaka kuboresha utendaji wa chuo kwa kukiongezea nguvukazi/rasilimali watu. Ni dhamira ya Serikali pia kupunguza tatizo la ajira kwa watanzania kwa kutengeneza nafasi nyingi za ajira iwezekanavyo. Pia ni matumaini ya serikali kuwa ajira zinazopatikana zitashindanishwa kwa haki kwa watanzania wote wenye sifa. Tofauti yake, kwa nyakati tofauti chuo kimetangaza nafasi za ajira lakini sehemu kubwa ya nafasi hizo huwa tayari zina wenyewe na hatimaye waliajiriwa.

  Mwezi Februari 2016 chuo kilitangaza nafasi za ajira. Katika nafasi hizo imefahamika kwamba sehemu kubwa tayari zina wenyewe. Zitakazobaki zitaendelea kujazwa kidogo-kidogo hadi mwaka 2017. Imepangwa hivyo ili baadhi ya walengwa wa viongozi wa chuo waweze kupata ajira hizi endapo hazitatokea zingine, watakapokuwa wamemaliza masomo yao kutoka vyuo mbalimbali wanavyosoma hivi sasa. Walengwa hao wanapewa ajira hizo kwa njia ya kujaza nafasi ambazo mara nyingi zinaitwa “hazikupata watu wenye sifa” na hivyo kuendelea kutangazwa tena na tena mpaka watakapofika kutoka vyuoni. Mpango huu umekuwa kama jambo la kawaida katika chuo hiki, kila nafasi za ajira huchukua zaidi ya mwaka kujazwa zingine zilienda mpaka miaka mitatu.

  Mheshimiwa Rais,
  Chuo cha Ufundi Arusha kwa sasa hakina Mwenyekiti wa Bodi ya Uendeshaji (Bodi ya Uongozi). Kwa mujibu wa sheria iliyoanzisha Chuo cha Ufundi Arusha, Mwenyekiti wa Bodi ni mteule wa Rais. Imekuwa kama ni kawaida sasa kwa Bodi ya Uendeshaji kukutana na kufanya vikao vya Bodi na kulipana posho bila kuwepo Mwenyekiti wa Bodi na bila kibali cha Waziri mwenye dhamana ya Elimu kama itabidi kufanya vikao hivyo.

  Mheshimiwa Rais,
  Mara nyingi Serikali imekuwa ikikaangwa kwa mafuta yake yenyewe. Hii ni kwasababu baadhi ya watendaji wasio waaminifu Serikalini wamekuwa wakihongwa kwa fedha hizihizi za umma zilizopatikana kifisadi na hatimaye kuachia mafisadi kuendelea kuteketeza rasilimali za nchi bila huruma.

  Mheshimiwa Rais,
  Sijaweza kukuona ana kwa ana na pia sikuweza kukufikishia barua hii kwa njia nyingine. Lakini nafahamu kwamba Serikali ina mkono mrefu, na hivyo barua hii itafika kwako. Nia ya barua yangu ni ili uweze kupata taarifa sahihi za mambo yanayofanyika ndani ya Serikali yako mheshimiwa licha ya watendaji walio chini yako kufahamu kuwa mambo ya ufisadi na ubadhirifu wa mali ya umma huyapendi. Ni maombi yangu kwako kuwa, ikikupendeza mheshimiwa agiza ili uchunguzi ufanyike kuangalia kama ni jipu, ikithibitika ni jipu na kama limeiva lipate kutumbuliwa mheshimiwa.

  Mheshimiwa Rais,
  Mimi na Watanzania wengi wenye mapenzi mema tunakuombea maisha yenye Heri na Baraka wewe na wasaidizi wako wote Serikalini.

  Wako mtiifu,

  Subira – Mtanzania Mzalendo
  Last edited by SUBIRA; 23-03-2016 at 09:24.

 2. #2
  TUA
  TUA is offline
  Senior Member
  Join Date
  Oct 2014
  Posts
  677
  Rep Power
  6
  Likes Received
  32
  Likes Given
  0

  Re: BARUA YA WAZI KWA MHESHIMIWA JOHN POMBE MAGUFULI - RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO

  BINAFSI NAUNGANA SANA NA WEWE KUMPONGEZA RAIS KWA KAZI NZURI ANAYOFANYA. PIANAMPONGEZA WAZIRI MKUU NDUGU KASSIM MAJALIWA KAZI NZURI. SISI WANANCHI TUKO NYUMA YAO KWA MAOMBEZI NA SALA MUNGU AWAJALIE AFYA NJEMA. NI WAKATI SASA WA WATANZANIA WOTE KUJIUNGA KWA PAMOJA KAMA TULIVYOFANYA ILE VITA YA KUMNG'OA IDDI AMIN ALIPOTUVAMIA. TUELEWE SASA KUWA KUNA ADUI MWINGINE ALITUVAMIA NDANI YA NCHI YETU NA KUOTA MIZIZI. ADUI HUYU NI UFISADI ULIOKITHIRI, HIVYO TUSHIRIKIANE WANANCHI KWA UMOJA WETU TUMUONDOE ADUI HUYU NJE YA MIPAKA YA TANZANIA.

