Hali ni tete! Siku chache baada ya nyota wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ kuwasiliba wasanii wenzake kwenye wimbo wake mpya wa Shika Adabu Yako, ameibuka akidaiwa kujisalimisha polisi kufuatia kutishiwa kuuawa na watu asiowafahamu.

CHANZO CHAWEKA WAZI

Kwa mujibu wa chanzo chetu, baada ya kuachia wimbo huo, jioni yake tu, Nay alipigiwa simu na watu asiowafahamu wakimtaka aupotezee wimbo huo kabla haujamgharimu maisha kwa njia yoyote ile.

APUUZA, ATUMIWA MESEJI

Chanzo kilidai kuwa, Nay alipuuzia simu hizo lakini alishangaa ilipofika asubuhi siku iliyofuata, alikuta ujumbe wa maneno (SMS) kwenye simu yake ukiwa na maneno makali na ya kuendelea kumtishia kifo.Naye alikiri kutishiwa kuuawa. Alisema hatua ya awali alichukua uamuzi wa kwenda Kituo cha Polisi Kimara, Dar lakini hakufunguliwa faili la kesi kwa maelezo kuwa, usiku huo askari wasingeweza kufanya hivyo badala yake walimtaka arudi kesho yake.
HUYU HAPA NAY
“Hapa nilipo nimechanganyikiwa. Kwa hali ilivyo nimeona bora niende polisi maana najua nitauawa wakati wowote. Nilikwenda Polisi Kimara lakini sikufanikiwa, sasa najiongeza, nitakwenda Kituo cha Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam (kwa Kamanda Simon Sirro).
Wikienda: “Nimesikia unakwenda Lindi kwenye shoo, sasa huko Polisi Kanda Maalum umeshakwenda au utakwenda ukirudi?”