Close

Results 1 to 4 of 4
 1. #1
  Moderator
  Join Date
  Apr 2015
  Posts
  1,067
  Rep Power
  6
  Likes Received
  21
  Likes Given
  0

  NEC yatangaza kuanza mchakato wa kura ya maoni

  Tume ya Uchaguzi ya Taifa (NEC) imesema kuwa mchakato wa kupigia kura za maoni katiba mpya inayopendekezwa umeanza baada ya kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu.  Mwenyekiti wa NEC, Jaji Mstaafu Damian Lubuva amesema kuwa Tume hiyo ilisimamisha mchakato wa kura za maoni kwa Katiba Mpya inayopendekezwa ili iweze kushughulikia Uchaguzi Mkuu na sasa imeurejesha mezani kwa ajili ya utekelezaji.

  “Tulikuwa tunangoja tumalize uchaguzi. Kama vile ambavyo Mnyamwezi anavobeba mzigo, unamaliza mmoja unakwenda kwa mwingine. Sasa tumemaliza uchaguzi mkuu tunakwenda kwa lingine,” alisema Jaji Lubuva.

  Alieleza kuwa mchakato huo unahitaji bajeti kubwa, hivyo wananchi watajulishwa muda ukifika kuhusu hatua zinazoendelea.

  Taarifa hii ya NEC inakuja wakati ambapo vyama vya upinzani vinavyounda Ukawa vimekuwa vikisisitiza kuwa Katiba hiyo irudishwe kwenye hatua za majadiliano ili kuibeba Rasimu ya Tume ya Warioba, huku upande wa Chama Cha Mapinduzi wakionesha kuiunga mkono kwa asilimia zote.

  Wakati akilihutubia Bunge kwa mara ya kwanza, Rais Magufuli alieleza kuwa anatambua kuwa ana kiporo cha Katiba Mpya na kwamba atalisimamia ipasavyo.
  hakikisha hupitwi na habari

 2. #2
  Senior Member
  Join Date
  Jun 2015
  Posts
  722
  Rep Power
  5
  Likes Received
  23
  Likes Given
  1

  Re: NEC yatangaza kuanza mchakato wa kura ya maoni

  Mnataka kula tena mlivyo walafi sitta na wenzie washa tia hasara taif hili kwa katiba Bubu mbona Warioba alisha kusanya maoni ya wananchi na ile ndio Katiba
  punda hajasoma lakini kazi hakosi

 3. #3
  Senior Member
  Join Date
  Nov 2015
  Posts
  133
  Rep Power
  5
  Likes Received
  4
  Likes Given
  2

  Re: NEC yatangaza kuanza mchakato wa kura ya maoni

  wembe n uleule ushindi tuuuu ccm twapeta na tutazidi kupeta hatunaga shida zaidi ya kuwakalisha
  Chama Imara CCM Daima]

 4. #4
  Senior Member
  Join Date
  May 2014
  Posts
  431
  Rep Power
  6
  Likes Received
  34
  Likes Given
  24

  Re: NEC yatangaza kuanza mchakato wa kura ya maoni

  KATIKA SWALA NYETI LA KATIBA HAKUNA USHINDI WA CCM...KUSHANGILIA USHINDI NI UZUZU!

  AIDHA KWA WAPENDA MABADILIKO HASARA HAIKO KWENYE FEDHA...HASARA KUBWA IKO KATIKA ATHARI KUBWA ISIYOMITHILIKA KWA WENGI KWA MAISHA NA MAENDELEO KWA UJUMLA YA WATANZANIA WALIO WENGI!!!

Posting Permissions

 • You may not post new threads
 • You may not post replies
 • You may not post attachments
 • You may not edit your posts
 •