 3. #3
  Senior Member
  Join Date
  Sep 2014
  Posts
  468
  Rep Power
  6
  Likes Received
  28
  Likes Given
  17

  Re: BARUA YA WAZI KWA MHESHIMIWA JOHN POMBE MAGUFULI - RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO

  Kupata kazi katika Chuo hicho ni vigumu kama ngamia kupenya kwenye tundu la sindano.

  Wengi walioomba nafasi za kazi hata hawakuwahi kujibiwa kama barua zao za kuomba kazi zilifika au la.
  Wanaoomba nafasi za kazi hapo kama hawana refa wanajisumbua. Inasemekana baadhi ya barua za waombaji hufichwa kwa makusudi.

  Wakati mwingine wanafanya shotilist lakini walengwa hawajulishwi ili waweze kufika kwenye intaviu.

  Yaani ni Mungu tu anajua

 4. #4
  Junior Member
  Join Date
  Mar 2016
  Posts
  26
  Rep Power
  0
  Likes Received
  0
  Likes Given
  0

  Re: BARUA YA WAZI KWA MHESHIMIWA JOHN POMBE MAGUFULI - RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO

  Tatamadiba na Nambalapala wanaweza kufahamu.
  Mwananchi akiwa na kero anayodhani kwamba mtu pekee wa kuitatua ni Rais anatakiwa kufuata
  utaratibu gani kumfikishia Rais ujumbe?

 5. #5
  Junior Member
  Join Date
  Mar 2016
  Posts
  28
  Rep Power
  0
  Likes Received
  1
  Likes Given
  0

  Re: BARUA YA WAZI KWA MHESHIMIWA JOHN POMBE MAGUFULI - RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO

  Mlengwa mmoja inasemekana alikamatwa na cheti feki kwenye usaili uliofanyika hivi karibuni. Kuna taarifa kwamba Serikali imeshaanza kutupia macho matatizo ya Chuo cha Ufundi Arusha

 6. #6
  TUA
  TUA is offline
  Senior Member
  Join Date
  Oct 2014
  Posts
  677
  Rep Power
  6
  Likes Received
  32
  Likes Given
  0

  Re: BARUA YA WAZI KWA MHESHIMIWA JOHN POMBE MAGUFULI - RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO

  Mheshimiwa Rais,
  Mimi ni Raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ninakupongeza sana kwa kazi nzuri unayofanya kuhakikisha kwamba wananchi wote wa Tanzania wanafaidi matunda ya Uhuru.

  Mheshimiwa Rais,
  Ninakupongoza na ninakuombea kwa Mwenyezi Mungu ili uendelee kutimiza ahadi yako ya kutumbua majipu kwa kupambana na rushwa, ubadhirifu wa mali za umma na ufisadi nchini kama ulivyolitangazia Taifa kupitia Bunge tarehe 20-11-2015. Ni imani yangu kuwa kama ulivyoahidi katika hotuba yako, ufisadi, ubadhirifu wa mali za umma na rushwa serikalini vitageuka kuwa wimbo uchukizao badala ya wimbo ufurahishao kama ilivyokuwa imezoeleka hapo awali.

  Mheshimiwa Rais,
  Pia ninapenda kuchukua nafasi hii kumpongeza na kumwombea Waziri Mkuu, Mheshimiwa Kassim Majaliwa kwa kazi nzuri sana anayofanya. Kadhalika napongeza watendaji wote uliowateua kuunda Serikali yako katika Wizara mbalimbali ili kukusaidia kufanikisha malengo yako ya kuleta hali bora zaidi kwa wananchi wote wa Tanzania katika maisha yetu ya kila siku.

  Mheshimiwa Rais,
  Ni vigumu kuweza kutimiza ahadi yako ya kupambana na rushwa, ubadhirifu wa mali za umma na ufisadi nchini kama hutapata taarifa sahihi za ni nini kinatendeka katika maeneo mbalimbali ya nchi. Kama Raia wa kawaida tunao wajibu wa kutoa taarifa sahihi za kila jambo lisilo la kizalendo lenye nia ya kuharibu ustawi wa jamii na Taifa. Kwa mujibu wa Ibara ya 27 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ni wajibu wa kila mtu kulinda mali asilia ya Jamhuri ya Muungano, mali ya Mamlaka ya Nchi na mali yote inayomilikiwa kwa pamoja na wananchi.

