Close

Results 1 to 2 of 2
 1. #1
  Moderator
  Join Date
  Apr 2015
  Posts
  1,067
  Rep Power
  7
  Likes Received
  21
  Likes Given
  0

  Mwakyembe apiga Teke katiba asema sio Kipaombele cha serikali ya awamu ya Tano  Dr. Harrison Mwakyembe, Waziri wa Katiba na Sheria amewataka Watanzania wanaoulizia hatima ya mchakato wa katiba mpya kutambua kuwa suala hilo si sehemu ya vipaumbele vya Dk. John Magufuli.

  Mwakyembe amesema hayo jana usiku katika mahojiano maalum aliyofanya na Marin Hassan, mtangazaji wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), juu ya utendaji wa wizara yake katika siku 100 za serikali ya awamu ya tano.

  Waziri huyo alisema kuwa katiba mpya haina umuhimu mkubwa katika maisha ya kila siku ya watu na wala sio kipaumbele cha rais Magufuli kwani ni kiporo tu alichoachiwa na serikali ya awamu ya nne na atakifanyia kazi wakati atakapoona inafaa.

  “Watu wanadhani katiba mpya ndiyo kila kitu, wanaona katiba ni muhimu kuliko kulipia watoto waende shule, wanafikiri katiba mpya ikishapitishwa tu basi kesho yake wataletewa mkate na chai kitandani jambo ambalo sio kweli,” amesema Dk. Mwakyembe.

  Aliongeza kuwa: “Kwa sasa rais bado anafanyia kazi vipaumbele vyake kwanza ikiwemo kusimamia elimu bure, kuongeza kasi ya ukusanyaji mapato ya serikali na kusimamia uwajibikaji wa watumishi wa umma na hivyo kelele za katiba mpya hazina msingi.”

  Katika hatua nyingine, Waziri Mwakyembe alisema Watanzania ambao bado wana ndoto kuwa mchakato wa katiba mpya unaweza kuanzia katika hatua ya kujadiliwa kwa rasimu ya katiba ya Jaji Joseph Warioba kuachana na wazo hilo kwani limepitwa na wakati.

  Alisisitiza kuwa katiba iliyopendekezwa na kupitishwa na wajumbe wengi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni halali kwani ilipatikana kwa mujibu wa sheria na taratibu licha ya kususiwa na wajumbe wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

  Ukawa unaoundwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Chama cha Wananchi (CUF), National League for Demokracy (NLD) na NCCR Mageuzi.

  “Rais alishasema alipohutubia bunge, kwamba kuna kiporo nimeachiwa, sasa mimi nashangaa hawa watu! tena wengine wana shahada za sheria, wanaongea nini? Hatua ya rasimu ya Warioba ilishapitwa na wakati na tayari tunayo katiba pendekezwa,” aling’aka.

  Mwakyembe alihitimisha kwamba utakapofika wakati wa kulifanyia kazi suala la katiba mpya, serikali ya awamu ya tano itaendelea na hatua ya kura ya maoni ya katiba pendekezwa na sio vinginevyo.
  hakikisha hupitwi na habari

 2. #2
  Senior Member
  Join Date
  May 2014
  Posts
  431
  Rep Power
  7
  Likes Received
  34
  Likes Given
  24

  Re: Mwakyembe apiga Teke katiba asema sio Kipaombele cha serikali ya awamu ya Tano

  Mwakyembe, mwanasheria msomi lkn kama wasomi wengi wa nchi yetu walivyoamua kujidhalilisha, haongei jambo jipya kuhusu KATIBA AMBALO WENGI HATUJUI!

  Tunajua Mwakyembe, JPM na ASILIMIA KUBWA YA VIGOGO WA CHAMA TAWALA - CCM hawakuwahi hata siku moja kutaka MABADILIKO YOYOTE YALE YANAYOPIGIWA KELELE NA WANANCHI WALIO WENGI!

  CCM kupitia JK walitekeleza ajenda ya MABADILIKO...KUELEKEA KUPATIKANA KATIBA YA WANANCHI, KWA UZITO WA SHINIKIZO LA UMMA - SI VINGINEVYO!

  HAIKUSHANGAZA BASI KUSHUHUDIA VIGOGO HAO WAKILA NJAMA KUBAKA DEMOKRASIA KWA KUUNDA NDIVYO SIVYO WAJUMBE WA BUNGE LA KATIBA AMBAO WALITEKELEZA DHAMIRA YAO OVU PALE DODOMA KWA KUZIMA MATAKWA YA UMMA WA WATANZANIA NA BADALA YAKE KUBATILISHA KWA KUCHOMEKA KATIBA PENDEKEZWA, AMBAYO KIMSINGI NI ILE ILE, YA CCM, YA MWAKA 1977!!

  KUMBUKUMBU BADO MBICHI KWAMBA JK AKIJUA WAZI KWAMBA HAWAKUWA NA DHAMIRA YOYOTE KUTEKELEZA AJENDA YA WANANCHI YA MABADILIKO WALITEKELEZA MAKAKATI KIUFUNDI KUHADAA UMMA NA DUNIA. JK ALISEMA MAPEMA MCHAKATO WA KUPATIKANA KATIBA UKISHINDIKANA BASI TUNARUDIA KATIBA ILE ILE YA 1977....NA KIMSINGI NDIVYO ILIVYOTOKEA...NDIVYO WALIVYOPANGA...CCM HAWAKUWAHI KUWA TAYARI MABADILIKO KUFANYIKA!!

  RAIS JPM ALIKUWA MJUMBE MMOJAWAPO PALE DODOMA ALIYESHIRIKI UBAKAJI WA MCHAKATO WA KIDEMOKRASIA, KUWANYANG'ANYA WANANCHI HAKI YAO KUFANYA MABADILIKO YA KIKATIBA KWA LENGO LA KUONDOKANA NA UTAWALA MBOVU ULIOSABABISHA NA UNAOENDELEA KUSABABISHA MAJANGA YA UMASKINI NA KIJAMII KATIKA MAISHA YA WATANZANIA WALIO WENGI!

  MWAKYEMBE AFANYE KEJELI ZOTE ATAKAZOFANYA LKN KAMWE HAWEZI KUFIFISHA NDOTO YA UMMA WA TANZANIA KUFANYA MABADILIKO YALE WANAYOYATAKA ILI WAWEZE KUISHI VIZURI KATIKA NCHI YAO NA KUNUFAIKA NA RASLIMALI AMBAZO HAZIJAWEZA KUWANUFAISHA NA KUONDOA HATA ILE MAANA YA MATUNDA YA UHURU!
  Last edited by PAMBAZUKO; 06-06-2016 at 00:12. Reason: clarity

Posting Permissions

 • You may not post new threads
 • You may not post replies
 • You may not post attachments
 • You may not edit your posts
 •