Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ akiwa na mwanaye Tiffah.

Exclusive! Baada ya mjadala wa muda mrefu, hatimaye mzazi mwenzake Nasibu Abdul ‘Diamond’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ amekubali kumpeleka mtoto aliyezaa na staa huyo wa Wimbo wa Utanipenda kwa babu yake Abdul Juma waliyekuwa na tofauti naye.

Kwa muda mrefu, Zari anadaiwa kushindwa kumpeleka mtoto huyo (Tiffah) kwa babu yake kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kusapoti bifu la ‘baby’ wake (Diamond) aliyekuwa na tofauti na mzazi wake huyo.

Kwa mujibu wa chanzo kilichopo ndani ya familia ya mama Diamond, bifu hilo limeshamalizika hivyo ndugu wameshamueleza Zari akubali kwenda kwa baba Diamond ili iwe ishara ya kumaliza tofauti zao na kufungua ukurasa mpya.Babaake Diamond.

“Zari amekubali kumpeleka, kilichobaki ni kupanga siku tu. Tena nasikia hata baba Diamond wameshamueleza, ameshaandaa mapokezi ya nguvu ikiwemo dua maalum.

“Baba Diamond hana kinyongo wameshazungumza na mama Diamond wameshamaliza tofauti zao, Diamond mwenyewe hana tatizo kilichobaki ni kwenda tu kule kufanya dua,” kilieleza chanzo.
Baada ya kupata habari hizo, mwanahabari wetu licha ya kumtafuta mama Diamond hakuweza kupatikana lakini baba Diamond alipatikana na kukiri kuwepo kwa mipango hiyo.“Wewe nani kakupa hizo habari? Nyinyi kweli kiboko. Oke, namshukuru Mungu, wameniahidi kuja. Nawasubiri kwa hamu, nimuone mjukuu wangu na mkwe wangu Zari maana namsikia tu kwenye vyombo vya habari. Maandalizi nishayafanya na itabidi tufanye na dua,” alisema baba Diamond.

Diamond aliingia kwenye bifu na baba yake kwa kile kilichodaiwa kuwa mzazi huyo kutomjali staa huyo kipindi alipokuwa mdogo hususan kipindi alipoachana na mama Diamond na kila mtu kuishi kivyake.