  Mheshimiwa Rais,
  Chuo cha Ufundi Arusha ni mali ya Mamlaka ya Nchi. Chuo hiki kina dhamana ya kutoa mafunzo bora kwa wananchi wote wa Tanzania. Katika kutekeleza majukumu yake, chuo kimekumbwa na matatizo mbalimbali. Miongoni mwa matatizo yaliyopo ni upatikanaji wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia, upungufu wa malazi kwa wanafunzi, Ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka.

  Mheshimiwa Rais,
  Kutokana na upungufu wa malazi wanafunzi wengi wa kike wanakaa nyumba za kupanga mitaani. Matokeo yake wanafunzi wengi wamepata ujauzito na wengine wengi wameshindwa masomo yao kwa kukosa mazingira rafiki ya kujisomea. Wanafunzi wanaoathirika zaidi ni wanafunzi wanaosoma ngazi ya cheti na stashahada ambao wengi wanatokea kidato cha nne (4) na wengi wana umri wa chini ya miaka 18.

  Mheshimiwa Rais,
  Chuo kingeweza kuondokana na tatizo la upungufu wa malazi kama kungekuwa na nia hiyo. Chuo kilikuwa na matofali zaidi ya 20,000, Chuo kinapata simenti kutoka kiwanda cha Tanga simenti na wanafunzi huwa wanafanya mazoezi ya kujifunza kujenga chuoni. Ni kiasi kidogo sana cha rasilimali fedha kingeweza kutumika kuondokana na tatizo la malazi chuoni.

  Mheshimiwa Rais,
  Chuo huwa kinapata msaada wa simenti tani nane (8) kila muhula kwa ajili ya kuendesha mafunzo kutoka kiwanda cha Tanga simenti. Kadhalika chuo kilikuwa na matofali zaidi ya 20,000 yaliyopigwa chuoni na kubaki katika ujenzi wa jengo la Ujenzi na Umwagiliaji. Kutokana na mazingira yasiyoeleweka, haifahamiki inakokwenda simenti hii ya msaada na pia haikufahamika yalikokwenda matofali yale yote. Mbaya zaidi ni pale ambapo kiasi cha Tsh 1,400,000,000/= zimeonekana kuibwa katika mradi huu wa ujenzi wa Jengo hili la madarasa ambalo lilikadiriwa kujengwa kwa Tsh 2.63 bilioni lakini mpaka sasa limeshagharimu Tsh 4.00 bilioni likiwa bado halijakamilika.

  Inavyoonekana tatizo la malazi liliachwa na kuwa kubwa ili serikali iweze kutenga mabilioni ya fedha kwa ajili ya ujenzi wa mabweni. Kutengwa kwa fedha za ujenzi wa mabweni kungeweza kupelekea kufujwa kama ilivyokuwa kwa miradi mbalimbali ya ujenzi iliyofanyika chuoni kuanzia Januari 2010. Chuo kimekua kikifuja fedha nyingi za umma kupitia kampuni ya chuo ijulikanayo kama ATC-PCB.

  Mheshimiwa Rais,
  Chuo cha ufundi Arusha kina njia mbalimbali za mapato, lakini kwa sasa chuo kinaendeshwa kwa madeni. Upande mmoja wafanyakazi wanadai chuo stahili mbalimbali na kwa upande mwingine wazabuni/wafanyabiashara nao wanadai chuo mabilioni ya fedha kwa huduma mbalimbali walizotoa kwa chuo. Sintofahamu inazidi zaidi pale ambapo haijulikani madeni haya yatalipwa lini na ni nini ilikuwa msingi wa madeni haya.

  Mheshimiwa Rais,
  Kutokana na matumizi yasiyoridhisha ya fedha za chuo, hata wanafunzi wa kozi ya Ujenzi na Umwagiliaji wameshindwa kufanya mazoezi yao inavyostahili. Wanafunzi hao wameshindwa kufanya mafunzo yao sawasawa kwa kukosekana eneo la kufanyia mazoezi (Practical practice). Wanafunzi hawa walitakiwa kuanza kufanya mazoezi hayo kwenye shamba darasa lililopo eneo la Oljoro tangu mwaka 2013.

  Wafadhili mbalimbali walitoa fedha kwa ajili ya kujenga miundombinu ya shamba hilo. Inakadiriwa kuwa kiasi cha TZS 400,000,000/= kilitolewa na wafadhili kwa ajili hiyo lakini mpaka sasa wanafunzi hawajaweza kufanya mazoezi katika shamba hilo na haijulikani ni lini wataanza kufanya mazoezi kwenye shamba hilo. Kwa sasa shamba hilo limegawanywa kwa baadhi ya wafanyakazi wa chuo kwa lengo la kujilimia.

