TAMKO LA VIONGOZI WA DINI WAWAKILISHI KWENYE BUNGE LA KATIBA Inasikitisha kusikiliza kauli ya wajumbe toka Taasisi za Kidini, Ni majuzi tu tumesoma kuhusu Tamko la Jukwaa la Wakristo Tanzania, Tamko hilo lilionyesha kulalamika kuhusu mwenendo wa BMK na wao wametoa masharti karibu sita kuhusu Katiba Mpya. Sasa iweje leo viongozi wetu hawa wa Kiroho watoke hadharani kulalamika kwamba mambo yanapotoshwa. Tunashangaa sana maana taasisi zilizowatuma zilishatoa misimamo yao hadharani kwamba wao walipendekeza kwamba wanataka serikali tatu, lakini tulichoshuhudia wawakilishi hao wao walisema wanataka serikali mbili. Ikumbukwe kwamba maandiko yanatufundisha juu ya Upofu unaosababishwa na Rushwa na usaliti kama alivyofanya Yuda Iskariote. Kwa hali ilivyo sasa Ukweli ni kwamba Watanzania hatudanganyiki, Tutaonyesha msimamo wetu kwenye kura ya Maoni, Mungu awasaidie sana mpate kuelewa hekima ya kawaida tu na Hofu ya Mungu.
Connect With Us