Gavana wa New Jersy Chris Christie akimuunga mkono Donald Trump


Katika kile kinachoonekana kama hatua ya kushangaza katika kinyanganyiro cha urais nchini Marekani gavana wa jimbo la New Jersey Chris Christie amemuunga mkono billionea Donald Trump katika uteuzi wa chama cha Republican.

Bwana Trump aliitaja hatua hiyo kama aliyokuwa akiihitaji zaidi.Wawili hao walikuwa mahasimu hadi wiki mbili zilizopita wakati bwana Christie alifutilia mbali kampeni yake.

Bwana Christie alisema kuwa Trump alikuwa katika nafasi bora ya kumshinda Hillary Clinton ambaye anatafuta nasafi ya kuwania urais kupitia chama cha Democratic.Hio leo Clinton atatafuta uteuzi katika jimbo la South Carolina ambalo bwana Trump alishinda kupitia chama cha Republican.