  Mheshimiwa Rais,
  Katika mazingira yenye utata baadhi ya watumishi wa chuo walijilipa mishahara binafsi kuanzia Juni 2010 na haifahamiki ni mamlaka gani zilizowapa mishahara hiyo. Wapo wafanyakazi/watendaji wenye mishahara binafsi serikalini lakini huwa inafahamika ni mamlaka gani zimewapa watendaji hao mishahara hiyo. Kwa mtizamo huo, imefikiriwa kwamba pengine mishahara hiyo ilipatikana kwa njia ya kutumia madaraka vibaya, au kwa kujuana au kwa kuangalia sura zaidi ya sifa ya mtumishi husika. Hali hii imezua manung’uniko na huenda ari ya kazi imeshuka kwa baadhi ya watumishi na pengine utafiti ungefanyika leo ungeweza kuonesha kwamba tija chuoni imeshuka.
  Mheshimiwa Rais,
  Chuo cha Ufundi Arusha kimekuwa na bahati ya kupata vibali vingi vya ajira tangu mwaka 2010 hadi sasa. Serikali kwa nia njema imetaka kuboresha utendaji wa chuo kwa kukiongezea nguvukazi/rasilimali watu. Ni dhamira ya Serikali pia kupunguza tatizo la ajira kwa watanzania kwa kutengeneza nafasi nyingi za ajira iwezekanavyo. Pia ni matumaini ya serikali kuwa ajira zinazopatikana zitashindanishwa kwa haki kwa watanzania wote wenye sifa. Tofauti yake, kwa nyakati tofauti chuo kimetangaza nafasi za ajira lakini sehemu kubwa ya nafasi hizo huwa tayari zina wenyewe na hatimaye waliajiriwa.

  Mwezi Februari 2016 chuo kilitangaza nafasi za ajira. Katika nafasi hizo imefahamika kwamba sehemu kubwa tayari zina wenyewe. Zitakazobaki zitaendelea kujazwa kidogo-kidogo hadi mwaka 2017. Imepangwa hivyo ili baadhi ya walengwa wa viongozi wa chuo waweze kupata ajira hizi endapo hazitatokea zingine, watakapokuwa wamemaliza masomo yao kutoka vyuo mbalimbali wanavyosoma hivi sasa. Walengwa hao wanapewa ajira hizo kwa njia ya kujaza nafasi ambazo mara nyingi zinaitwa “hazikupata watu wenye sifa” na hivyo kuendelea kutangazwa tena na tena mpaka watakapofika kutoka vyuoni. Mpango huu umekuwa kama jambo la kawaida katika chuo hiki, kila nafasi za ajira huchukua zaidi ya mwaka kujazwa zingine zilienda mpaka miaka mitatu.

  Mheshimiwa Rais,
  Chuo cha Ufundi Arusha kwa sasa hakina Mwenyekiti wa Bodi ya Uendeshaji (Bodi ya Uongozi). Kwa mujibu wa sheria iliyoanzisha Chuo cha Ufundi Arusha, Mwenyekiti wa Bodi ni mteule wa Rais. Imekuwa kama ni kawaida sasa kwa Bodi ya Uendeshaji kukutana na kufanya vikao vya Bodi na kulipana posho bila kuwepo Mwenyekiti wa Bodi na bila kibali cha Waziri mwenye dhamana ya Elimu kama itabidi kufanya vikao hivyo.

  Mheshimiwa Rais,
  Mara nyingi Serikali imekuwa ikikaangwa kwa mafuta yake yenyewe. Hii ni kwasababu baadhi ya watendaji wasio waaminifu Serikalini wamekuwa wakihongwa kwa fedha hizihizi za umma zilizopatikana kifisadi na hatimaye kuachia mafisadi kuendelea kuteketeza rasilimali za nchi bila huruma.

  Mheshimiwa Rais,
  Sijaweza kukuona ana kwa ana na pia sikuweza kukufikishia barua hii kwa njia nyingine. Lakini nafahamu kwamba Serikali ina mkono mrefu, na hivyo barua hii itafika kwako. Nia ya barua yangu ni ili uweze kupata taarifa sahihi za mambo yanayofanyika ndani ya Serikali yako mheshimiwa licha ya watendaji walio chini yako kufahamu kuwa mambo ya ufisadi na ubadhirifu wa mali ya umma huyapendi. Ni maombi yangu kwako kuwa, ikikupendeza mheshimiwa agiza ili uchunguzi ufanyike kuangalia kama ni jipu, ikithibitika ni jipu na kama limeiva lipate kutumbuliwa mheshimiwa.

  Mheshimiwa Rais,
  Mimi na Watanzania wengi wenye mapenzi mema tunakuombea maisha yenye Heri na Baraka wewe na wasaidizi wako wote Serikalini.

  Wako mtiifu,

  TUA – Mtanzania Mzalendo

 7. #7
  Member
  Join Date
  Jan 2015
  Posts
  44

  TAARIFA KWA UMMA
  UWEPO WA TAARIFA ZA UPOTOSHAJI KUHUSU CHUO CHA UFUNDI ARUSHA 8. #8
  Junior Member
  Join Date
  Feb 2015
  Posts
  25
  Rep Power
  0
  Likes Received
  0
  Likes Given
  0

  Re: BARUA YA WAZI KWA MHESHIMIWA JOHN POMBE MAGUFULI - RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO

  Chuo hakina nafsi na maana ya Chuo ni kwa ujumla wake (inclusive: majengo, wafanyakazi na wanafunzi). Neno chuo lingetakiwa kuwa (qualified) lielezwe vizuri lieleweke lisiache maswali. Lakini

  Matatizo yanayodaiwa hayapo chuoni haiwezi kuchukua zaidi ya saa moja kufahamu ukweli vizuri kama yapo au hayapo ikiwa mtu yeyote awe raia wa kawaida au kutoka mamlaka za serikali atatembela chuo kwa njia yake anayojua na kuongea na mfanyakazi mmoja mmoja na pia mwanafunzi mmoja mmoja bila kushirikisha Uongozi wa Chuo.

  Mnyonge mnyongeni lakini haki yake apewe. Kwanini tuandikie mate wakati wino upo? Chuo kina matatizo mengi, yanayohusu ufisadi, matumizi mabaya ya ofisi ya Umma na ukandamizaji kwa wafanyakazi.

  Serikali ikiamua kufuatilia seriously haitachukua zaidi ya siku moja au mbili kufahamu ukweli wote. Tusidanganyike na matangazo yanayofanywa. "Hata mwizi anayekamatwa na mali ya wizi mkononi akifikishwa mahakamani anakana kwamba hakuiba". Hivyo siyo kila kinachosemwa ni kweli na si kila kinachokanushwa ndivyo ilivyo.

  Nafahamu kwamba Rais wetu mpendwa anayo mikono mingi tena mingine ni mirefu sana, ninamwomba kwa heshima na taadhima, kwamba ikimpendeza aseme neno moja tu ili matatizo ya Chuo cha Ufundi Arusha yaweze kuisha. Rais anazo njia nyingi za kuweza kumaliza matatizo ndani ya jamii. Matatizo haya yakiisha, wananchi wako walio chuoni hapa tutaishi kwa amani.

  Kuishi kwetu kwa amani kutatufanya tuweze kufanya kazi kwa ufanisi na tija ili tuweze kulifikisha Taifa kwenye uchumi wa kati kama unavyopenda Mheshimiwa Rais.
  Last edited by SUBIRA; 03-07-2016 at 13:05.

 9. #9
  Member
  Join Date
  Jan 2015
  Posts
  44
  Rep Power
  0
  Likes Received
  0
  Likes Given
  1

  Re: BARUA YA WAZI KWA MHESHIMIWA JOHN POMBE MAGUFULI - RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO

  Quote Originally Posted by TUA View Post
  Mheshimiwa Rais,
  Mimi ni Raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ninakupongeza sana kwa kazi nzuri unayofanya kuhakikisha kwamba wananchi wote wa Tanzania wanafaidi matunda ya Uhuru.

  Mheshimiwa Rais,
  Ninakupongoza na ninakuombea kwa Mwenyezi Mungu ili uendelee kutimiza ahadi yako ya kutumbua majipu kwa kupambana na rushwa, ubadhirifu wa mali za umma na ufisadi nchini kama ulivyolitangazia Taifa kupitia Bunge tarehe 20-11-2015. Ni imani yangu kuwa kama ulivyoahidi katika hotuba yako, ufisadi, ubadhirifu wa mali za umma na rushwa serikalini vitageuka kuwa wimbo uchukizao badala ya wimbo ufurahishao kama ilivyokuwa imezoeleka hapo awali.

  Mheshimiwa Rais,
  Pia ninapenda kuchukua nafasi hii kumpongeza na kumwombea Waziri Mkuu, Mheshimiwa Kassim Majaliwa kwa kazi nzuri sana anayofanya. Kadhalika napongeza watendaji wote uliowateua kuunda Serikali yako katika Wizara mbalimbali ili kukusaidia kufanikisha malengo yako ya kuleta hali bora zaidi kwa wananchi wote wa Tanzania katika maisha yetu ya kila siku.

  Mheshimiwa Rais,
  Ni vigumu kuweza kutimiza ahadi yako ya kupambana na rushwa, ubadhirifu wa mali za umma na ufisadi nchini kama hutapata taarifa sahihi za ni nini kinatendeka katika maeneo mbalimbali ya nchi. Kama Raia wa kawaida tunao wajibu wa kutoa taarifa sahihi za kila jambo lisilo la kizalendo lenye nia ya kuharibu ustawi wa jamii na Taifa. Kwa mujibu wa Ibara ya 27 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ni wajibu wa kila mtu kulinda mali asilia ya Jamhuri ya Muungano, mali ya Mamlaka ya Nchi na mali yote inayomilikiwa kwa pamoja na wananchi.

  Mheshimiwa Rais,
  Chuo cha Ufundi Arusha ni mali ya Mamlaka ya Nchi. Chuo hiki kina dhamana ya kutoa mafunzo bora kwa wananchi wote wa Tanzania. Katika kutekeleza majukumu yake, chuo kimekumbwa na matatizo mbalimbali. Miongoni mwa matatizo yaliyopo ni upatikanaji wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia, upungufu wa malazi kwa wanafunzi, Ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka.

  Mheshimiwa Rais,
  Kutokana na upungufu wa malazi wanafunzi wengi wa kike wanakaa nyumba za kupanga mitaani. Matokeo yake wanafunzi wengi wamepata ujauzito na wengine wengi wameshindwa masomo yao kwa kukosa mazingira rafiki ya kujisomea. Wanafunzi wanaoathirika zaidi ni wanafunzi wanaosoma ngazi ya cheti na stashahada ambao wengi wanatokea kidato cha nne (4) na wengi wana umri wa chini ya miaka 18.

  Mheshimiwa Rais,
  Chuo kingeweza kuondokana na tatizo la upungufu wa malazi kama kungekuwa na nia hiyo. Chuo kilikuwa na matofali zaidi ya 20,000, Chuo kinapata simenti kutoka kiwanda cha Tanga simenti na wanafunzi huwa wanafanya mazoezi ya kujifunza kujenga chuoni. Ni kiasi kidogo sana cha rasilimali fedha kingeweza kutumika kuondokana na tatizo la malazi chuoni.

  Mheshimiwa Rais,
  Chuo huwa kinapata msaada wa simenti tani nane (8) kila muhula kwa ajili ya kuendesha mafunzo kutoka kiwanda cha Tanga simenti. Kadhalika chuo kilikuwa na matofali zaidi ya 20,000 yaliyopigwa chuoni na kubaki katika ujenzi wa jengo la Ujenzi na Umwagiliaji. Kutokana na mazingira yasiyoeleweka, haifahamiki inakokwenda simenti hii ya msaada na pia haikufahamika yalikokwenda matofali yale yote. Mbaya zaidi ni pale ambapo kiasi cha Tsh 1,400,000,000/= zimeonekana kuibwa katika mradi huu wa ujenzi wa Jengo hili la madarasa ambalo lilikadiriwa kujengwa kwa Tsh 2.63 bilioni lakini mpaka sasa limeshagharimu Tsh 4.00 bilioni likiwa bado halijakamilika.

  Inavyoonekana tatizo la malazi liliachwa na kuwa kubwa ili serikali iweze kutenga mabilioni ya fedha kwa ajili ya ujenzi wa mabweni. Kutengwa kwa fedha za ujenzi wa mabweni kungeweza kupelekea kufujwa kama ilivyokuwa kwa miradi mbalimbali ya ujenzi iliyofanyika chuoni kuanzia Januari 2010. Chuo kimekua kikifuja fedha nyingi za umma kupitia kampuni ya chuo ijulikanayo kama ATC-PCB.

  Mheshimiwa Rais,
  Chuo cha ufundi Arusha kina njia mbalimbali za mapato, lakini kwa sasa chuo kinaendeshwa kwa madeni. Upande mmoja wafanyakazi wanadai chuo stahili mbalimbali na kwa upande mwingine wazabuni/wafanyabiashara nao wanadai chuo mabilioni ya fedha kwa huduma mbalimbali walizotoa kwa chuo. Sintofahamu inazidi zaidi pale ambapo haijulikani madeni haya yatalipwa lini na ni nini ilikuwa msingi wa madeni haya.

  Mheshimiwa Rais,
  Kutokana na matumizi yasiyoridhisha ya fedha za chuo, hata wanafunzi wa kozi ya Ujenzi na Umwagiliaji wameshindwa kufanya mazoezi yao inavyostahili. Wanafunzi hao wameshindwa kufanya mafunzo yao sawasawa kwa kukosekana eneo la kufanyia mazoezi (Practical practice). Wanafunzi hawa walitakiwa kuanza kufanya mazoezi hayo kwenye shamba darasa lililopo eneo la Oljoro tangu mwaka 2013.

  Wafadhili mbalimbali walitoa fedha kwa ajili ya kujenga miundombinu ya shamba hilo. Inakadiriwa kuwa kiasi cha TZS 400,000,000/= kilitolewa na wafadhili kwa ajili hiyo lakini mpaka sasa wanafunzi hawajaweza kufanya mazoezi katika shamba hilo na haijulikani ni lini wataanza kufanya mazoezi kwenye shamba hilo. Kwa sasa shamba hilo limegawanywa kwa baadhi ya wafanyakazi wa chuo kwa lengo la kujilimia.

  Mheshimiwa Rais,
  Katika mazingira yenye utata baadhi ya watumishi wa chuo walijilipa mishahara binafsi kuanzia Juni 2010 na haifahamiki ni mamlaka gani zilizowapa mishahara hiyo. Wapo wafanyakazi/watendaji wenye mishahara binafsi serikalini lakini huwa inafahamika ni mamlaka gani zimewapa watendaji hao mishahara hiyo. Kwa mtizamo huo, imefikiriwa kwamba pengine mishahara hiyo ilipatikana kwa njia ya kutumia madaraka vibaya, au kwa kujuana au kwa kuangalia sura zaidi ya sifa ya mtumishi husika. Hali hii imezua manung’uniko na huenda ari ya kazi imeshuka kwa baadhi ya watumishi na pengine utafiti ungefanyika leo ungeweza kuonesha kwamba tija chuoni imeshuka.
  Mheshimiwa Rais,
  Chuo cha Ufundi Arusha kimekuwa na bahati ya kupata vibali vingi vya ajira tangu mwaka 2010 hadi sasa. Serikali kwa nia njema imetaka kuboresha utendaji wa chuo kwa kukiongezea nguvukazi/rasilimali watu. Ni dhamira ya Serikali pia kupunguza tatizo la ajira kwa watanzania kwa kutengeneza nafasi nyingi za ajira iwezekanavyo. Pia ni matumaini ya serikali kuwa ajira zinazopatikana zitashindanishwa kwa haki kwa watanzania wote wenye sifa. Tofauti yake, kwa nyakati tofauti chuo kimetangaza nafasi za ajira lakini sehemu kubwa ya nafasi hizo huwa tayari zina wenyewe na hatimaye waliajiriwa.

  Mwezi Februari 2016 chuo kilitangaza nafasi za ajira. Katika nafasi hizo imefahamika kwamba sehemu kubwa tayari zina wenyewe. Zitakazobaki zitaendelea kujazwa kidogo-kidogo hadi mwaka 2017. Imepangwa hivyo ili baadhi ya walengwa wa viongozi wa chuo waweze kupata ajira hizi endapo hazitatokea zingine, watakapokuwa wamemaliza masomo yao kutoka vyuo mbalimbali wanavyosoma hivi sasa. Walengwa hao wanapewa ajira hizo kwa njia ya kujaza nafasi ambazo mara nyingi zinaitwa “hazikupata watu wenye sifa” na hivyo kuendelea kutangazwa tena na tena mpaka watakapofika kutoka vyuoni. Mpango huu umekuwa kama jambo la kawaida katika chuo hiki, kila nafasi za ajira huchukua zaidi ya mwaka kujazwa zingine zilienda mpaka miaka mitatu.

  Mheshimiwa Rais,
  Chuo cha Ufundi Arusha kwa sasa hakina Mwenyekiti wa Bodi ya Uendeshaji (Bodi ya Uongozi). Kwa mujibu wa sheria iliyoanzisha Chuo cha Ufundi Arusha, Mwenyekiti wa Bodi ni mteule wa Rais. Imekuwa kama ni kawaida sasa kwa Bodi ya Uendeshaji kukutana na kufanya vikao vya Bodi na kulipana posho bila kuwepo Mwenyekiti wa Bodi na bila kibali cha Waziri mwenye dhamana ya Elimu kama itabidi kufanya vikao hivyo.

  Mheshimiwa Rais,
  Mara nyingi Serikali imekuwa ikikaangwa kwa mafuta yake yenyewe. Hii ni kwasababu baadhi ya watendaji wasio waaminifu Serikalini wamekuwa wakihongwa kwa fedha hizihizi za umma zilizopatikana kifisadi na hatimaye kuachia mafisadi kuendelea kuteketeza rasilimali za nchi bila huruma.

  Mheshimiwa Rais,
  Sijaweza kukuona ana kwa ana na pia sikuweza kukufikishia barua hii kwa njia nyingine. Lakini nafahamu kwamba Serikali ina mkono mrefu, na hivyo barua hii itafika kwako. Nia ya barua yangu ni ili uweze kupata taarifa sahihi za mambo yanayofanyika ndani ya Serikali yako mheshimiwa licha ya watendaji walio chini yako kufahamu kuwa mambo ya ufisadi na ubadhirifu wa mali ya umma huyapendi. Ni maombi yangu kwako kuwa, ikikupendeza mheshimiwa agiza ili uchunguzi ufanyike kuangalia kama ni jipu, ikithibitika ni jipu na kama limeiva lipate kutumbuliwa mheshimiwa.

  Mheshimiwa Rais,
  Mimi na Watanzania wengi wenye mapenzi mema tunakuombea maisha yenye Heri na Baraka wewe na wasaidizi wako wote Serikalini.

  Wako mtiifu,

  TUA – Mtanzania Mzalendo

 10. #10
  Member
  Join Date
  Feb 2015
  Posts
  32
  Rep Power
  0
  Likes Received
  0
  Likes Given
  0

  Re: BARUA YA WAZI KWA MHESHIMIWA JOHN POMBE MAGUFULI - RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO

  Leo ni mapumziko kwa ajili ya kumbukumbu ya kifo cha baba wa Taifa na aliyekuwa Rais wa kwanza wa Tanzania Mwalimu Nyerere. Baba wa Taifa anakumbukwa kwa mengi na alilifanyia taifa mambo mengi na ndiyo maana wengi tunamkumbuka na bado tutaendelea kumkumbuka sana. Mapenzi ya watanzania kwa baba wa Taifa si kwa sababu nyingine yoyote, bali kwa uzalendo wake kwa nchi yake.

  Baba wa Taifa aliipenda nchi yake pamoja na wananchi na kwa njia hiyo alifanya elimu kuwa bure ili wananchi wote wapate elimu, Na kwa kufanya hivyo, kila mtanzania alipata nafasi sawa na mwingine kupata elimu. Kwa kutambua kwamba elimu na hasa elimu ya ufundi ni muhimu kwa uchumi wa nchi, alianzisha chuo cha Ufundi Dar es salaam ambacho sasa ni Taasisi ya Teknolojia Dar es salaam (DIT), Chuo cha Ufundi Arusha (ATC), na Chuo cha Ufundi Mbeya ambacho kwa sasa ni Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST).

  Kwa sasa nataka kuongelea Chuo cha Ufundi Arusha (ATC) ambacho kilianzishwa kwa msaada wa serikali ya Ujerumani na ambacho Baba wa Taifa kwa jitihada zake mwenyewe zilisababisha chuo hiki kuanzishwa. Ni bahati mbaya sana kwamba wakati tunaadhimisha miaka 17 tangu kifo cha baba wa taifa, Chuo cha Ufundi Arusha kimedumaa na hakuna dalili zozote kama kitaweza kukua na kustawi kama ilivyo kwa kilichokuwa Chuo cha Ufundi Mbeya au Chuo cha Ufundi DSM.

  Wakati viongozi wa vyuo tajwa hapo juu wakifikiri kwa kina na kwa makini jinsi ya kuvifanya vyuo vyao kuwa bora zaidi na kufanya kile ambacho Taifa linategemea kutoka kwao, hali ni tofauti kabisa katika Chuo cha Ufundi Arusha. Vyuo vinahitaji watu makini, wenye sifa za hali ya juu na utumishi uliotukuka katika Bodi zao lakini kwa chuo cha Ufundi arusha sifa kubwa ya kuwa Mjumbe wa Bodi ni kuwa karibu au na uhusiano na Mkuu wa Chuo kwa njia moja au nyingine.

  Wakati viongozi wa vyuo wanaotaka kuvitoa vyuo vyao kutoka hatua Fulani kwenda hatua nyingine kwa kushirikisha kila mdau, na kufanya mambo yake kufahamika vizuri kwa wadau muhimu, kila kitu ni siri katika chuo cha Ufundi Arusha, isipo kuwa habari za upotoshaji kama ATC yaapa kumaliza tatizo la umeme Tanzania kiapo ambacho hakijawahi kutimia, Ugunduzi wa Helikopta ambao hata andiko la utafiti na majaribio yake hakuna, Kikuletwa kuweza kuzalisha umeme wa maji lakini hakuna kilichofanyika mpaka sasa katika jitihada za kuweza kuzalisha umeme licha ya Serikali ya Norway kutoa fedha kwa ajili ya mradi huo nk.

  Katika hali ya kuficha na kutafuta kila njia za kufanya mambo haya yasifahamike kwa umma imekuwa ni kawaida kwa uongozi wa juu wa Chuo kumtumia anayeitwa afisa uhusiano wa chuo aliyeajiriwa kwa upendeleo maalumu anayeitwa kwa jina la Gasto Leseiyo kununua baadhi ya waandishi wa habari ushwara/makanjanja ili kuandika habari mbalimbali kwenye magazeti na vyombo mbalimbali vya habari kwa ajili ya kuandika habari zisizo za kweli kwa nia ya kupotosha UMMA. Gasto Leseiyo amekuwa pia akiingia kwenye mitandao ya jamii kwa jina la Utemi kwa nia hiyohiyo ya kutaka kuaminisha umma mambo yasiyo ya kweli kwa ajili ya kuficha ukweli na kwa ajili ya kuchumia tumbo.

Posting Permissions

 • You may not post new threads
 • You may not post replies
 • You may not post attachments
 • You may not edit your posts
 •